Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
WANAUME TUACHE UBINAFSI!
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
Nilikuwa natoka Mashariki kuelekea Magharibi, sasa nitatokea Magharibi kurudi Mashariki. Kaskazini kwenda kusini kisha , kusini kurejea Kaskazini kama pepo za Kusi. Hivyo ndivyo safari yangu ilivyo.
Niite Taikon wa Fasihi, Kutoka Nyota ya Tibeli
Tabia ya ubinafsi imezidi kushamiri Sana kadiri siku zinavyosonga. Hii ni kusema kuwa Upendo siku hizi unayoyoma. Kwa maana kwenye upendo hakuna msamiati Ubinafsi.
Ubinafsi ni kitendo au hali au tabia ya kujipendelea kuliko pitiliza bila kujali Watu wengine.
Mtu yeyote anayejipenda kuliko pitiliza kamwe hawezi kukupenda, Kwa sababu MTU huyo ni mbinafsi.
Mtu mbinafsi hawezi kukupenda ingawaje atakuwa anakudanganya anakupenda.
Mtu mbinafsi hujiangalie yeye tuu bila kuangalia shida za Watu wengine,
Kwa mfano, mtu anaweza kuvuta sigara ndani ya Daladala, haoni kuwa Kwa wenzake ni kero, yeye anajijali mwenyewe MTU huyo ni mbinafsi, Hana upendo Kwa wengine Ila anajipendelea mwenyewe tuu.
Au mtu yupo nyumbani hasa nyumba ya Kupanga, anawasha muziki Kwa Sauti ya juu bila kujali kuwa anawakera Watu wengine mtu hiyo yupo kundi la Watu wabinafsi.
Hii itaenda sambamba na makanisa ya kilokole yanayopiga Makelele kucha kutwa huku yakizua usumbufu na uchafuzi wa mazingira, Sisi tutasema Makanisa hayo yanaubinafsi, yanajijali yenyewe bila kuangalia Watu wengine.
Ubinafsi ni kosa katika sheria za dini Kwa sababu huwezi kuwa mbinafsi alafu ukawa na upendo.
Ubinafsi pia ni kosa katika Asili(nature) Kwa sababu utazua matatizo ya kimahusiano baina ya mtu na mtu, au MTU na mazingira.
Tukirudi kwenye mada yetu ambayo itahusu ubinafsi wa Sisi wanaume ambao kimsingi tunatakiwa kuuacha mara Moja.
I) Ubinafsi wa Chakula.
Sijajua kama ni umaskini au ni kitu gani katika Aina Hii ya ubinafsi.
Baadhi ya wanaume tunapenda kuwekewa vile vyakula vizuri zuri na minofu mikubwa ya nyama mathalani Mapaja, kidari n.k. Huku tukiwaachia Wanawake na watoto wale vipapatio na vile finyango vidogo vidogo. Ukifuatilia sababu za hayo kufanyika haina hata mantiki.
Baba mwenye upendo anajua kabisa ndani ya familia kila mmoja anayohaki ya Kula chakula kizuri, kuanzia mke mpaka Watoto. Hivyo ni jukumu la Baba kufanya kazi Kwa bidii kuhakikisha anapata chakula cha kutosha ili kila mwanafamilia apate kitu Kizuri, wote wale mapaja.
Ikiwa uwezo utakuwa mdogo kulingana na majaliwa basi itabidi uundwe utaratibu wa kuwekeana zamu, leo Fulani na Fulani mtakula Paja, Wakati mwingine itakuwa Fulani na Fulani, hivyohivyo mpaka wote muishe.
Hivyo ndivyo familia inavyojengwa Kwa Upendo.
