Maneno ya Ujumbe wa Mh. Zitto kwa Viongozi Maswi na Prof. Muhongo hauna maadili ya Uongozi!

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Katika Gazeti la leo la Majira kuna ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Mh. ZZK kwenda kwa Katibu Mkuu wa Nishati na Waziri Mhusika wa Wizara Bw. Maswi na Prof. Muhongo.

Naomba kuunukuu

“Maswi, sijawahi gombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana, tuhuma ambazo wewe na Waziri wako mnatoa dhidi yangu ni uwongo, uzushi na za kupikwa.

Mwambie Waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachoamini, sina bei tupambane tu tuone nani ataumia,”


Hebu tuchambue busara ya kiongozi iko wapi katika maandishi hayo katika mizani za kawaida pasipo ushabiki?.Naamini kama ZZK amepata washauri wake pengine ni SHETANI pasipo shaka.
 
dogo kakosea tena

yeye ni chembe tu... akina maswi wako na serikali... haijawahi tokea an individual kupambana na serikali na kushindwa, hasa mtu mwenyewe akiwa na ego na pia akiwa a lone ranger, no matter how good he/she is

ZZK kuna sehemu kateleza, badala ya kuiangalia, yuko bize kupambana na utelezi na kulaumu mvua

RETREAT IS THE BEST THING FOR NOW
 
Kama ni kweli basi kuna kila dalili kijana hausiki na mgao wa mlungula
 
Kwa mtizamo wangu sijaona hajakosea sana, isipokuwa ningekuwa mimi ningepunguza ukali wa maneno kdg
 
Muda si mrefu huyu Muhongo ataumbuka kwa kulidanganya bunge. Anasema TANESCO wana hela ya ziada hata baada ya kulipia gharama zao wakati pesa wanayolipia umeme hawa kina Symbion na capacity charges zinamaliza mapato yote ya TANESCO kabla hawajalipa hata mishahara.Tuelezwa mmiliki wa PUMA ni nani!
 
Zitto kaingiwa na roho mtaka urais.
Zitto ana price tag.
Zitto hajielewi.
Tamaa na uchu wa madaraka vinamfanya awe muumini mkubwa wa uchawi wa yule mama wa CCM Kigoma.
Waswahili walisema, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Huu ndo mwisho wa Mzee wa Hummer 3
 
MMh MMh MMH isije ikawa ni ile mashine ya kufanya maigizo ya message,lakini kama ni kweli aliandika basi huyo bwana mdogo ni cocky anatuuonyesha wananchi kwamba ni zaidi ya tumjuavyo
 
Mimi nadhani hii inaonyesha uhakika alionao kuwa hajachukua mlungula. Kwani kama wana uhakika na tuhuma hizo basi hapa lazima watatoa ushaidi.
Ni vizuri ZZK kujisimamia mwenyewe. He has to fight for his political life.
 
hata mie ningeki\ua ZZK ningekula.kama tumesoma history na tukaelewa machungu walipata waafrika wa awali wakati wa ukoloni, afu bado migodi mikubwa na serkali yetu kuendelea kukosa meno kwa kuwasaidia wanyonge kwa nini atezeke. kama ni kweli mwache ale.. hilo ndio NSSF yake
 
Gagnija ,Kama unataka mmliki wa PUMA nenda BRELA ,its very simple to countercheck,lakini kama wewe siyo mvivu.
 
Last edited by a moderator:
Sina uhakika na kauli za utata za Mh.Zuberi Zitto Kabwe, kwa hili anahitaji aeleze kwa ufasaha ni yepi aliyokuwa anashabikia? na kwa manufaa ya nani? aidha anatuimanisha nini kama anastahili kuendelea kutumikia wananchi wake? Asiye mwaminifu kwa kidogo, utamwamini vipi kwa mambo makubwa?
 
dogo kakosea tena

yeye ni chembe tu... akina maswi wako na serikali... haijawahi tokea an individual kupambana na serikali na kushindwa, hasa mtu mwenyewe akiwa na ego na pia akiwa a lone ranger, no matter how good he/she is

ZZK kuna sehemu kateleza, badala ya kuiangalia, yuko bize kupambana na utelezi na kulaumu mvua

RETREAT IS THE BEST THING FOR NOW

I put my signature under your valid comments
 
Zitto kaingiwa na roho mtaka urais.
Zitto ana price tag.
Zitto hajielewi.
Tamaa na uchu wa madaraka vinamfanya awe muumini mkubwa wa uchawi wa yule mama wa CCM Kigoma.
Waswahili walisema, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Huu ndo mwisho wa Mzee wa Hummer 3

Put yourself in ZZK shoes. Kama unauhakika kuwa hujachukua pesa alafu mtu anakupakazia uongo mkubwa kama hivi utatumia lugha gani kufikisha ujumbe wako. Mimi hapa sioni tatizo as long as hajachukua hiyo pesa. Maneno ya mheshimiwa mheshimiwa ndo yanatufanya kuwa na nidhamu wa woga.
 
Back
Top Bottom