Mambosasa: Kilichopelekea mwanafunzi wa UDSM akamatwe ni kusambaza uzushi mtandaoni

Ndio tumefikia hapa, yani mtu haruhusiwi kuongelea madhaifu ya sehemu husika na kuonesha hatari inayoweza kutokea huko mbele? Mtu kabisa ndani ya nchi yake?
Umenena. Mbona hawakamati jicho la mwewe?
 
724e56f52420553c9b01ec0c78e01bdd.jpg
 
Stupid!
Uzushi na mkurugenzi amekiri.
Bila hizo picha wangejua kuwa mijumba yao ni MCHANGA MTUPU.
 
Uzushi ni habari ambayo si ya kweli. Akajifunze kiswahili huyu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dar Lazaro Mambosasa amesema walimkamata mwanafunzi Kumbusho Dawson baada ya kusambaza uzushi kwenye mtandao,

Kamanda ameelezea kama mwanafunzi huyo angekuwa na taarifa yoyote basi angeipeleka kwa mkandarsi wa majengo au mmiliki wa majengo hayo

Mtu aliyekuwa alalamike ni mmiliki wa majengo hayo na sio yeye

Pia amesema ameshangaa watu kulalamika na kupokea usumbufu mkubwa kwa jambo hilo wakati kuna maghorofa makubwa hapa Dar yalishaanguka na kuumiza watu lakini hakuna watu hawakuonyesha kuvutika kama ilivyokuwa kwa jambo hili

Uzushi upi sasa kwani jengo ndio lilijengwa vile???Nyie police hao CCM wanawadanganya sana
Polisi hawana ujuzi wa ujenzi kwa hiyo wameamini kwamba jengo lile limejengwa kisasa linaweza kupasuka na kujiziba kama alivyosema engineer wa TBA
 
Hivi mtu mzima na akili timamu, mwenye watoto pengine na wajukuu.. unasimama mbele ya kamera za Waandishi wa habari kutetea upuuzi kama huu...!!

Ni kitu gani kimewakumba watu hawa... Inasemwa siku zote mtu mwenye taarifa za ujambazi azitoe iwe police au public... Kijana huyo kutumia hadhira kufikisha taarifa ambazo yamkini watu wa kwanza kudhulika endapo maafa yangetokea ni wao wanafunzi.... we unataka mwenye nyumba alalamike..na mwenye nyumba hakai hapo..!! Epushia mbali ukweli kwamba yeye tayari anamaslahi na jengo hilo ambapo haiwezekani akatoa taarifa mbaya zirakazosababisha kukimbiwa na wapangaji..!!

Ukweli mdogo kama huu ni kweli Mambosasa sasa anashindwa kuuona? Jamani cheo cha Kamishina mbona ni kikubwa kuliko huu utetezi wa Mambosasa... Nini kimewakumba police???

BACK TANGANYIKA
Mkuu mi nadhani hata hao waandishi wanaitwaga kwenye press conference za hivi TUWACHeNJIE, ina maana wao huwa hawa ulizi hata maswali kutoa utata wataarifa wanazokusanya.....

BBC swahili uwaite kwenye press conference uongee hujajipanga, lazma upigane kama sio kuwanyanganya cameras zao...
Stupid Media za Bongo...
 
Kwa kifupi utawala huuu unataka kutengeneza kizazi cha watu waoga wasioweza kuhoji chochote! Sasa najiuliza hii ni kwa faida ya nani ?
Ni kweli ameishatengeneza kizazi cha waoga hasa ndani ya ccm ni serikali yake kwani hakuna na namaanisha hakuna hata mmoja ndani ya chama na serikalini anayehoji chochote zaidi ya kupiga makofi na kutabasamu.
Amewaweza ccm na vijitawi vyake kama polisi na vinginevyo! Nashauri polisi wabadilishe sare wavae kijani na nyeusi kuliko kuendelea kuvaa sare za mkoloni! Hii itapendeza zaidi kwani kila atakayewaona hatohoji juu ya kufikiri kwao kama balozi wa nyumba kumi!
 
Hakuna ujenzi wa kisasa unaoruhusu nyufa wewe! Acha kuandika uongo.

Polisi hawana ujuzi wa ujenzi kwa hiyo wameamini kwamba jengo lile limejengwa kisasa linaweza kupasuka na kujiziba kama alivyosema engineer wa TBA
 
Yule Mambosasa alikua kipa bora sana huyu Mambosasa kauli zake akikakaa dakika tano mbele anaweza kuzikataa...
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Dar Lazaro Mambosasa amesema walimkamata mwanafunzi Kumbusho Dawson baada ya kusambaza uzushi kwenye mtandao,

Kamanda ameelezea kama mwanafunzi huyo angekuwa na taarifa yoyote basi angeipeleka kwa mkandarsi wa majengo au mmiliki wa majengo hayo

Mtu aliyekuwa alalamike ni mmiliki wa majengo hayo na sio yeye

Pia amesema ameshangaa watu kulalamika na kupokea usumbufu mkubwa kwa jambo hilo wakati kuna maghorofa makubwa hapa Dar yalishaanguka na kuumiza watu lakini hakuna watu hawakuonyesha kuvutika kama ilivyokuwa kwa jambo hili

Taifa la wajinga usitegemee kuona unayoyataka
 
Huwezi kinijibu hivyo mimi, tumeshasema ni expansion slot, ila tutachukua hatua ya kukarabati....

Naona hizo Expansion slot zinavyozidi kutanuka na ninyi mnazidi kutamani kuongelea...

Sasa kwa kumshikilia huyo kijana wanategemea baridi ije ili zijizibe.....

Time will tell
 
Tatizo sio taarifa ya hizo nyufa, issue Dogo ni wa chama kile in Mwakalinga's voice.
 
Back
Top Bottom