EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Nimesoma sheria za JF sijaona sehemu na adhabu ya mtu anayeleta vitu vya uzushi, uongo, picha fake nk. Ama nimekuwa nikiona thread za uzushi zikihamishwa au kuondolewa bila ya mhusika kupewa adhabu. Hii inaashiria nini, kwamba ninaweza kuleta mambo hayo bila wasiwasi wowote kwa vile najua hakuna adhabu itakayotolewa zaidi ya thread yangu kuhamishwa. Mtu analeta thread kuwa kuna chama kinampango wa kuingiza silaha bila ushahidi na bila kufanywa chochote ni hatari kwa usalama si kwa JF tu bali na nchi kwa ujumla.