Maono: Nguvu ya kujua yajayo kupitia sauti ya roho takatifu: Clairaudience

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,494
Katika makala hii nitazungumzia nguvu nyingine ya muujiza moja kati ya nguvu za miujiza walizonazo watu wengi ambayo ni Clairvoyance;

Hii ni moja kati ya nguvu za miujiza ambayo wenye nayo huitwa clairvoyants hawa hutambulika kama watu wenye uwezo wa kuona yajayo;

Chochote kinachohusu jambo linalokuja kuhusiana na mtu,kitu au eneo.

wenye uwezo huu wengine huwaita walii yaani vipenzi vya mwenyezi Mungu.

Hapa nitakuelezea juu ya nguvu ya miujiza walionayo watu hawa huenda wewe pia unayo lakini hujifahamu.

Clairvoyance:
ni uwezo ambao mtu huwa nao ambao humsababisha kuweza kuona yanayokuja mbele yaani fikra au maono yake yana kuwa na uwezo wa kuona yajayo (future).

unachotakiwa kuelewa kwanza neno hili ‘clairvoyance’ limetokana na lugha ya kifaransa kwa maana ya utengano wa maneno mawili yaliyoungana yaani clair na voyance ikiwa na maana kwamba neno ‘clair,’ ni clear kwa lugha ya kingereza ambapo kiswahili tunasema ni wazi hivyo kivumishi chake kinakuwa ni -eupe na kitenzi chake ni safi au safisha,

kwa wataalamu wa kiswahili watakuwa wanafahamu naongelea nini na voyance ni vision kwa kingereza ambayo kwa kiswahili ni maono.

Hivyo basi;
Kwa maana nyepesi ni kwamba Clairvoyance ni maono ya wazi au maono meupe yasio na doa au shaka ingawa imegawanyika katika vipengele tofauti tofauti vya kuweza kuona yajayo sasa kuna matawi ya Clairvoyance lakini hapa tutaanza na clairaudience;





ambapo;

Clairaudience;
Maana yake ni kusikia kwa uwazi yaani nguvu ya miujiza yenye kumuwezesha mtu kuweza kusikia sauti kutoka kwenye ulimwengu wa roho kama vile wanyama wanavyoweza kusikia sauti za watu makaburi basi kuna wanadamu pia wamejaliwa uwezo huo.


Clairaudience ni nguvu ya kiroho ambayo humsaidia mtu katika kuwa na uwezo wa kusikia sauti kutoka nyanja na muelekeo tofauti na dunia hii tuliopo yaani kusikia upande wa pili au kwa maneno mengine tunasema dunia ya kiroho iliyopo na huwa ni uwezo wa kusikia sauti za roho takatifu yaani roho zilizojikita katika utukufu wa kumtukuza Mungu na Masters ambao wanachomoza kutoa taarifa kutoka ulimwengu wa roho. Pia ni uwezo wa mtu kusikia umbali usiokuwa wa kawaida

Clairaudience pia inajumuisha maono,muongozo na hekima kutoka katika utakaso wa roho yako mwenyewe na kuwa na uwezo wa kuwa sahihi katika kusikia ushauri wa roho na maono yake.

Katika dunia ya leo nguvu hii watu wengi utawakuta ni wenye kujisifu wanayo na kila mtu utakuta anajitahidi kuiendeleza hata kama sio majaliwa yake na kuanza kutumia njia tofauti tofauti zisizofaa katika kuiamsha na kukuta anakuwa laghai na mtumwa wa shetani au mashetani.

Clairaudience ni moja kati ya nguvu kubwa sana za miujiza ambayo mtu yoyote anaweza kutamani kuwa nayo…
maana huweza kumnufaisha mtu aliyonayo na watu wanaokuzunguka kwa sababu katika faida zake ni kuweza kujua yajayo na watu wengi huwa na tamaa ya kuweza kujua mambo kabla hayajatokea.

Kwa maneno mengine,
watu ambao wameikomaza nguvu hii ya miujiza ni watu wenye uwezo mkubwa wa kusikia na kupokea jumbe mbali mbali kutoka katika ulimwengu wa kiroho ikiwa ni kutoka kwa malaika,majini,wanyama,roho za watu waliokufa au hata kupokea ushauri wa Mungu kupitia malaika wake.

Na hii kwa watu wengi wasio na maana wala hekima kwao ni simulizi na mambo ya kusadikika kwa maana ni kitu hawajawahi kusikia wala kuona na hata sehemu wanazokuwa wameona ni kwenye Movies na Misalsal yaani Series tofauti tofauti hivyo wanakuwa wanaamini kuwa hakuna kitu kama hicho. Hao ni wale ambao hawana tofauti na wale ambao hawakuamini mifano na watu waliopita kabla yao.

