Hiki kitu niliwahi kusema hawa jamaa walipoanza kuleta ushikaji tu katika kazi ndio walipoua timu.

Unampaje kilaza kama Ed Woodward akuendeshee klabu kubwa ya soka kama Manchester United?

Ndani ya miaka 10 ya Ed kama mtendaji mkuu wa timu thamani ya United imeshuka sana hatujashinda taji hata moja la EPL.

Sheikh Mansour anamchukua Ferran Sorriano kutoka Barcelona ya moto aje amuendeshee timu ndani ya miaka 10 chini yake Manchester City tayari wamebeba EPL 5 jumlisha na mataji mengine 10 chini yake yaani chini Ferran Sorriano City wamebeba makombe 15.

Ferran Sorriano alianza kazi na Ed Woodward kwa wakati mmoja walipishana miezi michache tu ila ndani ya miaka 10 tokea 2012 tayari Ferran Sorriano amebeba EPL 5, Ed Woodward mpaka anaondoka ofisini hajabeba hata moja.
Hata Chelsea iliponunuliwa na Roman Abromovic alimchukua mtendaji mkuu David Dein kutoka Man u, ila man u tunamatajiri vilaza sana
 
We ferdinand we waache tuone watachofanya...
Screenshot_20220822-210727_Facebook.jpg
 
Naamini EtH ndio kocha na anawajua wachezaji wake kuliko mimi ila nadhani ana tatizo kwenye upangaji wake wa timu.

Acha nisubiri apatiwe wachezaji anaowataka nione vituko.
 
Naamini EtH ndio kocha na anawajua wachezaji wake kuliko mimi ila nadhani ana tatizo kwenye upangaji wake wa timu.

Acha nisubiri apatiwe wachezaji anaowataka nione vituko.
We unataka nani apangwe magwaya au Fred maana sio makosa wamepewa nafasi alafu wanazingua
 
Naamini EtH ndio kocha na anawajua wachezaji wake kuliko mimi ila nadhani ana tatizo kwenye upangaji wake wa timu.

Acha nisubiri apatiwe wachezaji anaowataka nione vituko.
Kwahiyo anajiona kapatia mwenyewe kumuweka Eriksen kama CM wakati wenye nafasi zao wapo.

Timu kama man utd inaingia na AMF wawili dhidi ya Liverpool. Ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom