Maoni: Ubinafsi na uchoyo ndio huchangia zaidi kabila kukosa maendeleo

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
UBINAFSI Ni tabia ya kujiona wewe ni bora kuliko wengine hutaki wengine wawe kama wewe pale unapokuwa na nafasi fulani kudharau wengine

Katika baadhi ya makabila kuna watu miongoni mwao wamepata nafasi kubwa ya kuwasaidia wengine lakini wameshindwa kwa sababu ya ubinafsi matokeo yake jamii zao zimezidi kuwa masikini ziisizo hata na connection.

UCHOYO(SELFISH) Hii ni tabia ya kujiona wewe una stahili kupata na wengine hawastahili kbsaa,,tabia ya kutojali wengine kujilimbikizia vitu ambavyo kama ungegawia wengine basi jamii yako inge jaa wasomi, matajiri, n.k.

Kuna watu wame bahatika kumiliki mali nyingi mpaka zinawazidi lakini hawapo tayari kuanzisha kitu au miradi itakayo wasaidia wasionacho kupata kitu kwenye jamii zao ili kuleta maendeleo chanya sababu kubwa ni uchoyo na ubinafsi

MATOKEO YAKE NI KUKOSA KUWA NA UMOJA BAINA YA KABILA: sababu kubwa ni Ubinafsi na uchoyo, umoja unaweza kuundwa lakini miongoni mwao kuna wanaokuwepo wachoyo na wabinafsi mwishowe umoja unapotea kisa uchoyo

UPENDO hauwezi kustawi kwenye uchoyo na ubinafsi upendo una imarika kwenye kuvumiliana na kusaidiana tofauti na hivyo tutazidi kupoteana kila siku
 
Back
Top Bottom