Maoni yangu kuhusu tatizo la ajira kwa vijana Tanzania

Jun 10, 2014
30
5
FAHAMI MATSAWILY JUMA
fahamijuma@yahoo.com facebook:fahami matsawily
twitte:fahami matsawily
phone: 0717262629


TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA TANZANIA


Tatizo la ukosefu wa ajira ni suala ambalo limeendelea kuwatesa vijana katika nchi yetu licha ya takwimu za uchumi wa Tanzania kuonesha kukua kwa wastani wa asilimia 7.1 na kufanya vizuri katika kipindi cha muongo mmoja uliopita lakini umaskini haujapungua kama ilivyotegemewa kwa wananchi

pia uchumi umeshindwa kutengeneza ajira zenye tija inawezekana tatizo ni sera zetu na mikakati yetu kama mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
pamoja na serikali kuwa na program na mikakati mbalimbali iliyolenga kuwawezesha wananchi wenye vipato vya chini kupitia Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi lililoundwa kwa sheria Na 16 ya mwaka 2004.likiwa na dhamana ya kusimamia,kuratibu shughuri zote za uwezeshaji wananchi.

mfano 1.mfuko wa wajasiriamari 2.mfuko wa maendeleo ya vijana 3.mabilioni ya Jk, 4.mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi 5.mfuko wa uwezeshaji wa wajasiriamari 6.mfuko wa maendeleo ya vijana 7.mfuko wa pembejeo za kilimo 8.mfuko wa wanawake 9.mfuko wa uwezeshaji wa wajasiriamari wadogo wadogo 10.mfuko wa maendeleo ya jamii. n.k

mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA 1,11),mpango wa kurasimisha mali na biashara (mkurabita), mpango wa kuboresha mazingira ya biashara (mkumbita)
lakini bado kuna changamoto ya walengwa (targeting group ) ili kuwasaidia wanaohusika pesa hizi zinapelekwa kwenye makundi/watu machache pia kukosekana kwa chombo maalum cha kusimamia mikakati hii (target gruop)
Pia pamoja na kuwepo kwa utitiri wa mabenki hapa nchini karibu zaidi ya 45 bado wananchi maskini wa vijijini na mijini sio marafiki wa mabenki haya kwani hawajanufaika na huduma za mabenki kutokana kuwa na viwango vikubwa vya riba na masharti magumu pia kutokana na kutokuwepo kwa sheria ya saccos (saccoss act) zimeanzishwa saccoss nyingi sana ambazo zimewatia matatizoni wananchi wengi kwa kuuziwa mali zao kutokana na hizi saccoss kuwa na riba kubwa na masharti magumu.

kundi kubwa linaloathirika ni la vijana kwa sababu hawana asseti, au dhamana za kuchukulia mikopo ikizingatiwa kuwa karibu asilimia 90 (90%) ya ardhi ya nchi yetu haijapimwa nchi nzima.

nchi nyingi duniani zipo kwenye marekebisho ya sera na mikakati ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kupunguza umaskini. kukua kwa uchumi usio shirikishi hakuwezi kutatua tatizo la umaskini na ajira kwa vijana.
mfano nchi ya Nigeria ndio nchi inayoonekana kuongoza katika bara la Afrika kwa uchumi wake kukua ambapo wastani wa pato lake la ndani ni karibu dola za marekani bilioni 500 huku pato la mtu mmoja mmoja nchini Nigeria ni USD 2688 wakati huo tatizo la ajira ni 23.9%
huko Afrika ya kusini ambalo linaonekana kuwa Taifa la pili kwa uchumi na takwimu hizo zinazoonyesha wastani wa pato lake la ndani ni USD bilioni 350 huku pato la mtu mmoja mmoja Afrika kusini ni dola za marekani 7336 kwa wakazi wake karibu milioni 48 wakati huo inakabiliwa na tatizo la ajira kwa asilimia 24 (24%).

Tanzania takwimu za ukosefu wa ajira zinaonyesha tatizo la ajira ni asilimia 11.7 (11.7%) nimeyasema haya ili nieleweke vizuri kuwa pamoja na kuongezeka kwa wastani wa pato la ndani ya nchi na kukua kwa uchumi kama shughuri za uzalishaji hazitahusisha idadi kubwa ya wananchi ni dhahiri kuwa tatizo la ajira na umaskini unaweza kubaki palepale.
tusipokuwa makini pia uchumi wetu unaweza kukua lakini wananchi wakawa maskini na tatizo la ajira likawa palepale.nchi nyingi duniani zipo kwenye marekebisho ya sera na mikakati ya kupunguza tatizo la umaskini na tatizo la ukosefu wa ajira.Tanzania tunapaswa kulichukulia suala hili kwa uzito wa kipekee kwa mustakbari wa vijana wetu.