Kuokoa muda na kutofanya maelezo yawe marefu kwanza kabisa tuanze kwa kuangalia ni jinsi gani utajijua kama una nguvu hii ya clairaudience:

Dalili za mtu mwenye clairaudiance ni kama ifuatavyo:

1. Utakuwa na tabia ya kuongea peke yako:
Ikiwa ni mtu ambaye unapenda kuzungumza ukiwa peke yako na huwa ni mtu wa kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe pamoja na kujishauri mwenyewe, halafu kujiliwaza mwenyewe basi tambua moja kwa moja una dalili ya kwanza kati ya dalili zinazo muonyesha mtu mwenye kipawa cha Clairaudience.


2. Dalili nyingine ni kama wewe ni mtu wa kujifunza zaidi kwa kupitia kusikiliza kuliko kusoma au kuangalia basi una dalili nyingine ya Clairaudience
Pia kama una tabia ya kushindwa kuwa makini katika kusoma au kujihisi uzito kujibu ujumbe wa maandishi,
kusinzia ukitizama movies au vipindi vya televisheni
na kama ni mtu ambaye unapenda kuhifadhi kitu kwa kutumia kusikiliza kuliko maandishi

kama una tabia ya usikivu na kupenda zaidi kusikiliza kuliko kutumia milango mingine ya fahamu basi unategemewa zaidi kuwa na uwezo wa Clairaudience.

3. Dalili nyingine ukiwa ni mtu wa kuchukia sauti kubwa au mtu kuongea sauti kubwa au sauti ya ghafla ikitokea na unajihisi mwili kusisimka au kuchanganyikiwa ukiskia sauti mfano mtu mwenye hyperacusis na ni mtu mwenye kupenda ukimya zaidi na utulivu hii pia ni dalili ya mtu mwenye clairaudience.

kama unajikuta ni mtu wa kutaka kupumzika au kutamani kuondoka sehemu kelele zikianza, au kama kelele zinakufanya usikie hasira na kukosa amani, na kama ni mtu wa kupata maumivu laini ya kichwa ukiskia kelele, basi kama una dalili hizi jua una nguvu hii ya miujiza ya usikivu.

4. Dalili nyingine kama ni mtu wa kupenda kukaa peke yako na kukaa kimya kwa muda kunakufanya ujihisi amani na kama unahisi kelele na maneno maneno au kubishana na watu kuna kukosesha amani na pia ukikaa peke yako lazima uondoke na kitu kama ujumbe au wazo na kama ukikosa muda wa kukaa peke yako unajihisi kuna kitu unakosa basi hii ni aina nyingine ya dalili za mtu mwenye Clairaudience

5. Dalili nyingine ni kama unasikia maskio yanavuma au kulia kama mdudu wakati mwingine
kama huwa unahisi maskio yanapiga pia au kuskia mtu anakuita the moment unataka kulala au sauti unaskia na mwingine anasema haskii basi una nguvu hii ya clairaudience na wale wenye nayo basi mara nyingi huwa ni watu ambao wakisema maskio yaache kupiga au kuskia sauti za upande wa pili basi hutokea kimya vilevile hawani watu ambao kama umewahi kuwaona shule mara nyingi akisema jambo kwa hisia basi darasa zina hukaa kimya na wanafunzi wengine husema shetani kapita yaani hutokea kimya cha ghafla na yeye hujikuta ndio wa mwisho kusema neno. maana hao ni watu ambao kero ikizidi maskioni kwa sauti za maongezi basi huamuru kimya kipite.

6. Dalili ya sita ni kama unaskia mazungumzo ya watu kutoka umbali fulani ambao sio wa kawaida na kuskia sauti za watu ambao hawapo karibu yako. Basi hii mara nyingi huwa roho za upande wa pili zinakuwa zinajaribu kukusemesha.

Na kama huwa unaskia sauti zinazungumza na hupati kutambua maneno yanayozungumzwa basi hii ni dalili nyingine ya mtu mwenye nguvu hii ya miujiza pia unaweza kuomba kutafsiriwa na roho lugha ambayo mtu unakuwa huielewi.

7. Dalili ya saba kama ukitizama kwenye Televisheni au radio na kuskia ujumbe ambao unakuwa kama unakusemesha wewe moja kwa moja na kama unaskia ni ujumbe unaokujia kwa sababu tu ya jambo lililokutokea muda mchache uliyopita basi una nguvu hii ya Clairaudience.

jitahidi kuwa unaandika chini maneno yanayokuja au sauti zinazotoka kwenye maskio yako ambazo sio za ulimwengu wa nyama kuwa unaandika ukisoma ujumbe mzima basi utaona kabisa ni maelekezo unapewa.

