Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,821
- 59,424
bahati mbaya ugomvi mwingine huzuka sehemu ambayo haikupi wasaa wa kutafakari; kwenye kadamnasi ya watu...........usiku wa manane!
Nyote wa wawili mmenena mambo muhimu sana lakini tunahitaji kusaidia njia za haraka za kudhibiti hizi hasira
Wasaa upo sana MJ..tatizo ni utayari wa watu kuutumia.
Kunyamaza is the best thing you can do badala ya kuanza kurusha maneno.
Kama ni kwenye kadamnasi we nyamaza ikiwezekana simama ondoka eneo hilo...waliokuzunguka wanaweza kukuona zoba/mwoga but it's better and safer that way on the long run. Kama mko nyumbani/chumbani geukia TV yako..hama chumba...toka nje yani kwa vyovyote vile epuka kureact wakati hasira imekufika machoni.
Binafsi kama sitaki kuondoka nilipo hua namwambia kabisa mtu aliyenikasirisha asiniongeleshe.
Na mimi sitaongea mpaka ntakapohisi nafuu...kwamba sasa naweza ongea na hata kama ni kumsema huyo mtu ntafanya hivyo reasonably. Ntasema yale nnayohitaji ayasikie though yanaweza kumuuma nia yangu haitakua kumuumiza bali kumfanya ajifunze/elewe ubaya wa kilichotokea kabla. And yes....watu wa aina hii hua tunaonekana tuna kiburi ila ni kwa faida ya wote!!!