mfano nchi ya kenya mwaka huu wa bajeti yake ya Ksh trilioni 8.1 2014/2015 imetenga ksh bilioni 1.8 sawa na sh. bilioni 32.4 za kitanzani kwa ajili ya mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa vijana. ambapo mfuko huo unasimamiwa na baraza la vijana Taifa la kenya (the national youth council of kenya) na wizara husika. Tanzania kwenye bajeti yetu tumetenga shilingi ngapi kwa ajiri ya vijana na zinaweza kusimamiwa na naniii????
Ajira ni shughuri yoyote ya halali inayompatia mtu kipato. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB) na Shirika la kazi Duniani (ILO) Tatizo la ukosefu wa ajira tunaweza kulitazama katika namna tatu (3). mfano katika nchi yetu ya Tanzania tofauti na nchi nyingi Duniani aina zote hizi 3 bado zimeendelea kuota mizizi na kuendelea kuwatesa sana wananchi wetu.
1.Ajira isiyotoa kipato cha kuridhisha
2.Ajira isiyokidhi matarajio
3.ukosefu wa ajira jumla (jobless)

1. Ajira isiyotoa kipato cha kuridhisha.
hili ni kundi la wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu na ya muda mrefu kwa malipo kidogoukilinganisha na kazi wanayofanya kundi hili huwesabiwa katika kundi la ukosefu wa ajira duniani kote mfano. vijana wanaokota makopo (plastic),wanaofanya kazi viwandani,migodini,vibarua (manual work)

2.Ajira isiyokidhi matarajio
kundi hili linajumuishwa kwenye kundi la ukosefu wa ajira japo linataka kufafana na kundi la kwanza ila tofauti yake ni hili kundi la wafanyakazi wanaofanya kazi halali za kutumia Taaluma,ujuzi,kipaji, nguvu na maarifa waliyonayo katika kufanya kazi lakini malipo wanayopata hayakidhi matarajio yao.

mfano wa wafanyakazi katika kundi hili ni kama: wafanyakazi wa majumbani,bar,hoteli,migahawa,walinzi binafsi,wafanyakazi wa migodini,viwandani,makampuni binafsi, madereva wa vyombo vya moto mfano malori,mabasi,binafsi,n.k
wafanyakazi hawa asilimia 80 (80%) wanafanya kazi bila mikataba ya kazi. Athari yake hulipwa mshahara kidogo pili huwa hatarini kupoteza maslahi yao pindi ajira yao inapostishwa ghafra au kufariki tatu hukosa fursa ya kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (social security) kwa maslahi yao ya baadae.

Hapa pia kuna kundi la wafanyakazi wa vipaji kama: wasanii wa muziki,filamu,ngumi,mpira,vichekesho,sarakasi,mitindo n.k hawa wanafanya kazi kubwa lakini ujira wa kazi zao haukidhi matarajio yao kutokana na urasmu,wizi wa kazi zao au kunyonywa na wadhamini wao.
katika kundi hili pia hata wafanyakazi wa serikali huangukia kundi hili kama: Walimu, wauguzi, wafanyakazi kwenye mashirika ya umma,n.k.
wafanyakazi hawa hufanya kazi kwa kujituma ili wapate ujira utakaokidhi matarajio yao lakini hali huwa tofauti kwani ufanya kazi hadi uzeeni bila kuwa na maisha yenye maendeleo kama matarajio yao kutokana mishahara kidogo kulinganisha na hali halisi ya uchumi wa wakati husika. mfano mfumuko wa bei,thamani ya shilingi, n.k

Pamoja na kuwepo kwa sera ya Taifa ya ajira ya 2008, sheria ya ajira na mahusiano kazini Na.6 ya mwaka 2004 na sheria ya Taasisi za kazi Na.7 bado hali sio nzuri kwa mujibu wa takwimu zinaonesha Tanzania ni nchi ya 6 Duniani kwa kulipa mishahara ya chini.

3.Ukosefu wa ajira jumla (jobless)
Takwimu za ukosefu wa ajira nchini bado haziridhishi kwani taarifa zinaonesha kuwa tatizo la ukosefu wa ajira ni asilimia 11.7 kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 na zaidi tofauti na matarajio ya MKUKUTA ambao ulipanga kushusha asilimia ya ukosefu wa ajira mpaka asilimia 6.9 ifikapo mwaka 2010 Hali inazidi kuwa tete siku hadi siku kutokana na idadi ya vijana ambao hawana ajira kuongezeka.

Kwa Taarifa ya shirika la kazi duniani ya mwelekeo wa ajira kwa vijana ulimwenguni [GrobaL EmpLoyment Trend for youth] inaonesha kuwa Tatizo la ajira kwa vijana Tanzania wenye elimu kuanzia sekondari na kuendelea ni kubwa kuliko wale wenye elimu ya kiwango cha chini.
Aidha watanzania wenye elimu za chini wamepata ajira lakini ajira zao ni duni ama kipato cha chini na za mazingira hatarishi kama sehemu mojawapo ya kuwatumikisha kwa kuwa uelewa wao juu ya masuala sheria na taratibu za kazi ni mdogo.

