Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inasaka zaidi ya Sh. bilioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mashine

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,976
32,379
Wanaukumbi.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), inasaka zaidi ya Sh. bilioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mashine za Kieletroniki za kodi (EFDs) 200,000, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli alilowataka wazitoe bure kwa wafanyabiashara.

Rais Magufuli alipokutana na wafanyabiasharawa Taasisi ya sekta Binafsi nchini (TPSF) mwishoni mwa mwaka jana, alipendekeza TRA itoe bure mashine hizo ili mamlaka iangalie mapato kutoka kwao.

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, akizungumza jana ofisi kwake alisema wanaendelea kufanya utaratibu wa kupata fedha hizo.“Wanaohitajika kupewa mashine ni 200,000 ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili… wafanyabiashara watakaopata ni wale wasiosajiliwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ” alisema.

Alisema mara baada yakupata fedha hizo watapanga utaratibu wa jinsi ya kuzigawa na kuzihudumia.Aliongeza kuwa, wale ambao walinunua mashine hizo kwenye awamu ya kwanza, tayari wamerejeshewa malipo ya gharama za mashine hizo walipopeleka marejesho ya kodi.

Source: TRA
 
Hahaaa haa Magufuli alisema kimashine hiko si laki nne tu?

Hahaa kweli usilolijua ni usiku wa giza...

masuala ya uchumi hayaendi kwa amri tu za Rais.....

Magufuli ananikumbusha yule mtu alieona kuna jamaa kaoa mke halafu anampa amri...'leo upike kuku'
mara leo upike pilau'

Jamaa na yeye akakukurupuka kuoa akifikiri ukishaoa ni amri tu kwa mkeo

na yeye akatoa amri leo pika kuku...akarudi akakuta ugali unamsubiri..

kumbe mwenzie kabla ya amri za hadharani huacha pesa za kutosha na amri zake

yeye mkewe hajamuachia kitu akaibuka tu na amri leo pika kuku.....

Sasa kumbe ni bilioni 100 zinahitajika...wakati bilioni 100 za elimu bure tu hazijatosha
 
Siasa ni mchezo mbaya sana, hasa kwa mataifa haya machanga ambayo rais ni kama Mungu, rais anaweza kusema kitu kama anashaur tu au akaongelea mtazamo wake ambao kiukweli wakat mwingine unaweza usiwe sahihi lkin kwa vile ni africa hiyo inakuwa ni maelekezo na lazima yafuatwe, ktk mfumo kama huu kiongoz anatakiwa aandikiwe mambo ya kusema manake sentesi zake hata mbili tu zinaweza kuleta crisis, hebu fikiria mashine ina faida zaid kwa wafanyabiashara, sababu ni tool pia ya ku keep records za biashara zao, kodi ya nchi ni lazima lkin eti wao wapewe bure, mbona wafanyakazi wanalipa kodi wengine zaid ya milion kwa mwezi, na ndio kodi inayoongoza hawana privilage yoyote? Hili kwa mtazamo wangu alitoa wazo lilipaswa kufanyiwa analysis mapendekezo yatolewe, kama wawe subsidized na kiwango flan ambacho kitakuwa kinapunguzwa kwenye kodi, sa ww utoe bure matengenezo kwa nani, na how sustainable will it gonna be, halaf hizo ni kodi zetu wananchi tunapswa kutoa idhin kupitia bunge. Hii nchi kutoka itatuchukua muda sana.
 
Kutokana na makadirio ya makusanyo ya TRA , 100 bilions ni makusanyo ya chini ya siku tatu. Lakini vile vile hela kiasi kama hicho kinahitajika kutanulia uwanja wa ndege wa Mwanza ambao umesimama tokea May 2015 mkandarasi anataka alipwe 17 Bilions tu aendelee na kazi. Lakini serikali iko tayari kutoa 6 Bilions kwa uchaguzi wa Zanzibar.
 
Huu utaratibu wa serikali kutoa vitu bure utakuja kutusumbua sana kwani unarudisha utegemezi wa kizembe hasa kwa.watumiaji wa vitu kutegemea vya bure.Mf ni Elimu bure
Mashine ni uwekezaji...
 
Mkuu bilion 100 kwa mashine 200,000 ni elfu 50? mbona hulitendei haki jukwaa?
Ama kweli mwisho wa fedheha ni aibu. Kwa hesabu hiyo kumbe kila kimashine kimoja kinagharimu Tsh 50,000 tu. Duuuh! hawa jamaa walikuwa wanaiuza Tsh 600,000.