Vinginevyo MKE yeye mwenyewe Kwa vile ndiye incharge wa mambo ya mapishi na shughuli zingine za nyumbani, yeye ndio aseme Kwa mapenzi yake, akiwaambia Watoto Jamani Hiki ni chakula cha Baba yenu,
Alafu Baba ukija Kutoka mizunguko yako, lazima uwe Gentleman, unaweza kusema; ooh! Chakula cha leo kinaharufu nzuri, embu!(unaonja) oooh! Nikitamu pia, unamtazamo Mkeo unamwambia wewe ni fundi, unajua mpaka unajua tena. Unamkonyeza kichokozi kisha unambusu Kwa mbali,
Unachukua mnofu mmoja unampa mtoto, mtoto anapokea, Mkeo anamkanya mtoto, unasisitiza Acha mtoto ale, Mkeo anakaza, unamkatia kipande kidogo mtoto ale.
Au kama ni wale wa Kula Kwa pamoja, Mkeo kakuwekea minofu mikubwa, basi wewe unampunguzia sehemu ya Ile minofu.
Halikadhalika Mwanamke akiwa na minofu atampunguzia mumewe. Hiyo tunaita Love.
ii) Ubinafsi wa Kihisia.
Hii ndio Ipo Sana.
Wanaume lazima tuelewe, vile tunavyoumia Wakati Wake zetu wanatongozwa au kuchapwa na kubenjuliwa na wahuni ndivyo Wanawake wanavyoumia tukiwa-cheat.
Ipo kasumba na dhana potofu kuwa Sisi wanaume tunatamaa ni kweli tunatamaa ndio maana tukaambiwa tuoe Mwanamke mzuri kadiri ya vigezo vyetu ili hizo tamaa za mwili huyo Mwanamke azikomeshe.
(Sisemi hapa kama MTU Mwema) nazungumzia ubinafsi wetu kama wanaume.
Ni ubinafsi wa Hali ya juu kutokuthamini hisia za wengine hasa Mkeo na watoto.
Unajali hisia zako pekee, vile zitakavyokutuma unazifuata.
Alafu muda huohuo unaumia Mkeo akitoka nje. Huo ni upunguani.
Au unakuta kijana anampotezea muda Binti WA watu huku akijua kabisa hatamuoa, huo ni ubinafsi wa Hali ya juu.
Mtu kama hutomuoa mwambie Mimi sitakuoa, mtongoze demu mwambie ukweli wote, mwambie umemtamani, yeye ni mzuri, na unataka mapenzi yake. Ila hauna Mpango WA kumuoa.
Kama yupo interested na mahusiano ya namna hiyo atakukubalia, au atakataa kama hayupo tayari kuingia kwenye relationship ya hivyo.
Mbona Sisi wengine tupo wazi na tunapewa tuu bila hiyana,,, Kuliko umdhulumu MTU ni Bora umwambie ukweli, uamuzi ubakie kwake.
iii) Ubinafsi wa kusosholaizi
Wewe ndiye unataka utumie mitandao pekeako, wewe ndio unataka ukiwa nyumbani chaneli uipendayo uonyeshwe, wewe ndiye unajitoa out pekeako mara Bar Hii mara Ile, wewe pekeako ndio unandugu na marafiki. Come on!
Kisingizio chako ni oooh! nikimpa Uhuru MKE wangu nitachapiwa😂😂😂
Hizo ni Akili au Matope.
Kuchapiwa kunategemea na Akili na tabia ya Mwanamke.
Hata akiwa nyumbani au umfunge jela awe pekeake akiamua kuchapwa atachapwa tuu.
Ubinafsi ni pamoja kutaka kummiliki. Mwenzako kama Kandambili zako, yaani kama Mfugo wako.
Wekeni sheria, Kanuni na Standards za familia yenu. Kisha kila MTU awe huru kuishi Maisha yake Kwa furaha ndani ya Ndoa yenu.
Kama zitavunjwa hizo Kanuni hasa zile sheria kubwakubwa basi itamkwe kabisa kuwa Ndoa itavunjwa.
Rahisi Sana.
Kuliko umnyime mwenzako Uhuru Kwa kumbana kisa ubinafsi wako.
Huko ni kutokujiamini
Ubinafsi ni pamoja na kutaka kuidhibiti Free Will ya MTU mwingine.
Familia nyingi na ndoa nyingi zinaanguka Kwa sababu ya ubinafsi uliopitiliza ya wenza ndani ya Ndoa.
Sabato NJEMA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam