Maoni yangu kuhusu Paul Makonda na Kigamboni

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Wana jamvi,

Niseme tu kwamba ninayo yasema hapa ni maoni yangu binafsi naweza kusahihishwa au la, ni kwamba Paul Makonda anaingia kugombea kwenye Jimbo ambalo alikuwepo Aliye wahi kuwa Naibu Waziri wa Afya, je huyo Waziri mstaafu hagombei tena kwa jimbo hilo?

Makonda kuonekana kugmbea huko sidhani kama kuna uwezekano wa kukatwa ila Waziri mstaafu ndiye anaweza akakatwa.

Kugombea kwa Paul Makonda kuna weza kunipa dira kuwa anaweza akapita na kuhakikisha anakuwa mbunge ili apewe u spika katika Bunge la Jamhuri yote haya anayatafuta ili na yeye apewe kinga ya kutoshtakiwa endapo kuna madudu na mambo mengine aliwahi kuyafanya akiwa Mkuu wa Mkoa maana wote hawa wakuu wa mihimili tayari wana kinga ya kutoshtakiwa.

Sasa hapa ndio panakuwa pagumu maana kwa lazima anaweza akahakikisha anapita ili apewe kinga.
 
Yote "labda" ni sawa...

Lakini nani kakuambia kuna kitu kinaitwa "kinga ya kutoshitakiwa!!??'

Hakuna mtu ambaye atatenda makosa hapa duniani na hususani Tanzania halafu asiwajibike kwa makosa yake, HAYUUUPO....!

Hii ni " natural principle ", hakuna wa kuitengua, hakuna sheria inayoweza kutungwa na binadamu itaitengua kanuni hii...!!.

Waliojitungia kanuni hii, hakuna neno sahihi la kuwa - describe zaidi ya kusema, NI WAJINGA, hawakujua watendalo....!
 
Ndugulile aliambiwa siku "wewe ni Naibu Waziri wa wizara ya afya, jimboni kwako hakuna madaktari wala madawa".

Hii kauli ilikuwa ni ujumbe tosha kumchonganisha na wapiga kura wake.

Kama ana akili na busara angekaa pembeni. Kuna msemo unasema " mwenye nguvu mpishe".

Bashite anashinda mchana kweupe kwa mbeleko ya baba.
 
Kugombea kwa Paul Makonda kuna weza kunipa dira kuwa anaweza akapita na kuhakikisha anakuwa mbunge ili apewe u spika katika Bunge la Jamhuri yote haya anayatafuta ili na yeye apewe kinga ya kutoshtakiwa endapo kuna madudu na mambo mengine aliwahi kuyafanya akiwa Mkuu wa Mkoa maana wote hawa wakuu wa mihimili tayari wana kinga ya kutoshtakiwa.
Kwa mjibu wa katiba ya nchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, spika siyo lazima awe mbunge, ila awe na zile sifa za mtu kuwa mbunge.

Naibu spika ndiye lazima awe mbunge.
 
Screenshot_20200719-210639.png
 
Yote "labda" ni sawa...

Lakini nani kakuambia kuna kitu kinaitwa "kinga ya kutoshitakiwa!!??'

Hakuna mtu ambaye atatenda makosa hapa duniani na hususani Tanzania halafu asiwajibike kwa makosa yake, HAYUUUPO....!

Hii ni " natural principle ", hakuna wa kuitengua, hakuna sheria inayoweza kutungwa na binadamu itaitengua kanuni hii...!!.

Waliojitungia kanuni hii, hakuna neno sahihi la kuwa - describe zaidi ya kusema, NI WAJINGA, hawakujua watendalo....!
Unajicontradict.

Unasema mtu huyo hayupo.

Kisha unasema waliotunga ni wajinga.

Kwahiyo wapo ila wajinga au hawapo kama ulivyosema?
 
Makonda anawanyima Usingizi sana Mafirauni, Wauza Unga, Wasio na Marinda, Wazee wa Shisha, Wazee wa Kutelekeza Familia nk.
Kijana mwenzako kwanini umchukie badala tuombeane heri maana sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu!
Kila lakheri Baba Keagan.
 
