Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Kwa mwenedndo huu: Mkama + Kinana + Nape + Nchimbi (Ms)+ Zagkhia.......matandao JK full. One important thing: I can see Lowasa being Screwed F-u-cked to the level!
 
Jamani nyoka ni nyoka tu na sifa ya nyoka ni sumu yake, kwa kule kujivua gamba nyoka anakuwa na kasi zaidi na kama ni koboko basi anaweza kudhuru wengi na hofu yangu kwa CCM kwa kuwa mwenyekiti ni yule yule sitegemei jipya zaidi ya kuongezeka kwa kasi ya ufisadi.
 
helow members jk na serikal yake wanataka kuliingiza taifa katika machafuko hamuoni kama mswada wa kuunda tume ya kukusanya maoni umegubikwa na hila na mizengwe kwa waliousoma plz
 
kweli kuna watu wanachekesha sana. hivi matatizo ya watanzania yalikuwa yanahitaji kutatuliwa kwa kubadilisha secretariat ya ccm hadi bwana mkubwa akapokelewe kwa vifijo na nderemo wakati hatujui hao waliopachikwa wata fanya nini hata basi uwezo wao upo wapi. hebu tu tuweni makini kwa kuhakikisha hatusahau mambo ya msingi ya kitaifa kama katiba, hatima ya muuungano nk. But for the case of wakereketwa wa thithiem nawatakia nderemo mema maana these ceremonies may be the last. Enjoy while you can!
 
Hivi hao vijana waliokuwa wanapigana vikumbo kutoa matamko machafu dhidi ya chadema hata mmoja mungu hakumuona kwenye hii biashara na magamba feki?
 
Mimi nachangia mada hii kutokana na avatar yako nzuri, kama hii ndiyo sura yako basi natangaza mapenzi na wewe.... vinginevyo ulichoandika ni pumba na si shangai maana mara nyingi Mungu huwa hapendelei ki hivyo (sura nzuri na brains)
 
Wanajf

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kukisafisha Chama sasa hivi kinaanza kumeremeta

Nakumbushia mkoa wa DAR es salaam kuandaa maandamano makubwa ya kumpokea na kumpongeza

Hata wanaJF wenye mapenzi mema na JK na MUkama kuwapa nguvu maana TANzania inazaliwa upya
Chama chako bado kichafu kinanuka,madon wa ufisadi bado wapo,kilichofanyika ni kupaka nyumba rangi nje ilihali ndani ni chafu na kuta zimejaa tando za buibui na makorokoro mengine
 
Hivi hao vijana waliokuwa wanapigana vikumbo kutoa matamko machafu dhidi ya chadema hata mmoja mungu hakumuona kwenye hii biashara na magamba feki?
Hawa walikuwa wanawapigania mafisadi wao wanaowapa hela ili wawaseme vizuri mbele ya vyombo vya habari
 
NEC nayo leo imeahirishwa hadi kesho na JK anayo ajenda nzito mwenyewe japo Msekwa ndiye anao utangulizi.

Maelezo ya kwanza yalihusiana na CC naomba nisiwachanganye kwa title ya thread

Mkubwa kamatia badae uendelee kutupa za ukweli mpaka kieleweke
 
Hawa walikuwa wanawapigania mafisadi wao wanaowapa hela ili wawaseme vizuri mbele ya vyombo vya habari

kwa hiyo wamelamba garasa siyo? Nguvu zote zile hadi mapovu yalikuwa yanawatoka na kukusea baba zao heshima. I love politics
 
Jamani nyoka ni nyoka tu na sifa ya nyoka ni sumu yake, kwa kule kujivua gamba nyoka anakuwa na kasi zaidi na kama ni koboko basi anaweza kudhuru wengi na hofu yangu kwa CCM kwa kuwa mwenyekiti ni yule yule sitegemei jipya zaidi ya kuongezeka kwa kasi ya ufisadi.

duuuuu
 
Ndg zangu wana Jf, ninyi ni mashaidi kuwa watoto wote wa wana siasa kawa makamba, msekwa, mongela hao ndiyo wakuu wa wilaya, wakulugenzi. Kazi kweli2
 
Nape ni opportunist tu na si vinginevyo hivyo hata awe nani ndani ya ccm hamna jipya atakalofanya labda kwa vijana wale waliolala usingizi pale karemjee hall juzi kati na si vijana makini.................:rip:CCM>
 
Hapo umsesma Kiloni, Makamba yawezekana ni hopeless lakini usisahau wameshughulikia mapaka sasa the 'official leadership' lakini siyo yenye shida, yenye shida ni defactor leadership - hiyo haijaguswa na huenda haitaguswa. Mara nyingi CCM wameshakaribia sana kuigusa ile 'point of pain' lakini ghafla kigugumizi huwapata na wakaamua kuingia mitini kila mtu na lwake.

Hapo kwenye red mkuu umemaliza yooote...hii inayoendelea ni sinema tu kama ile ya mmiliki wa Dowans!!!watakapo gusa hapo kwenye red kila mwenye akili timamu atatambua na si kabla ya hapo.
 
Agree, lakini ataweza kuongoza majeruhi wengi namna hiyo? na How strong he is to handle kundi la RA au EL plus Makamba?

hili ndio gamba gumu kuliondoa,halihitaji mwamba bali linataka kisu kikali cha kuliondoa,bila kuliondoa gamba hili sina uhakika kama ccm itarudisha mvuto!

Na kwa kumweka Zakia Meghji kama mtuza hazina wao; hawajajivua hilo gamba. Ni Zakia aliyekuwa Waziri wa fedha wakati mambo ya EPA yanafumuka na akatetea sana mpka yalipomfika shingoni. Sioni kilichofanyika zaidi ya kuwa ni mafisadi walewale wengine wanawekwa benchi na wengine wanaingizwa mchezoni.
 
Back
Top Bottom