Manesi wa rufaa kutukana, kudharirisha wajawazito!

Poleni kina mama......hata kama iliandikwa ''mwanamke utazaa kwa uchungu'' naona hawa wahudumu nao wanazidisha uchungu huo, kwa kuwawekeeni mazingira magumu....but ukiangalia vizuri issue hii tatizo ni dola!

BWT...thought initially Mwana wa Mungu ni he...kumbe ni she...!
 
Tuige wenzetu ambao wazazi wa kiume wanaruhusiwa kuingia na wenzao. Tuone huyo muuguzi atakaefanya mas'hara wakati jamaa anamkazia macho!
 
Jamaniee, kwa wale ambao hamjaoa, tafuteni kwanza maisha hadi yawe mazuri ndo muoe, msikimbilie bila kuwa na pesa nyingi, kwasababu kwenye ndoa pesa zinahitajika sana hasa pale mwenzi wako akiwa mjamzito. kwa wale ambao wameoa, na pengine hawana pesa nyingi sana, au pengine wamezipata juzijuzi tu, wanaweza kukubaliana na mimi kuhusu lawama zangu kwa manesi wa hospitali za rufaa hapa tz.

Kusema ukweli, tumechoka na watu hawa. wanatutukana na kutudharirisha sana wanawake tukienda kujifungua kule. Kwa wale ambao hawana habari na jinsi inavyotokea huko, ni balaa. ukienda kule, ukaona namna wamama walivyojipanga mstari kwenye vitanda vyao, wakiwa uchi wamepanua mapaja yao kule na kule huku nanihii ikiwa iko wazi kabisaa, na manesi wakiwa hata hawajali pale mmoja wao atakapokuwa tayari anatoa mtoto. mara nyingi huambiwa aendelee tu kusukuma na matusi juuu, na kuambiwa alifurahia nanilii ya mmewe kumbe hajui maumivu, anaweza akaachwa hadi mtoto anywe maji. wengine hujitahidi hadi wanachanika, si unajua tena. wenye uzazi wa kwanza ndo kabisaa, hajui, akijitahidi kama anakosea nesi anakuja anamtandika kibao kikali na kumsaidia ati anataka kuua mtoto kwanini wakati hajamsaidia hapo mwanzo. watoto wengi wanaokufa ni manesi wanasababisha hospitalini.wanaume waoneeni huruma wake zenu.

Ukimpa Nesi kama alfu ishirini hivi, huwezi amini, wana njia zao za kusaidia kumtoa mtoto kwa mara moja tena kwa uangalifu mkubwa. utakuta wanasema huyo ni mdogo wao, na wanamtunza sana huyo mama.

vitanda vyenyewe hamna, kitanda kimoja wanaweza wakalala wajawazito wawili. na si vitanda special kwa kujifungulia sehemu zilizo nyingi. damu zinaweza kuambukizana, ni balaa tupu. kwa wale ambao hawawezi kuwapeleka wake zao aghakan hospital kwenye malaki na maelfu huko, kwakweli wanapata shida sana. Nesi ni mfalme nchi hii kwa wanawake, hata huku majumbani tu, anaweza akakopa hadi hela kwa watu hakataliwi,kwasababu ukileta nyodo hujui utaenda hospital yao au vipi.

hivi selikali imeshindwa kuwadhibiti hawa watu? kama hawataki kazi si waache waje manesi waadilifu na wacha Mungu? watu wanatafuta kazi kila siku mbona! hadi lini? tumechoka jamani. inasikitisha. kwanza ni udhalilishaji tosha. kwa wale wanawake ambao walishawahi kuzalia hospital za selikali wanajua hili. pamoja na kwamba humu ndani watakuwa wachache kwasababu wanawake waliomo humu wengi ni wasomi na wana afford hospital za garama. naomba selikali ilifuatilie hili.kama selikali imeshindwa, basi sisi wananchi tunaweza kulikomesha wenyewe hukuhuku mtaani...na hao manesi wataona kumbe wao ni watumishi sio mamwinyi.

madhara mengi watu wanapata kwasababu ya kuzaa kwa shida inayosababishwa na manesi kutofanya kazi yao kule leba. watu wanachanika hadi waume zao wanawakimbia kwasababu maumbile yao yanakuwa yamepanuka(kama hawatashonwa). why? watu wanapata hata fistula, watu wanalaani kuzaa, watoto wanakunywa maji hadi wanafia mlangoni. ati jamani tusiongee hili kwasababu ni taboo? hiii taboo ambayo hatu iaddress tutaificha hadi lini wakati wanawake wanazidi kufa na watoto wetu wanazidi kufa? imagine umetunza mimba miezi tisa afu mtoto anakufa wakati wa kujifungua, au waifu wako anakufa au anaharibika sehemu za siri? tuifanye tabooo? Mungu atawahukumu ninyi manesi.



kama mtu maisha hayajawa mazuri mpaka40's asubiri tu? haijakaa vizuri hiyo!

hayo ni mambo ya kawaida kabisa kwenye hosp za serikali, mjazano humo vyumbani ni hatari tupu, lakini pia zina umuhimu wake, mie frnd wangu ana uwezo mkubwa tu kifedha na alianzia clinic kwenye hosp za private mpaka anakaribia kujifungua alikuwa amevimba/kama amejaa maji mwilini, hiyo hiyo hosp ya private ilimshauri aende kwenye hosp za kawaida mana wao walishindwa kujua tatizo, akakimbizwa KCMC kumbe alikuwa na tatizo fulani ambalo ma docs wa huko private walitakiwa waligundue tangia mimba ikiwa na miezi 5 lakni hawakuligundua zaidi ya kumpa bed rest kila anapoenda, na alijifungua baby salama tu huko KCMC but ndio pesa mbele huduma ifuate.
 
Tuige wenzetu ambao wazazi wa kiume wanaruhusiwa kuingia na wenzao. Tuone huyo muuguzi atakaefanya mas'hara wakati jamaa anamkazia macho!


ukiingia kwenye ward ya wajawazito mwenyewe utakmbia, huo mlundikano humo ndani,wengine wamelala chini uchi, wengine wawili/watatu kitandani uchi, hizo leba zenyewe ni wawili/watatu kwa mpigo, hayo labda kwenye hosp za private, hizi ze2 hazifai kabisa kwa hiyo dizaini.
 
nitashangaa kuona kuna mtu humu ndani anawasapoti manesi...kuna jamaa hapo juu kasema ati manesi wasitwishwe lawama. sijui jamaa kaona mkewe nesi? kama wanashindwa kazi waache, kuna watu jobless kibao tu mtaani huko wanaweza kuwa manesi wazuri.
 
Back
Top Bottom