Maono yangu kwa Tanzania baada ya miaka 3 (2019 mpaka 2022)

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,708
8,995
Nimekuja Tanzania kwa likizo baada ya miaka 3 na mpaka sasa nipo hapa na haya ndiyo maono yangu tangu 2019 mpaka leo

Sehemu ambazo zina mabadiliko mazuri

1. Ujenzi kwa ujimla umeongeka hasa airport terminal ya Dar ambayo imepunguza usumbufu sana
2. Urafiki kwa wageni umeongezeka airport sana
3. Watalii wameongezeka

Siasa
1. Mikutano ya CCM imezidi ambayo haina tija. Nilipita huku Ununio dereva wangu ana lalamika mikutano kila siku
2. Rushwa bado ipo kwa watendaji hasa uhamiaji na Nida yaani mfano baada ya kuweka namba yangu kwenye form nimekuwa nikipata simu za wafanyakazi kujaribu kuniomba pesa kwa kisingizio wamenisaidia.
3. Barabara za ndani hata Dar bado sio nzuri. Inashangaza Sinza serikali imeshidwa kuweka barabara za ndani kwenye mitaa na ni mbovu kuliko 2019.

Mangine

1. Uwezo wa Tanzania kwenye huduma za afya umeongezeka sana. Magojwa ya kichunguzi kama cancer wanajagundua mapema kuliko zamani
2. Watoto chini ya miaka 18 ni wengi sana sana Tanzania
3. Usafi umeongezeka kiasi mfano sasa kwenye bar wameweka vyoo vya haja ndogo tofauti na kubwa na kusababisha usafi kuongezeka
4. Mfumuko wa bei bado upo lakini pesa hasa kwa wafanyakazi ipo kulinganisha na 2019. Malalamiko yame pungua sana

Nitaendelea kuongeza weekend hii naenda Arusha
 
Back
Top Bottom