8. Dalili ya saba ni kama kauli za Mungu kutoka kwenye vitabu vyake kama Qur'an,torati,Injili,Zaburi,Biblia na muziki ni kitu pekee kinachotuliza roho yako au mashairi au simulizi ukisikiliza unakuwa unapata nguvu na kama ni mtu wa kustick kwenye Ayah au kifungu kimoja au mziki mmoja kwa muda mrefu na hutaki kubadilisha basi ni dalili nyingine kubwa za mtu mwenye nguvu hii

Hizi zote ni dalili za mtu mwenye nguvu hii ya miujiza ambapo tukienda kwenye dalili ya nane tunasema.


Metaphysical.jpg



9. Kama wewe ni mtu ambaye watu wanakusifu kwa usikivu na watu hukufuata kwa ajili ya ushauri nasaha na kama ni mtu mwenye uchungu mkali kwa mambo yanayozunguka familia au mkusanyiko wa kikundi cha marafiki zako au umoja wenu unakutegemea wewe pia na kama ni mtu mwenye kufundisha watu bure na kuwaelekeza mambo bure hata kama watu wana kushauri kuwa unalipisha huduma yako na kama ni mtu mwenye kupenda zaidi kuachia wengine wazungumze na wewe ukae ukiskiliza basi jua kabisa pia una dalili nyingine ya Clairaudience

10. Dalili ya tisa ni kwamba unakuwa ni mtu wa kusikia ushauri au kupewa ushauri kutoka katika kichwa chako mwenyewe kuna kuwa kama kuna mtu anaongea kukusemesha na kukupa ushauri nao ukiufuata unakuwa ni wenye faida basi moja kwa moja una dalili nyingine ya Clairaudience.

11. Dalili ya kumi ni kuwa na uwezo wa kusikia yale ambayo wengine wanakuwa hawasikii mfano wake ni pale ambapo unaona kwa mbali watu wanazungumza na husikii badala ya kuangalia unawageuzia sikio lako nayo pia ni dalili nyingine ya mtu mwenye nguvu hii.

Kama una nyingi ya dalili hizo nilizotaja hapo basi moja kwa moja una nguvu hii na ulikuwa hujitambui sasa ni nafasi yako ya kujijua na kuweza kujitambua na kujifunza jinsi ya kuweza kuiamsha nguvu hii na kukusaidia katika mambo mbali mbali.

FANYA YAFUATAYO KUWEZA KUIMARISHA NGUVU HII
Kwa maelekezo jinsi ya kufanya na kuimarisha nguvu hii na faida zake unaweza kutizama video hii humo nimeelezea pia na sehemu yako ya ubongo inayoweza kukufanikishia nguvu hii na kama unataka pia kwenda kiroho zaidi nimeelezea pia malaika ambaye anaweza kukusaidia kufungua nguvu hii.



Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
 
Watu wenye tabia hizo sisi huku huwaita ni waganga wa kienyeji au watabili,watu hawa wanakipawa cha kuijua kesho,anaweza akaliona jambo,halafu kesho yake akawaita wana kijiji na kuwaambia kitakachotokea,hawa watu huwa ni watu kama wenye mawazo mengi,mnaweza kuwa mnaongea nae,lkn yeye gafra akawa kama anasinzia,ndani ya dakika hata tano tu,anakuwa ameonyeshwa jambo zito analoweza kulielezea kwa mda wa saa nzima,
 
Watu wenye tabia hizo sisi huku huwaita ni waganga wa kienyeji au watabili,watu hawa wanakipawa cha kuijua kesho,anaweza akaliona jambo,halafu kesho yake akawaita wana kijiji na kuwaambia kitakachotokea,hawa watu huwa ni watu kama wenye mawazo mengi,mnaweza kuwa mnaongea nae,lkn yeye gafra akawa kama anasinzia,ndani ya dakika hata tano tu,anakuwa ameonyeshwa jambo zito analoweza kulielezea kwa mda wa saa nzima,
Good point mkuu
 
Toa details zako jina lako na la mama tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa
Mwishoe utaniambia niandae Na jogoo mwekundu...Huyo jini hawezi kuyajua hayo?
Kama Majini Wana mauwezo kama mnavyowasifia aje Kwa kuangalia ID ya JF Tu ...
Info zangu Ni privacy yangu lakini kama jini wako yupo hatoitaji vikolombwezo vyote hivo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom