Mambo ya kuzingatiiwa na DEREVA unapokaribia alama za ZEBRA

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
FACT KUHUSU ZEBRA
1. Punguza mwendo unapoikaribia zebra ili angalau uwe katika mwendo wa uwezekano wa kusimama ikiwa kuna mtu atakuwa anavuka barabara au kutaka kuvuka barabara. Kisayansi mwendo unaokuwezesha kusimama kiurahisi ni 50kph (approach speed)
2. Angaza kulia na kushoto kuona kama kuna watu wanaosubiri kuvuka au wanavuka;
3. Iwapo kuna mtu anasubiri kuvuka (is about to use) au anavuka (or is using a pedestrian crossing) kwenye zebra, SIMAMA KUMPISHA AVUKE. [Maana yake ni kwamba ni lazima wewe usimame kwanza ili yeye avuke au aanze kuvuka. Am,a kama utamkuta katikati au anamalizia kuvuka acha amalize kuvuka][kif.65(10)RTA 1973.
4. Usimpigie honi au resi dereva aliyesimama kupisha watu kuvuka kwenye kivuko (zebra)
5. Usimpite (ovateki) dereva aliyesimama kupisha watu kuvuka kwenye kivuko.
6. Muashirie dereva mwenzio kusimama, iwapo unahisi amekupuuza anataka kukuovateki ukiwa umepisha waenda kwa miguu;
8. Usimpigie honi au resi mwenda kwa miguu anayevuka ili aharakishe kuvuka
9. Iwapo kivuko kinaongozwa na taa, na taa ya Kijani imeshawaka kukuruhusu ilhali bado mwenda kwa miguu hajamaliza kuvuka, usiondoe gari hadi mwenda kwa miguu amalize kuvuka.
4078d3038bed49ffe7c6c4793d3f5761.jpg
 
Kuna mtu mmoja aliniambia eti zebra mwisho ni saa 12 jion, zebra ni Muda wa serikali tu je ni kweli
 
Kuna madereva wapuuzi sana, hawaheshimu kabisa zebra cross hasa hawa wanaokuwa na vipasso au vigari vilivyokaa kama mkate, pamoja na vidada!
Madereva wa malori makubwa kwa kweli huwa wanaheshimu sana zebra...
 
ninyi mnazungumzia viZEBRA vya mijini na majiji
toka upige mbaula gia 12 Dar- Bukoba au Tunduma utasimama viZEBRA vingapi km hukumaliza wiki bado upo TZ
kuna maeneo kuna viZEBRA mpaka vya wauza mikaa, bado Bumps bado 50
hilo gari litaumia si breki, shock-up, tairi
acheni kuna mateso sasa kuendesha gari katika barabara za TZ iwe mchana au usiku kutegewa mawe. unaambiwa ni marufuku kuyaruka.
Leo wapo waliowashwa risasi huko Muhimbili kwa ajili ya ZEBRA
 
Mkuu yani bomang'ombe zebra cross ipo mbele ya kituo lakini kukuta dereva anasimama ili upite labda gari za kitali ndo huwa xinasimama ila hao wengine ni mwendo wa honi tu tena na police yuko nashuhudia
 
Polisi traffic ndio mzembe yeye alitakiwa afanye law enforcement
 
Kuna madereva wapuuzi sana, hawaheshimu kabisa zebra cross hasa hawa wanaokuwa na vipasso au vigari vilivyokaa kama mkate, pamoja na vidada!
Madereva wa malori makubwa kwa kweli huwa wanaheshimu sana zebra...
Wengi wao sio madereva mkuu ni waendesha magari, ili uwe dereva lazima upitie mafunzo ya udereva sasa wengi wao wenye hivi vigari vidogo unakuta amenunua tu kajifunza kuweka "D" ni kuendesha na kulengesha gari barabarani anaenda kununua leseni yake TRA. Hawa wa magari makubwa kidogo ndio huwa na changamoto, si rahisi kununua leseni na hata kupata ajira kiuzembe lazima uwe dereva kweli (japo wapo wanaozingua pia)
 
Kuna madereva wapuuzi sana, hawaheshimu kabisa zebra cross hasa hawa wanaokuwa na vipasso au vigari vilivyokaa kama mkate, pamoja na vidada!
Madereva wa malori makubwa kwa kweli huwa wanaheshimu sana zebra...
Wakipigwa faini wanalalamika eti traffic wamekuwa tra huku wao wakiwa hawatimizi wajibu wao
 
FACT KUHUSU ZEBRA
1. Punguza mwendo unapoikaribia zebra ili angalau uwe katika mwendo wa uwezekano wa kusimama ikiwa kuna mtu atakuwa anavuka barabara au kutaka kuvuka barabara. Kisayansi mwendo unaokuwezesha kusimama kiurahisi ni 50kph (approach speed)
2. Angaza kulia na kushoto kuona kama kuna watu wanaosubiri kuvuka au wanavuka;
3. Iwapo kuna mtu anasubiri kuvuka (is about to use) au anavuka (or is using a pedestrian crossing) kwenye zebra, SIMAMA KUMPISHA AVUKE. [Maana yake ni kwamba ni lazima wewe usimame kwanza ili yeye avuke au aanze kuvuka. Am,a kama utamkuta katikati au anamalizia kuvuka acha amalize kuvuka][kif.65(10)RTA 1973.
4. Usimpigie honi au resi dereva aliyesimama kupisha watu kuvuka kwenye kivuko (zebra)
5. Usimpite (ovateki) dereva aliyesimama kupisha watu kuvuka kwenye kivuko.
6. Muashirie dereva mwenzio kusimama, iwapo unahisi amekupuuza anataka kukuovateki ukiwa umepisha waenda kwa miguu;
8. Usimpigie honi au resi mwenda kwa miguu anayevuka ili aharakishe kuvuka
9. Iwapo kivuko kinaongozwa na taa, na taa ya Kijani imeshawaka kukuruhusu ilhali bado mwenda kwa miguu hajamaliza kuvuka, usiondoe gari hadi mwenda kwa miguu amalize kuvuka.
4078d3038bed49ffe7c6c4793d3f5761.jpg
5 Mkuu kuna wadaladala anasimama tu kupakia abiria huku hakuna wavukaji kaenda kwa mguu,mi nawaovateki tu ila nikiwa na uhakika hakuna mvukaji
 
dodoma zebra zinazo heshimika ni mbili tu,
ya jamatini na zebra ya relini kama unaenda mahakama kuu opposite na kanisa.
 
Back
Top Bottom