Hii ni ishara kuwa pamoja na Taifa kuzalisha wasomi wa ngazi za juu kwa idadi kubwa lakini bado soko la ajira halijawapokea wasomi hao wengi wao wapo mitaani wanataabika.

sekta isiyo rasmi inaweza kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini kama ushauri wangu utafanyiwa kazi mfano sekta ya kilimo,ufugaji,uvuvi, huduma(hoteli,migahawa,bodaboda,n.k), biashara(machinga,mamantilie,wafanya biashara wadogo na wakubwa)
mfano kilimo:Tanzania imejaliwa kuwa na hekta millioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo lakini ni asilimia 23 tu ndiyo inayotumika. pia kuna hekta millioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia 1 (1%) tu ndiyo iliyo chini ya umwagiliaji.

karibu asilimia 70 (70%) ya ardhi ya ukulima wa mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono, asilimia 20 kwa kutumia maksai na asilimia 10 kwa kutumia trekta.wakati huo bado kilimo kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua. pamoja na serikali mwaka 2010 kutangaza program yake ya "kilimo kwanza" bado sekta hii inakabiliwa na changamoto kubwa sana.

program ya kilimo inayofaa ni ile ambayo inazingatia kutenga si chini ya asilimia 12 (12%) ya bajeti kwa ajiri ya kilimo kuendana na maamuzi ya viongozi wa nchi za umoja wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika kusini (SADC) yaliyotolewa nchini Msumbiji au maarufu makubaliano ya maputo (maputo protocal) mwaka huu wa bajeti 2014/2015 serikali imetenga sh bilioni 1,084.7 sawa na asilimia 5.46 (5.46%) bado hatuendani na makubaliano ya maputo protocal.

Ufugaji na uvuvi: Tanzania ni nchi ya pili Afrika baada ya nchi ya Sudan (Sudan kusini ikijumuishwa) kuwa na wingi wa mifugo wakati tunapata uhuru tulikuwa na mifugo karibu milioni 8 na sekta ya ngozi ilikuwa ni ya 5 katika mazao muhimu iliyoliinglizia Taifa fedha za kigeni kutokana na mauzo nje ya nchi.

Hivi sasa nchi yetu ina ng'ombe milioni 22.8, mbuzi milioni 15.6, kondoo milioni 7 na kuku zaidi ya milioni 38. Bahati mbaya thamani ya mifugo mingi kiasi hicho haijajitosheleza kibiashara na mchango wa sekta hii katika pato la Taifa kwa sasa ni mdogo sana ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Uvuvi: Tanzania ina pwani yenye rasilimari nyingi ya uvuvi.ina mwambao wa bahari wenye kilomita za mraba 64,000 pamoja na kilomita nyingine za mraba 223,000 za eneo la uvuvi bahali ya Hindi nchi yetu ina maziwa, Bahari, mito na mabwawa kama chanzo cha uvuvi.
lakini sehemu kubwa ya samaki wanaovuliwa hutumika ndani ya nchi kama kitoweo na kiasi kidogo husafirishwa nje ya nchi. Tanzania bado haijatumia ipasavyo hazina yake kubwa iliyojaliwa na Mungu katika sekta ya uvuvi.

TUTATATUAJE TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA TANZANIA???

1.AJIRA ISIYOTOA KIPATO CHA KURIDHISHA
kundi hili linahitaji msaada wa karibu ili kulinda maslahi yao. ni kundi linalofanya kazi kubwa malipo kidogo. linaweza kusaidiwa kama:
1.mfumo wa elimu lazima ufumuliwe upya ili elimu inayotolewa kwa wanafunzi iendane na mahitaji ya nyakati za sasa za kijamii, kiuchumi na kisiasa hasa upande wa mitaala.

Elimu isimamiwe na chombo kimoja tofauti na sasa sekta ya elimu ipo chini ya wizara tatu(tamisemi,utumishi,wizara ya elimu) pia ni muhimu tuwe na mjadala wa kitaifa juu ya lugha ya kufundishia mimi nina mapendekezo 2.
moja tunaweza kubadilisha mitaala yetu ya shule za Awali na msingi lugha ya kufundishia ikawa ni english kama shule za Academic (private) kuanzia darasa la kwanza ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanapoanza kidato cha kwanza kutumia muda mwingi kujifunza lugha mpya ya english kutafsiri maarifa suala ambalo limekuwa gumu kuwapelekea kukariri kile alichoandika mwalimu badala ya kuelewa [The students are not called upon to know but to memorize the contents narrated by teacher]

Pili tunaweza kufundisha masomo yote kwa lugha ya kiswahili na lugha ya english ikawa ni lugha ya lazima kunzia chini hadi chuo kama lugha ya mawasiliano duniani na kwa sababu china hawauzi kichina au japan hawauzi kijapani wanauza ujuzi na maarifa hapa kwetu Tanzania wanafunzi wetu wameshindwa kupata maarifa na ujuzi kwa sababu ya lugha lazima tuchukue maamuzi magumu na ya haraka ili kuinusuru Taifa letu.

