Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Nimeisoma mara mbilimbili sheria ya mabadiliko ya katiba iliyosainiwa juzi na rais na kugundua kuwa composition ya wajumbe ilivyo itapelekea kuvunjika kwa Muungano. Nitafafanua.
Kwa mujibu wa sheria hiyo wajumbe wa tume wanatakiwa kuwa sawa 50-50 kutoka pande zote hivyo kuwapa wajumbe kutoka Zanzibar nafasi nzuri ya ushawishi wakati wa kutoa maoni kudai nchi yao ipewe madaraka kamili kama nchi. Hali hii itaendelea kuwepo hadi kwenye bunge la katiba.
Kwa mujibu wa sheria hii bunge maalum la katiba litakuwa na jumla ya wajumbe 595, na kati yao angalau 219 watatoka Zanzibar ambao ni sawa na 37% ya wajumbe wote hivyo kuwafanya wawe na uwezo wa kupata walichokuwa wanakitafuta kwa muda mrefu, na safari hii wakifanya makosa tena hawatakipata kwa muda mrefu ujao.
Kwa mtazamo huu wa sheria hii ni dhahiri kuwa wazanzibari wataondoka na Nchi yao na hivyo kupelekea Muungano uliodumu kwa takriban miaka 50 kuvunjika rasmi.