Manispaa ya Ilala tunahitaji machinjio mapya ya kisasa

Africa one

JF-Expert Member
May 6, 2013
244
111
Machinjio ni moja ya sehemu muhimu katika jiji la Dar es salaam kwani sehemu pekee inayotumika kuandaa kitoweo/nyama zinazoliwa hapa jijini na sehemu zingine za nchi.
Kwa ujumla kuna machinjio kama tano yaliyo rasmi na yasiyo rasmi katika jiji hili.

Machinjio yanayojulikana japo yote sio rasmi ni pamoja na Ukonga Mazizini (Ilala), Vingunguti (Ilala), Mbagala(Temeke), Kimara na Tegeta ya Kinondoni na kati ya hayo Chinjio la Vingunguti ndilo la serikali na mengine yaliyotajwa hapo yanamilikiwa na watu binafsi.

Hapa nataka kuzungumzia machinjio ya Ukonga na Vingunguti na changamoto zake pamoja na umuhimu wa hitaji la machinjio mapya ndani ya manispaa ya Ilala. Nianze na chinjio la Ukonga Mazizini ambalo mimi ni mdau wake mkuwa kama mfanyabiashara hapo wa kuuza nyama bei ya jumla.

Kwa ufupi machinjio hii ilianzishwa tangu mwaka 1974 bila utaratibu wowote ule wala kibali cha kuweza kufanya biashara hiyo (hayo ni kwa mujibu wa moja wa wamiliki wa machinjio hayo Bw. Hamis) ambae alikuwa akihojiwa na Mh. Mbunge Mwita Waitara mbunge wa Ukonga.

Hata hivyo mda huo wote ilikuwa ikiendeshwa bila vibali au urasimi wowote kutoka serikalini hadi hapo mahojiano hayo yanafanyika mwaka huu.Pia hayo yanamilikiwa na umoja wa unajulikana kama UWEMA chini ya mwenyekiti wao Bw. Chambogo.Pia ktk eneo hilo kuna Umoja wa wauza Nyama bei ya Jumla(UWANJU) chini ya mwekiti Bw. Alfa na Michael Timbo.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na msuguano kati ya vyama hivi viwili yaani UWANJU na UWEMA hasa baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani umeongezeka zaidi hata kufikia sasa wafanya biashara hawana uhakika na biashara yao ya nyama, na hii imechochewa zaidi na baadhi ya viongozi wa serikali na wale wa kisiasa kutembelea eneo hilo na kubaini madudu yaliyokuwa yakifanyika hupo viongozi hao ni Waziri wa mifugo, kilimo na mifugo mh.

Mwigulu Nchemba, meya wa manispaa wa Ilala, mbunge wa ukonga pamoja na baadhi ya madiwani wanaozinguka eneo hilo.UWEMA wamekuwa wakiwatuhumu UWANJU kuwa wao ndio wanao waleta hawa viongozi jambo ambalo sio kweli kwani wao viongoz huwa wapo kwenye utendaji wa shughuli zao km kawaida, lakini hata hivyo kama UWANJU wanawaleta bado sioni tatizo kwa ujio wa hao viongozi wanakuja kuwatatulia changamoto zinazowakabili kwani kila tatizo linalotokea hapo hawa wafanyabiashara ndio wanaohangaika zaidi na familia zao pamoja na michango na mapato wanayochangia serikalini sio hawa UWEMA.

Kimsingi michango yote inayotoka ktk machinjio haya inatolewa na wafanyabiashara hawa na si mwingine.Mfano kuna ushuru wa halimashauri tsh. 2500/- kila ng'ombe, kuna 5300/- kila ng'ombe wanapewa wamiliki (UWEMA) bado kuna 6000/- kila ng'ombe ambazo zinalipwa mnadani moja kwa moja serikali kuu ambazo pia zinatolewa na hawa wafanyabiashara huo mzigo wote wa fedha unamgusa mfanyabiashara (UWANJU) lakini sisi kama wafanya biashara hatuoni mrejesho wowote zaidi ya kutabika.

Tuna changamoto ya machinjio hii kufungiwa mara kwa mara na mamlaka ta chakula na dawa TFDA kuwa machinjio haikidhi vigezo ila hali wamiliki wanachukua hela kila siku pia manispaa inachukua hela kila siku msaada wao kwetu ni upi.

Na hii ndio machinjio kubwa kuliko zote hapa Dar es salaam.Pia sisi wafanyabiashara tunafanyia biashara katika mazingira ya mbinyo sana maana kuna baadhi ya mazao ambayo ni ya mifugo tunayochija lakini eti hatuna mamlaka ya kuyamiliki kama vile damu ambazo wamiliki wanapokea mamilion ya shilingi kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo na hapa zaidi ya ng'ombe 400 huchinjwa kila siku.