2.elimu ya ujasiliamali mdogo mdogo
3.mikopo katika makundi madogo madogo isiyo na riba
4.msaada wa kisheria kulinda kazi zao (baraza la Taifa la vijana).
5.sera ya ajira ipitiwe upya na zile kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa zilindwe kwa nguvu ya kisheria na kisera na hapa kinahitajika chombo makini cha kusimamia hilo.

2.AJIRA ISIYOKIDHI MATARAJIO
kundi hili linanyonywa kupitia mikataba,kufanya kazi bila mikataba,malipo kidogo,kazi zao kuibwa kutokana na udhaifu wa sheria na usimamizi mbovu.
kundi hili linaweza kusaidiwa kama:

1.wafanyakazi wa majumbani,bar,migahawa,madereva, hoteli, hawa lazima wafanye kazi kwa mikataba iliyosainishwa serikali za mitaa kwa kuwa wanatoka sehemu mbalimbali ili mishahara yao ijulikane ni kiasi gani wanalipwa, pili pindi wanaposimamishwa kazi au kufariki watakuwa na nguvu za kisheria kudai malipo yao tatu watakuwa na fursa ya kujiunga na kunufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii (social security)
mfano wafanyakazi wa ndani,bar,migahawa akifanya kazi yenye malipo ya mshahara angalau wenye kima cha chini kabisa sh elfu 80 kwa mwezi baada ya miaka 3 atakuwa na kiasi cha milioni 2.8 huyu mtu tayari atakuwa na mtaji anaweza kufungua bar,mgahawa wa kwake mwenyewe au biashara yoyote.
2:mikopo ya muda mfupi na mikopo ya muda mrefu. mfano tutoe mikopo kwa vijana wenye vipaji lakini wamekwama kwa sababu ya mitaji.

mfano 1.wasanii filamu,muziki, 2.wachezaji wa sinema, sarakasi, mpira wa netibori, miguu, tenesi, pooL, 3.maonyesho ya ngumi, mitindo, riadha wakimbiaji, wachekeshaji (comedy) n.k makundi yote haya ni lazima yapatiwe mikopo ili watimize ndoto zao na ili tupanue wigo wa ajira kwa vijana nchini.
3.licha ya kuwepo sheria ya kazi na mahusiano kazini na sera ya ajira hiyo haitoshi vijana wanahitaji chombo (baraza) kitakachofuatilia na kusimamia utekelezwaji wa sheria na sera hizi kila siku vyombo vilivyopo vimeshindwa kabisa.

UKOSEFU WA AJIRA JUMLA (JOBLESS
wataalam wa masuala ya uchumi wanasema serikali haitoi ajira bali uchumi ndio unatoa ajira (job are created by economy) hapa Tanzania takwimu zinaonesha sekta rasmi huchukua takribani asilimia 2.8 (2.8) ya ajira na sekta isiyo rasmi ndiyo inayotoa ajira kubwa na pana imekuwa mhimili kwa kutoa mchango muhimu sana katika ukuzaji wa kipato,kupunguza umaskini,ukuzaji wa ajira na kuimarisha pato la Taifa kwani sekta isiyo rasmi inachangia kati ya asilimia 35-40 ya GDP.

hivyo sekta isiyo rasmi inaweza kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini. mfano kilimo,ufugaji,uvuvi,huduma,biashara,burudani, n.k zikitengenezewa mazingira mazuri ya kisera na mikakati mizuri.
1: Wafanya biashara ndogo ndogo (Machinga): Yatengwe maeneo maalumu ya wafanya biashara wadogo wadogo (machinga) katika miji katika kutekeleza hilo serikali ishirikiane na wamachinga wenyewe katika kupanga maeneo ya kufanyia biashara pamoja na kuwawekea miundombinu muhimu katika maeneo hayo ya biashara.

Na sio serikali kupanga mipango yake na kuwaletea watekeleze huo ni ubabe na hauna tija kwa Taifa kwani unaibua migogoro ya mala kwa mala kati ya serikali na wafanya biashara wadogo wadogo.
Eneo hili likiwekewa sera shirikishi na mikakati shirikishi litaajili idadi kubwa ya vijana na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini.
2: Boda boda: sekta hii nayo pia imeajili idadi kubwa ya vijana yafuatayo yanahitajika:
1.lazima wawe na leseni na wapewe elimu ya barabarani mala kwa mala kuokoa vifo vya vijana wetu na abilia wanaobebwa maana ajali zimeongezeka sana.

