kuduman201036
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 4,057
- 2,163
>> HAPA kuna MIKONO ya AKILI MALI >>
Mafisadi wengi wanapofanya deal yoyote ile kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhusisha wanasheria tena wengi.vimemo vimechomwa moto eeh?? afu bado mnalipa billion 4 kila mwezi iwe wanazalisha umeme or not??? dah haya bana kma mmeamua kutetea uozo serikalini kwa kigezo cha ''Tusifukue makaburi'' huku mkigombana na wafanyabiashara kma manji na mbowe ndio "mnafukua makaburi"???? ila kwa serikali noooo hamfukui???
Kwa aina hii ya wananchi mnaotetea uozo itatuchukua miaka 50 kufikia uchumi wa kati na viwanda.
Manji ahitajika Uhamiaji: Ofisi ya uhamiaji jijini Dar imemtaka mfanyabiashara Yusufu Manji kuripoti kwenye ofisi hizo baada ya kutoka hospitali alikolazwa.
Ofisa Habari wa uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam
amedai kuwa Manji ameajiri watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.
My take;
Kuacha habari hiyo mimi binafsi ningependa kuwashauri mamlaka ya uhamiaji ili kututhibitishia kuwa Operation hii kuwa sio ya visasi wala chuki binafsi kama inavyodhaniwa na wengi. Iendelee kwenye makampuni mengine hasaa yanayomilikiwa na Wahindi
Kumekuwa na Utitiri wa Raia wa India ambao wamekuwa wakifanya kazi ambazo wazawa wana uwezo wa kuzifanya
Wenzetu kenya wameweza kudhibiti utitiri wa Raia wakigeni kufanya kazi ambazo Raia wa kenya wana uwezo wa kuzifanya. Mfano mmojawapo ni kampuni ya Kenya Airways ukiacha Uongozi wa juu ambao ni Kuna Raia wa kigeni wachache. Wengine wote kuanzia mafundi wa ndege hadi marubani ni Wakenya wenyewe
Mfano mwingine ni kiwanda chao cha kutengeneza Magadi soda yanayotumika kutengeneza sabuni na vitu vingi kana vioo na chupa za glasi (soda hash dese) kiwanda chao kinaitwa TATA CHEMICALS kinachomilikiwa na raia India
Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa maelfu ya watu kenya kuanzia ajira rasmi na zile zisizo rasmi. Lakini mshangao ni kuwa katika maelfu ya waajiriwa wa kiwanda hicho Wahindi wapo wawili tu yaani GM(General manager) na Mhindi anaye husika na maswala ya Account tuu,, wengine wote ni wakenya
Lakini hapa kwetu utakuta kampuni kuanzia Utawala hadi Operations sector kumejaa raia wa kigeni
=======
Habari zadi zinasema...
UHAMIAJI WAKAMATA PASSPORT 126 QUALITY GROUP.
Upepo Mchafu umezidi Kumuandama Manji, Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....
John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.
Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.
Mara tu atokapo, aliport ofisi hii ili tumuunganishwe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.
Utakamatwa, utawekwa ndani, utajibu mashitaka.
View attachment 470417
Yusuf Mehbub Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini Tanzaznia na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu(CCM) Jimbo la Mbagala Dar es Salaam. Vilevile ni Mwenyekiti wa Club ya Mpira ya Nchini Tanzania Yanga Afrika SC.
Uhamiaji wana kesi ya kujibu hapo.!Waliingiaje nchini hao?
Amekamata passport 126 na watu 25 wanaofanyakazi bila kibali .sijaelewa vizuri hapo .nipassport pekee yake au !???
kwani sheria gani inakataza mtu kwenda kituoni na wanasheria zaidi ya mmoja??? kma sheria haijakataza kosa likwapi?? je umejuaje kma siku zote huwa anatembea nao hadi ufkiri ni siku ile tu alipoitwa polisi?? je unafaham kma kuna specialization kma commercial law, labor law n.k sasa kma hao saba wote ni different legal sectors kuna ubaya gani akienda nao wote wamsaidie ???Mafisadi wengi wanapofanya deal yoyote ile kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhusisha wanasheria tena wengi.
Jiulize mtu unaitwa police unaenda na wanasheria zaidi ya saba. Wa nini wote hao kama una kosa!
Mi nahisi hawa jamaa walikua wanafaham na pengine walikua wanavuta mshiko wameona inaweza ika back fire baada ya Manji kuwa amekamatwa na ujio wa kamishna Jenerali mpyaRais wa visasa .Muda wooote mlikywa wapi msilione hilo.au kwasababu ayo kwenye mtandao wakho!!!?
Toa taarifa mkuu vinginevyo na wewe utaonekana unashiriki uhalifu.ila huu unafiki wa serikali mi ndo siutaki kabisa, kuna wachina wangapi na wahindi wangapi wanaishi bila vibari? tena mi ofisi kwangu wapo kibao na wakija rushwa nje nje na unaona
Sasa kwenye issue hii ya madawa masuala ya Simba yanakujaje?!Hizi ni hujuma za simba
Wamesema akitoka hospitali, inamaana uhamiaji hawana data Kabla ya tukio la manji kukamatwa ndio useme watu hawana vibali!!!!!Sasa anaripoti vp wakati bado yuko chini ya ulinzi?
We Mr. Zero kweli,unadhani mm ni wa kujitangaza ovyo ovyo kama nyinyi mnaopata tu pesa twa balimi...Wewe umeshaisaidia nini hii Nchi?
Aondoke tu. Mbona rostam katupiga bao akakimbiasasa wanataka kumkimbiza tz huyo mhindi, kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza
Mafisadi wengi wanapofanya deal yoyote ile kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhusisha wanasheria tena wengi.
Jiulize mtu unaitwa police unaenda na wanasheria zaidi ya saba. Wa nini wote hao kama una kosa!