Manji atakiwa kuripoti Ofisi za Mamlaka ya Uhamiaji. Pasi 126 za kusafiria zakamatwa ofisini kwake

vimemo vimechomwa moto eeh?? afu bado mnalipa billion 4 kila mwezi iwe wanazalisha umeme or not??? dah haya bana kma mmeamua kutetea uozo serikalini kwa kigezo cha ''Tusifukue makaburi'' huku mkigombana na wafanyabiashara kma manji na mbowe ndio "mnafukua makaburi"???? ila kwa serikali noooo hamfukui???

Kwa aina hii ya wananchi mnaotetea uozo itatuchukua miaka 50 kufikia uchumi wa kati na viwanda.
Mafisadi wengi wanapofanya deal yoyote ile kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhusisha wanasheria tena wengi.

Jiulize mtu unaitwa police unaenda na wanasheria zaidi ya saba. Wa nini wote hao kama una kosa!
 
Manji ahitajika Uhamiaji: Ofisi ya uhamiaji jijini Dar imemtaka mfanyabiashara Yusufu Manji kuripoti kwenye ofisi hizo baada ya kutoka hospitali alikolazwa.

Ofisa Habari wa uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam
amedai kuwa Manji ameajiri watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

My take;
Kuacha habari hiyo mimi binafsi ningependa kuwashauri mamlaka ya uhamiaji ili kututhibitishia kuwa Operation hii kuwa sio ya visasi wala chuki binafsi kama inavyodhaniwa na wengi. Iendelee kwenye makampuni mengine hasaa yanayomilikiwa na Wahindi

Kumekuwa na Utitiri wa Raia wa India ambao wamekuwa wakifanya kazi ambazo wazawa wana uwezo wa kuzifanya

Wenzetu kenya wameweza kudhibiti utitiri wa Raia wakigeni kufanya kazi ambazo Raia wa kenya wana uwezo wa kuzifanya. Mfano mmojawapo ni kampuni ya Kenya Airways ukiacha Uongozi wa juu ambao ni Kuna Raia wa kigeni wachache. Wengine wote kuanzia mafundi wa ndege hadi marubani ni Wakenya wenyewe
983769e42f3f675acb9e7a422c8546a5.jpg



Mfano mwingine ni kiwanda chao cha kutengeneza Magadi soda yanayotumika kutengeneza sabuni na vitu vingi kana vioo na chupa za glasi (soda hash dese) kiwanda chao kinaitwa TATA CHEMICALS kinachomilikiwa na raia India


Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa maelfu ya watu kenya kuanzia ajira rasmi na zile zisizo rasmi. Lakini mshangao ni kuwa katika maelfu ya waajiriwa wa kiwanda hicho Wahindi wapo wawili tu yaani GM(General manager) na Mhindi anaye husika na maswala ya Account tuu,, wengine wote ni wakenya

Lakini hapa kwetu utakuta kampuni kuanzia Utawala hadi Operations sector kumejaa raia wa kigeni

=======

Habari zadi zinasema...

UHAMIAJI WAKAMATA PASSPORT 126 QUALITY GROUP.



Upepo Mchafu umezidi Kumuandama Manji, Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....

John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.

Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.

Mara tu atokapo, aliport ofisi hii ili tumuunganishwe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.

Utakamatwa, utawekwa ndani, utajibu mashitaka.
View attachment 470417
Yusuf Mehbub Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini Tanzaznia na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu(CCM) Jimbo la Mbagala Dar es Salaam. Vilevile ni Mwenyekiti wa Club ya Mpira ya Nchini Tanzania Yanga Afrika SC.


Wow, haya ndio mambo ya mwanamama kamishna eh! Inaonekana watendaji waaminifu wa uhamiaji walishachoshwa na uhuni wa mabosi wao wa zamani walioendekeza uhuni na hivyo kuwafanya waaminifu hawa wakose kwa kusemea na kupulia! Sasa wamepata kamishna mpya wameamua kumpa kazi wakijua ataifanya kwelikweli! Viva uhamiaji! Mbona sisi tukienda nchi zao tunafuata taratibu zote na tusipofuata wanatu'discipline'?
 
Luka 12:57-59
[57]Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki?
[58]Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
[59]Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
 
Wapite vyuo binafsi na shule binafsi .huko wamejaa..masecretary..wahasibu...wafagizi...shamba boy wa kigeni...halafu ni wajeuri....wana majibu mabovu.
 
Amekamata passport 126 na watu 25 wanaofanyakazi bila kibali .sijaelewa vizuri hapo .nipassport pekee yake au !???

kulikuw ahakuna sababu ya kuitaja hizo zaidi ya zile 25 zenye shida, tena pasport sio issue sissue ilikuw ani kuwa watu 25 wanfanya akzi bila kibali full stop~!
 
Mafisadi wengi wanapofanya deal yoyote ile kitu cha kwanza wanachofanya ni kuhusisha wanasheria tena wengi.

Jiulize mtu unaitwa police unaenda na wanasheria zaidi ya saba. Wa nini wote hao kama una kosa!
kwani sheria gani inakataza mtu kwenda kituoni na wanasheria zaidi ya mmoja??? kma sheria haijakataza kosa likwapi?? je umejuaje kma siku zote huwa anatembea nao hadi ufkiri ni siku ile tu alipoitwa polisi?? je unafaham kma kuna specialization kma commercial law, labor law n.k sasa kma hao saba wote ni different legal sectors kuna ubaya gani akienda nao wote wamsaidie ???
 
Nnachojua huyu bwana atatoroka na kukimbilia nje ya nchi kwa sababu uwezo wa kutoroka anao hata wangemlinda masaa 24,

Nisichojua ni hatma ya serikali ya viwanda, maana atafunga biashara zake atahamishia pesa zake nje kama Rostam kisha anakula kuku tu baasi.

Ndugu mliokuwa mmeajiliwa kwenye viwanda na miradi ya huyu jamaa anzeni kufungasha mizigo kurudi vijijini kwenu maana kazi kushnei chacha!!
 
Rais wa visasa .Muda wooote mlikywa wapi msilione hilo.au kwasababu ayo kwenye mtandao wakho!!!?
Mi nahisi hawa jamaa walikua wanafaham na pengine walikua wanavuta mshiko wameona inaweza ika back fire baada ya Manji kuwa amekamatwa na ujio wa kamishna Jenerali mpya
 
ila huu unafiki wa serikali mi ndo siutaki kabisa, kuna wachina wangapi na wahindi wangapi wanaishi bila vibari? tena mi ofisi kwangu wapo kibao na wakija rushwa nje nje na unaona
Toa taarifa mkuu vinginevyo na wewe utaonekana unashiriki uhalifu.
 
MOHAMED DEWJI NDIO BINGWA WA KUAJIRI WAHINDI WASIO KUWA NA VIBALI VYA KUISHI NCHINI-PALE KWENYE KIWANDA CHAKE KILICHOPO BARABARA YA AIRPORT KUNA WAHINDI WENGI HAWANA HATA VIBALI.
KWA KWELI KUNA WAHINDI WENGI SANA NCHINI HAWANA VIBALI VYA KUISHI-SEMA KAMA ILIVYOKAWAIDA YAO WANAHONGA MAAFISA WA UHAMIAJI WANAKUWA HAWAFATILIWI
 
Back
Top Bottom