2.wapewe elimu ya ujasiliamari ili pesa kidogo wanayopata iwasaidie mfano wanaweza kujiunga mifuko ya hifadhi ya jamii wakanufaika na mafao yanayotolewa na mifuko hiyo mfano fao la ajali,uzazi n.k
3.wawe na vazi rasmi litakalowatambulisha kama bodaboda na namba maalum zichapwe kwenye vazi hilo rasmi watakalokuwa wakilivaa wakiwa kazini ili kuondoa mwanya unaotumia na waharifu kutumia bodaboda katika wizi au madereva kuwaibia abiria wake wanapowasafirisha.
mfumo huu umesaidia sana katika nchi ya Rwanda pia nao walikuwa na tatizo kwenye sekta ya bodaboda kama Tanzania.

3:Ajira zinazotolewa na serikali zitolewe kwa usawa na sio kujuana kama inavyofanyika hivi sasa wenye uwezo ndio wapewe nafasi rushwa,na kujuana undugu vikomeshwe mala moja pia suala la uzoefu lisitumiwe kama kigezo cha kuwanyima nafasi vijana kwani wengi wao ni fresh from the school huo uzoefu wa miaka 3 wameupata wapi???
pia interview ziendeshwe mikoani tume ya utumishi iwe inatuma maafisa wake kuendesha hizi interview huko mikoani au washushe (ughatuzi) wa mamlaka ya uajiri kwa halmashauri ili kuondoa usumbufu wa kuwakusanya watu wote Dar es salaam. hapo kuna gharama za nauli kutoka mikoani kuja Dar pili wengi wao vijana hawana ndugu hapa Dar wakija wanafikia gest house bado ajira za kujuana na rushwa. kijana huyu akija kwenye interview mala 3 lazima familia wauze shamba ili aweze ashiriki interview ya nne maana atakuwa amefirisika kabisa.

4: mfuko wa maendeleo wa vijana uliopo kwa sasa hauna sifa ya kuitwa mfuko wa maendeleo ya vijana kwanza umeshindwa kushuka kwa vijana wenyewe chini kabisa (from the grass root) pili vijana wengi hawaujui tatu hakuna chombo cha vijana kinachousimamia nne wizara haiweze kushughulikia suala la kutoa mikopo kwa sababu haipo (connected from the grassroot).
mfano mwaka wa bajeti 2013/14 wizara ya vijana ilitenga bilioni 6.1 kwa ajili ya mikopo kwa vijana.swali ni je vijana wangapi wanajua hilo???
Je? ni vijana wangapi wamepata mikopo hiyo wenye mahitaji na wahusika??? vijana wa Bukopa ndani ndani,Mtwara ndani ndani wanajua kama wizara ilitenga bilioni 6.1 kwa ajili ya mikopo na wakajua utaratibu wa kuomba mikopo hiyo??? jibu sahihi ni Hapana.

wizara ya kazi na ajira nayo mwaka huu wa bajeti 2014/15 imetenga karibu bilioni 3 kwa ajiri ya vijana kwa utaratibu huu ni vijana wangapi na wanaostahili watanufaika na fedha hizi za serikali????
wenzetu kenya mwaka huu wa bajeti wametenga ksh. bilioni 1.8 sawa na sh. bilioni 32.4 za kitanzani kwa ajili ya vijana na fedha hizo zimepelekwa kwenye mfuko wa vijana ambao unasimamiwa na Baraza la Taifa la vijana (the national youth council of kenya) ushauri wangu
1. ufumuliwe mfuko wa maendeleo ya vijana utengenezwe upya.
2. serikali itenge bilioni 30 kila mwaka wa bajeti zipelekwe kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana kwa ajili ya mikopo hii itakuwa ni wastani wa bilioni 1 kila mkoa.
3.mfuko wa maendeleo ya vijana huu usimamiwe na baraza la Taifa la vijana. kama ilivyo kwenye nchi nyingine sio wizara kutoa mikopo kama ilivyo Tanzania.
4.mfuko wa maendeleo ya vijana kiwe ndiyo chombo cha kutoa mikopo kwa vijana chini ya usimamizi wa baraza la vijana
5.imefika wakati vijana watumie vyeti vya vyuo (academic certificate) kuchukulia mikopo kupitia kwenye baraza la vijana kwa kuwa uongozi wa baraza la vijana mfumo ambao ni mzuri unaanzia kwenye mtaa au kijiji hadi Taifa itakuwa rahisi kwa sababu watakuwa wanajuana vizuri.
kwa kuwa serikali kupitia wizara ya habari vijana, utamaduni na michezo ipo kwenye maandalizi ya kupeleka mswaada bungeni wa uanzishwaji wa baraza la Taifa la vijana.

pamoja na suala hili kuchukua muda mrefu sana na serikali kuwa kimya vijana tumeanza kutilia shaka nia ya serikali kusaidia kuundwa kwa chombo hiki muhimu kwa mustakbari wa vijana nchini.
kwa upande wa Zanzibar tayari serikali imeishapeleka mswaada bungeni wa baraza la vijana la Zanzibar na mchakato wao umefika mbali sana why not Tanzania bara?????

nchi ya Tanzania imeridhia mkataba wa vijana wa Afrika ambao unatoa Muundo unaosisitiza haki, majukumu na uhuru wa vijana kwa serikali, vijana wenyewe, wabia wa jumuiya za kiraia na wale wa kimataifa.
mkataba huu unatoa pia nafasi ya kuandaa programu na mpango mkakati wa kimataifa na uwezeshaji wake. pia mkataba huu utasaidia kutoa miongozo ya kisera na kisheria kwa sekta na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza mipango mikakati ya kuwaendeleza vijana nchini.
wenzetu Afrika mashariki tayari wote wana vyombo hivi muhimu vya kusimamia na kuwaunganisha vijana katika kuyatumikia mataifa yao.