Unajicontradict.

Unasema mtu huyo hayupo.

Kisha unasema waliotunga ni wajinga.

Kwahiyo wapo ila wajinga au hawapo kama ulivyosema?

No contradiction...

Soma tena na kwa umakini, you will see what you missed. Then, utaelewa....

Yes, ni WAJINGA wote. Kwa sababu hawakuwa na macho wala ufahamu wa kuielewa hiyo "natural principle" kabla hawajajitungia na kujipitishia sheria ambayo is purely against natural principle....

Kama hujaelewa, omba Mungu uwe mzima hadi siku hiyo uje uone kama sheria hiyo itakuja kumsaidia ama kumlinda mtu mhalifu awaye yeyote....

Case study: MALAWI

Kama hawaamini vile. Jana ulikuwa umejizungushia misheria kibao eti kujilinda....

Kufumbua na kufumbua hauko madarakani tena, unawapisha au unaondolewa kwa nguvu kuwapisha wengine...

Hao wengine, wanafuta na kuondoa ulinzi wote wa kisheria na kisilaha....

Mwisho wa siku, taaratibu matendo yako yote yanafuatana na wewe sambamba na mshahara wake...

NB: 1. Tenda HAKI ama WEMA kisha nenda zako.

2. Kila dhambi itahukumiwa. Na mshahara wa dhambi (mtendo ya dhambi) ni mauti - adhabu ya maumivu makali...

Nimekufafanulia vya kutosha. Kama hujaelewa, basi sina namna ya kukusaidia...
 
Ninavyojua ni kwamba sheria iliyotungwa leo haiwezi kuhukumu kitu ambacho jana hakikua kosa.

Hii haiapply hapa?
 
Kwahiyo Dr Tulia hawi Spika tena?

Ufipa mnaweweseka sana.......bunge linatunga na kutengua sheria!

Bunge linatunga sheria, hiyo ni irreversible....

Lakini siyo lazima sheria itenguliwe na Bunge...

Huyu Rais mpya wa Malawi, sheria ya kinga ya Rais na maofisa wake kutoshitakiwa ilikuwa ni kufumba na kufumbua tu mara baada ya kiapo, ikafutika...

Watu wako "Segerea na Ukonga za Malawi" wanapambana na hali zao...

Kujitungia sheria za kujilinda binadamu kwa dhambi zetu, NI UJINGA na kujilisha upepo tu...

Ni kujaribu kum - challenge Mungu muumba tu. Na adhabu yake si cha mtoto eti...
 
Yote "labda" ni sawa...

Lakini nani kakuambia kuna kitu kinaitwa "kinga ya kutoshitakiwa!!??'

Hakuna mtu ambaye atatenda makosa hapa duniani na hususani Tanzania halafu asiwajibike kwa makosa yake, HAYUUUPO....!

Hii ni " natural principle ", hakuna wa kuitengua, hakuna sheria inayoweza kutungwa na binadamu itaitengua kanuni hii...!!.

Waliojitungia kanuni hii, hakuna neno sahihi la kuwa - describe zaidi ya kusema, NI WAJINGA, hawakujua watendalo....!
UNAANDIKA NADHARIA, WEKA MAJIBU KWA UHALISIA. naamini muandishi amesoma vizuri mabadiliko ya sheria yaliyo fanywa hivi karibuni.
 
Ninavyojua ni kwamba sheria iliyotungwa leo haiwezi kuhukumu kitu ambacho jana hakikua kosa.

Hii haiapply hapa?

Siyo katika scenario hii...

Huwezi kujitungia sheria wewe kufunika makosa yako unless wewe tu uwe madarakani siku zote....

Hili la pili haliwezi kuwa. Natural principle haifanyi kazi kwa namna hii....

Utatoka tu na watakuja wengine ambao watakuwa na upanga wa kukuadhibu wewe....

Ujinga wa binadamu uko hapa. Kutolielewa hii kanuni muhimu kabisa ya maisha...

Ni kwa sababu ya kiburi...
 
Back
Top Bottom