Jambo la pili ni kuwa kutokana na makadirio ya makusanyo ya TRA , 100 bilions ni makusanyo ya chini ya siku tatu. Lakini vile vile hela kiasi kama hicho kinahitajika kutanulia uwanja wa ndege wa Mwanza ambao umesimama tokea May 2015 mkandarasi anataka alipwe 17 Bilions tu aendelee na kazi. Lakini serikali iko tayari kutoa 6 Bilions kwa uchaguzi wa Zanzibar.
 
Huu ni ubabaishaji, yaani TRA hawawezi kuongea na BOT/Banks ili hizo machine zipatikane? Rais alitoa mapendekezo kwa ''nini wasipewe bure'' alikuwa na maana kwamba kwanza wanalipa kodi wakiwekewa na pili hiyo kodi inarudi kwa muda mfupi sana. Kwa nini kuwe na vikwazo? Ukweli wa mambo tumekosa wabunifu tu. Wanaotakiwa kuwa na hizi mashine wangeambiwa waende Bank wazipate kwa mkopo ambao utalipwa na TRA baada ya mwaka moja au vingenevyo kutokana na marejesho yao ya kodi.

Watu wanataka watafuniwe hata chakula ambacho kiko mdomoni mwao. Pathetic! JPM was right, the problem ni TRA ambao hawana viongozi wenye upeo wa kufikiri na kutekeleza mapendekezo ya rais. Hapo lilikuwa ni swala la kuwaambia wafanyibiashara kwenda kwenye bank zao na kufanya hiyo changamoto kufanikisha hilo zoezi.
 
Kilichokisababisha utoke mapovu ya mdomo wa chini mimi sikioni

Makosa ni mengi kwanza ulitoka povu na kusema machine ni elfu 50, baadaye unarudi na kusema my bad. That is not acceptable for a Great Tinker! unaishushia hadhi hii Forum. Khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Makosa ni mengi kwanza ulitoka povu na kusema machine ni elfu 50, baadaye unarudi na kusema my bad. That is not acceptable for a Great Tinker! unaishushia hadhi hii Forum. Khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Thats why we are called humans! Sijui Jecha keshafanya makosa mangapi kwa kipindi cha miezi miwili hii. Jee haivunjii hadhi Zanzibar, Tanzania kwa jumla pamoja na chama tawala?
 
Tanzania ina udhaifu mkubwa sana kiuongozi na wala hakuna haja ya kudanganyana kwamba eti ikitoka CCM madarakani halafu chama kingine kikija ndio utakuwa muarobaini wa matatizo yetu. Hao wanasiasa wa upinzani ambao kwa sasa wanaoneka kuwa mbadala wa matatizo, wamekuzwa na wanasiasa pamoja na wataalam ambao ni wanaCCM. Wamepewa ushauri mwingi kabla ya wao kuonekana kuwa ndio suluhisho la matatizo ya nchi. Tunapungukiwa na rasilimali watu yenye uwezo wa kuendana na mahitaji ya ushindani wa kimataifa wa utafutaji wa maendeleo. Hao wanaonekana kuwa pembeni wakiwaaminisha watu kuwa wao ni mbadala wa sera za CCM, na wao ni wepesi sana. Tatizo litakaloweza kumsumbua Magufuli na marais watakaofuata ni ukosefu wa uwezo wa kuzalisha tija wa wasomi wetu, yapo mengine kama vile ukosefu wa uzalendo, kulewa madaraka mapema lakini tatizo kubwa ni incompetence inayoonyeshwa na baadhi ya wasomi wetu. Prof Ndalichako na wasaidizi wake wana kazi kubwa kwani matatizo ya kuzembea katika elimu yetu kwa sasa yanajionyesha kupitia udhaifu wa wasomi wanaoendelea kuandaliwa.
 
Zikiwa bure serikali itachemsha, ikiharibika wanatengenezewa au? na je ikiharibika beyond repair wanapewa mpya au?
 
Zikiwa bure serikali itachemsha, ikiharibika wanatengenezewa au? na je ikiharibika beyond repair wanapewa mpya au?

JPM alipotoa ushauri hakusema wapewe bure tu, alipima mizani yaani huyu mfanyabiashara analipa kodi kiasi gani akiwa na hii machine. Je asipokuwa nayo pengine halipi kabisa. Ukipima hiyo mizani utaona TRA watachukua kodi kwa wingi zaidi kama watawapa bure kuliko kungoja wao wanunue kwa hiari yao. Hapo ni kuagalia mbali zaidi unaweza kuweka vipengele vya hiyo bure.

Je, hivi sasa asiyekuwa na hiyo machine analipa TRA kiasi gani? Je, kuna njia ya kuhakiki kwamba hadanganyi?
 
Back
Top Bottom