Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,338
- 9,766
Ndugu zangu Watanzania,
Dunia inaendelea kusimama nasi, inaendelea kutufuta machozi, inaendelea kutupatia faraja na kutufariji, Inaendelea kutushika mkono, inaendelea kutupatia ushirikiano, inaendelea kutuonyesha upendo na ukarimu,Inaendelea kutuondolea upweke,huzuni,majonzi na simanzi ya kupoteza ndugu zetu kupitia maporomoko ya udongo kule hanangi ambayo yamechukua roho za watanzania wenzetu 76.
Baada ya wadau mbalimbali kutuchangia imekuwa zamu ya Marekani Taifa kubwa Duniani kiuchumi ,kijeshi,kiteknolojia n.k. ambapo limeweza kutuchangia dollar laki moja ambazo ni sawa na Zaidi ya million mia mbili hamsini pesa za kitanzania. Ambapo balozi wa Marekani nchini Tanzania mh Michael Battle ametoa pole sana kwa watanzania kwa msiba huo mkubwa uliolikumba Taifa letu.
Lakini pia Balozi huyo amesema kuwa ubalozi wa Marekani unaendelea kufuatilia kwa ukaribu sana kinachoendelea kule Hanang na kwamba itatoa na kuendelea kutoa misaada kwa kadri hali itakavyokuwa. Amesema kuwa Tanzania ni Rafiki mkubwa sana wa Marekani.
Ndugu zangu watanzania tuendelee kuwa watulivu na kuwaombea sana ndugu zetu waliopoteza wapendwa wao ili Mungu awape subira na kuwatia nguvu.kufiwa au kupoteza ndugu au mwana familia inauma sana .hivyo tunatambua maumivu makubwa waliyonayo wenzetu wa Hanang na ndio maana hatuna budi kuendelea kuwaombea na kuwasaidia kwa hali na mali.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.