Maazimio ya nchi wanachama wa Afrika mashariki ni kuwa ifikapo December 30 mwaka huu (30/12/2014) nchi wanachama ziwe zimekamilisha uundwaji wa mabaraza ya Taifa ya vijana na wanawake ili kutengeneza uongozi wa mabaraza ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki ili baada ya hapo waweze kuungana na wenzao (SADC).

Hivyo chonde chonde serikali pelekeni mswaada bungeni ili chombo hiki kiundwe haraka msije mkatukosesha fursa vijana wa Tanzania kujumuika na vijana wenzetu wa Afrika mashariki na SADC.
Nchi nyingi duniani baada ya vita ya pili ya Dunia zilianzisha mabaraza ya Taifa ya vijana ili kuwaunganisha vijana pamoja na kuwa na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

mfano wa nchi za mwanzo kabisa kuunda mabaraza ya vijana: switzeland (1933), sweden (1948), German (1949), Ireland (1967), Belgium (1970) n.k
kuna vijana wenzetu wanapata nafasi ya kutuwakilisha nje ya nchi kuhudhuria mikutano ya kimataifa ya vijana. swali linakuja hawa vijana wanapatikanaje kushiriki??? swali la pili wanaporejea nchini mrejesho wanampa nani???
Inashindikana kwa sababu hakuna (proper forum) ya kuwakutanisha vijana pamoja ili kuwaelimisha kile walichokuja nacho na vijana wenyewe kujichagulia mwakilishi wao na sio serikali kuwachagulia kama inavyofanyika hivi sasa.
Ushauri wangu wakati huu tunasubiria uundwaji wa baraza la vijana la Taifa. Ni ushauri wangu kwamba kila Halmashauri ifungue idara ya vijana au ofisi ya vijana kila Halmashauri nchi nzima kwa ajili ya kazi zifuatazo.

1.kusimamia 5% ya mapato ya ndani ya halmashauri inatengwa kwa ajili ya vijana na wanawake maana hakuna chombo cha kusimamia fedha hizi zinatengwa kila mwaka wa bajeti wa halmashauri.
2.kutoa elimu kwa vijana kuhusu mikopo hii namna ya kukopa na namna ya kurejesha, elimu ya ujasiriamali, na mikopo hiyo isiwe na Riba kwa sababu ni mikopo ya muda mfupi mfupi.
3.Idara ya vijana kila halmashauri zitakuwa zinapokea Taarifa na maelekezo ya wizara mbalimbali kwenda kwa vijana kote katika namna itakayo kuwa rahisi sana.

4.kuendesha semina,workshop,Training kwa vijana kuhusu masuala ya kijamii (social changes) masuala ya tabia, kuwaonyesha fursa zililizopo ambazo vijana wanaweza kuzitumia katika ujasiriamali.
5.chombo cha kusimamia masuala ya vijana katika halmashauri husika na kiunganishi kati ya vijana na serikali ili kupush mahitaji ya vijana kwa serikali.

Taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa ya mwaka 2013 inaonyesha kuwa wanachama wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii nchini ni takribani milioni 1.1 hivyo ni dhahiri kuwa hifadhi ya jamii inawahudumia watu wachache.
Ambao ni sawa na asilimia sita ya nguvu kazi na asilimia tatu ya watanzania wote.Inaoinyesha vijana wengi hawapo kwenye mifuko hii ya hifadhi ya jamii kitu ambacho ni hatari kwa mustakabadhi wa maisha yao ya baadae.
Sekta isiyo rasmi katika nchi nyingi duniani imekuwa na mchango mkubwa kusaidia katika hili mfano wa nchi ambazo sekta isiyo rasmi zimesaidia ni kama nchi ya China, Thailand na Korea Kusini.

Nchi ya china imefanikiwa kwa kufikisha hifadhi ya jamii vijijini tunapaswa kuhamasisha vijana wengi kutoka kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi kujiwekea akiba yao ya baadae au majanga Taifa liweke mikakati hiyo ikiwa na kuwachangia
asilimia kadhaa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Ukiuangalia mpango huu mzima na ushauri wangu utagundua kwamba kutakuwa na vijana wasomi (watakaoandaliwa kuwekeza kwenye viwanda) na wale ambao hawajasoma na waliosoma (watakaowekeza kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara na huduma) haya makundi yatabebana kwenye model hii na hivyo kila kundi litatoa ajira kwa watu wengi zaidi.

