Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Nimeuliza mara kadhaa humu kwa wanaoifahamu KATIBA ya CCM. Kamati kuu inaweza kujiuzuru mwenyekiti wake akabaki?
 
Holly Crap.
Hakuna kujivua gamba bali hapo ni kupaka rangi gamba. Hao watu mnaosema kuwa mmewasafisha bado wako ndani ya chama. Walitakiwa kuvuliwa madaraka, uanachama na kufikishwa mahakamani kwa kusababishia Taifa hasara.

Hilo game CCM inalocheza linaitwa MDAKO 2.0, unaondoa vi-mawe kwenye kijishimo halafu unavirudisha tena kwenye kijishimo kwa staili tofauti ya vidole. Huwezi kutuambia kuwa umesafisha chama wakati unamrudisha Zakia Meghi (Mama Mkwe), Kinana ambaye naye ana gamba lake analotakiwa kulivua, Lowassa bado anashikilia Kamati nzito ya Bunge, fisadiz wengine bado ni wabunge na wanachama wa CCM. Na visadi mkuu bado anawatambia kuwa vita ndo imeanza. Kazi kwenu.

CCM wameshindwa kujitakasa, wasubiri Tsunami ya ndani kwa ndani.
 
'MIMI NANG'ATUKA ILA WOSIA NNAOWAACHIA NI KUWA BILA CCM IMARA TZ ITAYUMBA'dat kind of a speech was given by Mwalimu JK Nyerere,jamaa wameshtuka leo kuwa bila CCM imara maneno ya Mzee Nyerere yatatimia dat y wameamua kumwagana.well done JAkaya katika hili.

Am missing some links ... Kuondoka kwa Makamba, Chiligati, na Membe na kuwaingiza Mkama (aliyekuwa tawala za mikoa akavuruga), Meghji (aliyekuwa fedha maji yakawa mazito) na Nape (waliyemtema wao wenyewe) kunaiimarishaje CCM yenye kina RA na EL na Vijisenti? Naomba mwongozo!
 
Holly Crap.
Hakuna kujivua gamba bali hapo ni kupaka rangi gamba. Hao watu mnaosema kuwa mmewasafisha bado wako ndani ya chama. Walitakiwa kuvuliwa madaraka, uanachama na kufikishwa mahakamani kwa kusababishia Taifa hasara.

Hilo game CCM inalocheza linaitwa MDAKO 2.0, unaondoa vi-mawe kwenye kijishimo halafu unavirudisha tena kwenye kijishimo kwa staili tofauti ya vidole. Huwezi kutuambia kuwa umesafisha chama wakati unamrudisha Zakia Meghi (Mama Mkwe), Kinana ambaye naye ana gamba lake analotakiwa kulivua, Lowassa bado anashikilia Kamati nzito ya Bunge, fisadiz wengine bado ni wabunge na wanachama wa CCM. Na visadi mkuu bado anawatambia kuwa vita ndo imeanza. Kazi kwenu.

CCM wameshindwa kujitakasa, wasubiri Tsunami ya ndani kwa ndani.

I cannot add more! Thanx
 
Siku akijiuzulu Jakaya Kikwete ndio siku nitaanza kufikiria kuipongeza CCM lakini kwa hii Comedy ya kumuondoa Makamba and allies bado! kama alivyosema Mbowe kule Dodoma, tatizo la CCM sio kwenye Gamba ni damu, ugonjwa wa CCM uko Damuni! kwa hivyo kujivua gamba ni sawa na kuweka mvinyo mpya kwenye chupa ile ile!
 
CDM kanyaga twende mpaka kieleweke. Watagombana hadi wabadilishe hata mavazi ya kijani na kuvaa ya kahawia.
 
Lowassa yupo Chama gani?
Chenge nae?
Rostam?
Riz 1
Makamba?
Meghji
.......
......
.......

Chama kimesafishika au kimezidi kujipakaza m*vi?
 
Maandamano nitawarushia maji machafu nikiwa ghorofani kwangu hapa magomeni maana lazima mtapita hapo; maana ni uchafu RA/Lowasa/Chenge bado wapo halafu mnasema mmezaliwa upya; jaribuni muone

Je Kipengele: mbona sikuona kumlaumu makamba alipokuwa badi yupo? kama hukumpenda kiasi hicho; au wewe ni wale bora liende na sasa unatafuta kupiga kelele mpya kesho mkama akiondoka unaanza tena maandamano?
 
tusidanganyane hata kidogo , kuku kuku tu jogoo jina, ccm ni ile ile tu, hakuna lolote!
 
CDM kanyaga twende mpaka kieleweke. Watagombana hadi wabadilishe hata mavazi ya kijani na kuvaa ya kahawia.

na hatimaye kuvaa BLUE kabisa kama wenzao vodacom waliofikia kupiga red red ka airtel
 
Tanzania inazaliwa upya Thanks Jakaya

Thanks for what? :angry: Mbona mafisadi wote akina Lowassa, Chenge, Karamagi, Rostam, Mkapa, Yona, Mkono na wengineo wegi mmeshindwa kuwafukuza ndani ya chama chenu cha mafisadi!? Hatudanganyiki kabisa CCM bado ni ile ile ya mafisadi kabla ya Makamba na timu yake kujiuzulu na hata baada ya kujiuzulu kwao. Na uozo wanaoufanya ndani ya nchi yetu miaka nenda miaka rudi utaendelea kuwepo.
 
Wadau mwenye updates zaidi ya nyoka aliyejivua gamba al-maarufu ccm mpaka sasa?
 
Kujiuzulu kulitakiwa kuanzie kwa mwenyekiti. Kwani chama kinaongozwa na Sekretariet tu? Ni nini majukumu ya Mwenyekiti hadi chama kikafikia hapo kilipo?

Mwenyekiti aelewe kitu kimoja kuwa wanaokuambia kuwa uwaondoe kina Makamba wanakuogopa wewe (kumekosekana ujasiri wa kumwambia mfalme kuwa uko uchi). Tatizo kubwa ni kuwa chama unachokiongoza kimegawanyika au kwa maneno marahisi ni kuwa kimeparaganyika. Maana yake ni kuwa viongozi wa juu mko na mambo yenu na wanachama wako na mambo yao. Kama chama mlitakiwa kwenda kwa pamoja bila hivyo matokeo yake ni hayo.

Viongozi wa juu wa CCM mnasimamia kutekeleza sera za kifisadi na rushwa wakati wanachama hawayataki hayo kwa sababu hayapo kwenye malengo yao. Tofauti na na Chama kama Chadema ambacho kinawasikiliza na kuwasemea wananchi walioduni, CCM mnawawakilisha wafanyabiashara na mafisadi.

Hakika kifo chenu (CCM) hakikwepeki ila mnaishi kwa matumaini ili siku za kuishi ziongezeke. Hakika sasa hivi mtu akisikika akitaja CCM katika fikra za watu kinachokuja haraka ni ufisadi, EPA, Richmond, Dowans, RA,EL, Karamagi, Chenge. Je, CCM kina uhusiano gani na hayo?
 
Back
Top Bottom