Mbunge Janeth Masaburi ampongeza Rais Samia Suluhu kwa kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi yetu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

Mbunge Janeth Masaburi Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Kuwekeza Miradi Mikubwa ya Maendeleo Katika Nchi Yetu

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Janeth Masaburi, amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi yetu

Mbunge Janeth Masaburi alisema hayo Jimbo la Segerea wakati wa ziara yake ya kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti wilayani Ilala ambapo Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan imewekeza pesa nyingi katika mradi huo.

"Ziara yangu dhumuni lake kuangalia utekelezaji wa Ilani katika miradi ya maendeleo ya Serikali, tunamshukuru Rais wetu na kumpongeza ametoa pesa nyingi katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo mradi wa machinjio Vingunguti, miradi ya sekta ya Afya, Sekta ya Elimu, Miundombinu ya Barabara "alisema Masaburi.

Mbunge Masaburi alisema kazi kubwa amefanya Rais hivyo mwaka 2025 kura zote zitaenda kwake za mkoa Dar es Salaam kutokana na mambo makubwa aliyofanya katika nchi hii .

Alisema Rais ana mapenzi mema ametoa pesa nyingi kwa ajili ya machinjio ya Vingunguti wilayani Ilala na wasaidizi wake wamefanya kazi kubwa pia tunawapongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura na Meya wake wa jiji hilo Omary Kumbilamoto, wamesimama Imara mpaka mwaka 2024 nyama zitasafirishwa kwenda nje ambazo zinazalishwa Tanzania..

Katika hatua nyingine mara baada kufanya ziara kukagua majengo ya machinjio hayo na kupokea changamoto mbalimbali alisema amezipokea na kuzifanyia kazi ,ikiwemo sehemu ya mfumo wa maji taka amewataka uboreshaji zaidi huku akiwataka waongeze usafi kila wakati.

Wakati huo huo aligawa majiko ya gesi bure kwa wanawake Mama Lishe wa Vingunguti na Kisukuru,na kuwataka wanawake kuunga mkono juhudi za Rais kutumia nishati mbadala ya gesi waache kutumia mkaa na uharibifu wa mazingira waache kukata miti ovyo.

Aliwataka Mama lishe wa Vingunguti kujenga tabia ya kutumia gesi watunze pesa kidogo kidogo wanunue gesi wakati wakisubiri mkaa mbadala kwa matumizi.

Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti alisema machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti yapo katika hatua za mwisho kukamili.

IMG-20231206-WA00631.jpg
IMG-20231206-WA00641.jpg
IMG-20231206-WA00651.jpg
 
Ifikie kipindi wanasiasa wapimwe kwa mambo ya kuumiza kichwa sio mambo mepesi kama ujenzi wa miundo mbinu, ununuzi wa madawati na ujenzi wa matundu ya choo au kuidhinisha bajeti.

Hayo yote yanawezekana fund ikiwepo.

Mambo ambayo mwanasiasa inabidi asifiwe ni kama ifuatavyo:

1. Kukabiliana mfumuko wa bei na gharama za maisha kulinganisha na uchumi wa dunia.(SIO KUSINGIZIA UCHUMI WA DUNIA UMEYUMBA KWA VITA ZA MASHARIKI YA KATI AU MBALI)

2. Kuleta ubunifu katika kutengeneza ajira mpya kwenye sekta binafsi na umma. (SIO KUAJIRI KWA AJIRA ZILEZILE AU KUDUMAA NA KUFA KWA SEKTA BINAFSI KWA UTITIRI WA KODI NA TOZO).

3.Kudhibiti wizi, rushwa, matumizi ya ovyo na hasara za mali za umma, ambazo msingi wake ni jasho la masikini ambao ni majority. (SHERIA KALI ZITUMIKE KWA WATAKAOTHIBITIKA KUHUJUMU NA KUFANYA UBADHILIFU IKIWEZEKANA WANYONGWE).

4. Kusimamia ustawi wa jamii kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinakidhi na zinatolewa kwa ubora. (WAZEMBE WAWAJIBISHWE SIO KUHAMISHWA VITUO, TEUZI ZA NAFASI NYETI ZIENDANE NA SIFA NA WASIFU WA MTU).

5. Usimamizi mzuri wa haki, maslahi na wajibu kwa watumishi wote wa umma na sekta binafsi. Maslahi yaendane na gharama za maisha. (PALIPO NA HAKI NA MASLAHI USTAWI NA MAENDELEO HUONEKANA)

n.k

Tupeane sifa zinazostahili. Binafsi sipendi kusifiwa kama sijafanya la maana au nimefanya jambo ambalo ni la kawaida.
 
Back
Top Bottom