Tukiwatumia vijana kwa kuona mbele wakiwekeza leo na wakafanikiwa kuendesha biashara zao kwa faida. maana yake ni kwamba baada ya miaka 20 Tanzania itakuwa na matajiri wengi zaidi na itatoka kwenye kundi la nchi za daraja la tatu. mimi naliona hili ndilo kundi pekee litakaloweza kuijenga Tanzania ya miaka 50 ijayo. Ni lazima tuwe na ndoto pia ni lazima tujipange kuzifikia ndoto zetu.
hakuna ujanja mwingine. Hatuwezi kufanikiwa kwa kutumia mikakati ile ile iliyotufikisha hapa.

vijana tuungane bila kujali itikadi zetu za vyama ili kupush suala hili kwani kama ni ugumu wa maisha hauangalii upo chama gani au dini gani tuweke pembeni itikadi za vyama vyetu tuliambie Taifa kwa pmoja kwamba haya ndio mahitaji yetu.
vijana tunahitaji mabadiliko Tunahitaji kuona mikakati itakayoaksi mustakbari wa maisha yetu ya baadae.

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU WABARIKI VIJANA WA TANZANIA
 
Nakubaliana nawe katika hoja hii ila pia Nigeria sekta isiyo rasmi imetoa mchango sana kwenye ukuaji wa uchumi ingawa inahitaji kurasimishwa na kuingia katika planned economy
 
Tumuulize aliekuwa anasema atatengeneza ajira million moja kwa vijana na maisha bora kwa kila mtanzania.

Ameishia wapi? 2005 Mpaka sasa?
 
Mifuko mingi inawaandaa vijana kuwa wachuuzi badala ya kuwaandaa kuwa wazalishaji. Kuna sekta kama ya ngozi, vijana wakiandaliwa vizuri uzalishaji wa kutengeneza viatu ni shughuli isiyohitaji mtaji mkubwa. Hao wenye pesa zao wangetafuta jengo na kuruhusu vijana kufanyia kazi zao kwa makubaliano ya kulipa kiasi fulani kwa kila pea ya viatu inayokamilika.

Kuna bwana mmoja yeye kanunua machine zote za kutengeneza samani kuanzia kuranda, kuchana, moulding n.k. na ameruhusu vijana wenye ujuzi kufanyia kazi zao kwenye hiyo karakana yao kwa makubaliano kila kazi inaandikishwa na ikikamilika kabla ya kutoka inalipiwa "machine charge" ni kundi kubwa sana linafaidika na uwekezaji wa huyu bwana na endapo wenye fedha zao wangeiga mtindo huu ajira zingeongezeka (Hii karakana iko Kibanda maziwa Arusha)
 
Hii article ni nzuri sana, ngoja badae niisime vizuri, nahisi inahitaji kusomwa kwa umakini. Asante sana mkuu wa good analysis.
 
Mifuko mingi inawaandaa vijana kuwa wachuuzi badala ya kuwaandaa kuwa wazalishaji. Kuna sekta kama ya ngozi, vijana wakiandaliwa vizuri uzalishaji wa kutengeneza viatu ni shughuli isiyohitaji mtaji mkubwa. Hao wenye pesa zao wangetafuta jengo na kuruhusu vijana kufanyia kazi zao kwa makubaliano ya kulipa kiasi fulani kwa kila pea ya viatu inayokamilika.

Kuna bwana mmoja yeye kanunua machine zote za kutengeneza samani kuanzia kuranda, kuchana, moulding n.k. na ameruhusu vijana wenye ujuzi kufanyia kazi zao kwenye hiyo karakana yao kwa makubaliano kila kazi inaandikishwa na ikikamilika kabla ya kutoka inalipiwa "machine charge" ni kundi kubwa sana linafaidika na uwekezaji wa huyu bwana na endapo wenye fedha zao wangeiga mtindo huu ajira zingeongezeka (Hii karakana iko Kibanda maziwa Arusha)

nakubaliana na wewe Ben mfano Nigeria ukiondoa sekta ya mafuta na ya mawasiliano zilizochangia GDP ni sekta ya muziki na filamu za Nollywood ndiyo inafuata pamoja na kuirasmisha sekta isiyo rasmi inahitajika mikakati ya kisera na kisheria mfano hapa kwetu wasanii kila siku wanalia njaa tuu na nchi haipati chochote.

pia nimezungumzia suala la kisera kwa mfano viwanda vya sukari vijishughulishe na uzalishaji wa sukari tu suala la kuzalisha miwa wapewa wawekezaji wadogo lakini pia viwanda siyo maua vinategemea uzalishaji na soko.

kama nchi inaimport mchele wakati huko mbeya,shinyanga wanahangaika na soko la mchele, kama nchi inaimport mafuta ya kula wakati wakulima wa alzeti singida wanahangaika na soko la mafuta yao bila shaka uzalishaji utashuka sana, kama nchi inaimport nyama ya kuku kwenye supermarket unategemea nini hawa watu wetu watahimili ushindani sokoni.
pia
 
Mifuko mingi inawaandaa vijana kuwa wachuuzi badala ya kuwaandaa kuwa wazalishaji. Kuna sekta kama ya ngozi, vijana wakiandaliwa vizuri uzalishaji wa kutengeneza viatu ni shughuli isiyohitaji mtaji mkubwa. Hao wenye pesa zao wangetafuta jengo na kuruhusu vijana kufanyia kazi zao kwa makubaliano ya kulipa kiasi fulani kwa kila pea ya viatu inayokamilika.