HITAJI LA MARCHINJIO MPYA.
.Tunahitaji chinjio linalokidhi vigezo vya TFDA watalaam wanajua hill.
.Tunahitaji chinjio ambalo liko mbali na makazi ya watu.
Pia tupate chinjio tutakalo kuwa huru kuhoji kile tunachochangia kama wadau kwani kwa sasa hata kujua idadi ya ng'ombe tunazochinja hawaturuhusu kuhofia kutumbuliwa.
Serikali tunaamini maeneo yapo katika hii manispaa, machinjio ni MGODI UNAOWEZA KUKUCHANGIA FEDHA NYINGI KAMA UTASIMAMIWA VEMA.
 
Kwa kuongezea uzito wa uzi huu kihusu mahitaji ya machinjo mapya na ya kisasa kwa Ilala.
.Kwa namna shughuli hii inavyoendeshwa kiholela ktk jiji la dar es salaam inahatarisha maisha na afya ya walaji wa kitoweo hiki cha nyama, maana ng'ombe zinachinjwa kiholela na kusababisha nyama kuzagaa na kuuzwa mitaani kama nguo, unakuta mtu anakuja na nyama nyumbani kwako eti anauza nyama kwenye ndoo.
Pale wauzaji wauzaji wanapojaribu kudhibiti hali ya uholela hapo pia ndipo wamiliki wanazua mzozo na chama cha Uwanju kwani wamiliki wao wanataka ng'ombe zichinjwe nyingi ili wapate hela nyingi kwa hiyo suala la kucontrol uchinjaji haliwahusu.
Hivyo tukiwa na machinjio ya kisasa tunaweza kucontrol hali hiyo kwani kwa vigezo vya TFDA machinjio lazima iwe na sehemu maalum ya kuhifadhi nyama zinazobaki na zinaweza kuuzwa hata baadae au kesho yake bila kuharibika.
Kitu kingine tukiwa na machinjio ya kisasa itasaidia kuondoa hofu kwa wakazi wanaoishi maeneo yanayozunguka hizo machinjio kwani kwa sasa hasa eneo la Ukonga mvua ikinyesha harufu na uchafu hutapakaa hadi ktk makazi ya watu kwani taka hizo zingine zinatiririshwa moja kwa moja hadi mifereji inayoingia ktk makazi ya watu.
Kubwa zaidi ni mapato ya serikali yanayopotea kwa kukosa usimamizi imara.
Mfano siku waziri amefanya ziara tu ya kushitukiza ktk machinjio ya Ukonga kuna gari lilibainiwa limepakia ng'ombe zaidi ya 70 lakini hesabu iliyowakilishwa ilikuwa ng'ombe 20 ktk gari hiyo moja, maana yake ni kuwa zaidi ya ng'ombe 50 hazikuwa ktk hesabu za serikali, hiyo ni gari moja kwa siku machinjio ya Ukonga hupokea zaidi ya gari zaidi ya gari tano kwa siku za aina hiyo.
Ukipiga hesabu kila ng'ombe huwa tunailipia tsh.2500/- zidisha hesabu kwa siku utaona kiasi cha fedha za serikali zinazopotea.

Kwa muktadha huo naamini manispaa yangu ya Ilala mtalifanyia kazi suala hilo.
Naamini uwezo mnao kama hamna tutafutie wafadhili watujengee kwa udhamini wenu ili sisi tulipe wenyewe tunaweza kama Umoja wetu wa UWANJU.

Vyanzo vyetu vya mapato ni pamoja na Mazao yetu ya mifugo yanayoporwa na wamiliki kwa kupewa mamilioni na watu waliowekeza kwenye damu ya ng'ombe zetu tunazonunua.

Pia tunaweza kuchanga kwa kila kichwa cha ng'ombe km tunavyolipishwa kwa sasa 5300 na wamiliki.
Tunajua tukijiwekea utaratibu itawezekama maana yatakuwa malipo ya mda tulikamaliza deni tutaweza kusaidiana sisi wenyewe kupitia hiyo hela.

Pia kupitia kinyesi cha wanyama hao tunaweza kuzalisha umeme (bio electric power) ambao unaweza saidia hata wale wanaotuzunguka.

Niishie hapo kwa kuwaomba wahusika kiyafanyia kazi haya ni muhimu kwa usitawi wa manispaa na jiji letu.
 
Hivi hiyo manispaa si inashikiliwa na ccm?, tuwape muda labda watatekeleza
 
mkuu muuza nyama umesikika vizuri na tayari tuko kwenye mchakato wa kuwasiliana na Mstahiki Meya wa jiji ili amtafute didas masaburi aonyeshe zilipo zile pesa za machinjio ya kisasa zaidi ya Tsh 2.5 bil .
 
Back
Top Bottom