Kuna bwana mmoja yeye kanunua machine zote za kutengeneza samani kuanzia kuranda, kuchana, moulding n.k. na ameruhusu vijana wenye ujuzi kufanyia kazi zao kwenye hiyo karakana yao kwa makubaliano kila kazi inaandikishwa na ikikamilika kabla ya kutoka inalipiwa "machine charge" ni kundi kubwa sana linafaidika na uwekezaji wa huyu bwana na endapo wenye fedha zao wangeiga mtindo huu ajira zingeongezeka (Hii karakana iko Kibanda maziwa Arusha)

nakubaliana na wewe Ben mfano Nigeria ukiondoa sekta ya mafuta na ya mawasiliano zilizochangia GDP ni sekta ya muziki na filamu za Nollywood ndiyo inafuata pamoja na kuirasmisha sekta isiyo rasmi inahitajika mikakati ya kisera na kisheria mfano hapa kwetu wasanii kila siku wanalia njaa tuu na nchi haipati chochote.

pia nimezungumzia suala la kisera kwa mfano viwanda vya sukari vijishughulishe na uzalishaji wa sukari tu suala la kuzalisha miwa wapewa wawekezaji wadogo lakini pia viwanda siyo maua vinategemea uzalishaji na soko.

kama nchi inaimport mchele wakati huko mbeya,shinyanga wanahangaika na soko la mchele, kama nchi inaimport mafuta ya kula wakati wakulima wa alzeti singida wanahangaika na soko la mafuta yao bila shaka uzalishaji utashuka sana, kama nchi inaimport nyama ya kuku kwenye supermarket unategemea nini hawa watu wetu watahimili ushindani sokoni.
pia
 
Habari vijana kwa wazee,
Napenda kuja na mada furukushi,hebu kijana na yeyote anaehusika,changia Nini kifanyike ili vijana waweze kujiajiri, nje ya mfumo wa serikali?? Tupaze sauti na mawazo fikirishi yenye masulihisho ktk tatizo kubwa la ukosefu wa ajira hapA kwetu Tanzania.
 
Vijana tuna ari ya Kupambana lakini mazingira ya nchi yetu hayasapoti kujiajiri, kati ya Vijana asilimia 100 watakao amua Kujiajiri ni Vijana kati ya asilimia tano tu ndo watakaoweza kuhimili kujiajiri, wengine asilimia 95 wanaishia njiani au wanafeli, ilo ni tatizo kubwa uwezi kuita hao waliofeli ni wazembe, ingekuwa asilimia chache ndo wanafeli ungesema uzembe, lkn asilimia 95 yote wanaishia njiani inatakiwa tuchunguze ni nn kinachofanya wafeli, Mazingira ya Tanzania watu wanafanya kazi sana ila wanachokipata hakiendani na wanachokifanya,
 
Viwanda ndio vina uwezo wa kuajiri Watu wengi...kuangaliwe namna ambayo zile bidhaa zisizo na ulazima wa kuagizwa kutoka nje ziwekewe mazingira magumu kama kodi n.k...yaani mizengwe.

Kama ni kuagiza basi ziagizwe malighafi tena zile zenye ulazima tu zisizopatikana hapa nchini.

Na hili liende sambamba na elimu ya uzalendo kwa Wananchi kupenda bidhaa za ndani....badala ya Watu kama kina Gwajima kutumia madhabahu zao kupiga soga basi walau wahimize wanaomuamini kuhusu umuhimu wa kutumia bidhaa za nyumbani.

Eneo lingine ni sanaa na michezo...tunapopeleka Washiriki Watatu tu Olympic basi tujue kuna mamia ya Vijana tunawakosesha ajira kwa uzembe tu wa kujiongeza, na hata juzi Nairobi kulikuwa na mashindano hatujashiriki...na hizo ndio ajira.

Pia tuongeze wigo kwenye michezo mingine mingi tu, mfano Tenis, Volleyball, handball, mbio za Baiskeli n.k.

Kwa upande wa Sanaa, kimuziki si haba ila kwa uigizaji tuache ushamba wa kutafsiri kazi za wengine, tuandae za kwetu tuuzie mailioni ya Wazungumzaji wa kiswahili East Africa na Africa na hata nje ya Africa.
 
Back
Top Bottom