Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Hivi watu wa vijijini ambako Ccm ina wanachama wengi wanajua kuwa chama chao kina mipasuko na hakina dira ya kumkomboa Mtanzania? Ni jukumu letu sisi kuwahamasisha watu wa vijijini na kuwaonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo Ccm si mkombozi wao wa kweli.
Saa ya ukombozi ni sasa.

Ukweli Makamba ameigharimu sana CCM na Uraisi wa Mh. JK. Mwaka jana alichukua hela za wagombea sana na kubadilisha matokeo na alimtumia mtoto wake mmojawapo pale kwenye makazi yake Morogoro.

Pia amechukua sana hela za watu aliowaahidi kuwa watapatiwa vyeo vya UKUU WA WILAYA na wengi wao ni wale waliogombea Ubunge wakakosa mwaka jana. Ukweli Makamba ni mtu wa vibahasha na Usalama wa Taifa walishapeleka taarifa nyingi naona busara za JK alikuwa anaamini atajirekebisha. Assishie hapo ajitahidi kufanya uteuzi wa watu wanaoeleweka sasa na Usalama umsaidie maana wanaweza mpindua kama Zuma alivyofanya Afrika ya Kusini. Awatumie vijana kama zamani, vijana wenye maono si type ya lumbilumbi kama akina Shigela na Malisa. Shigela alikuwa kijana mzuri sana lkn alipokubali kutumikia kundi la mafisadi amebadilika sana na mi kwa ushauri wangu hata yeye pale ang,olewe. Watu wanawataja lukuvi, Nchimbi na Wasira nakwambieni hawa hawafai bado ni watu wa makundi na Nchimbi ana ndoto pia za uraisi na Lukuvi anajiona nafasi ya Ukatibu Mkuu haimfai atafutwe mtu mwelewa msikivu na ambaye anaweza shuka chini kuona matatizo ya wananchi. Kuna balozi mmoja amepata kuwa mkuu wa mkoa jina limenitoka angefaa huyo nikipata jina nitawapatieni. tuwe na siasa za kiushindani na zenye muelekeo wa kuthamni zaidi maslahi ya taifa.
unamaanisha jack mwambi? ccm ni zaidi ya uijuavyo kwani makamba alikuwa na sifa gani hadi akawekwa pale? hata wakikmuweka riz1 sitashaNGAA
 
Heshima yako kaka Maggid

Mkuu...ccm haibadiliki na haitokuja kubadilika. Yanayoendelea huko Dodoma ni usanii mtupu...kwa ufupi hawa jamaa washapoteza mvuto kwenye akili na macho ya watanzania. Kumn'goa Makamba,Chenge na Rostam hakuisaidii ccm ng'o....soon hawa ccm watatokomea mfano wa KANU ya kenya. Keep watching wakuu....
 
Ahsante EMT.
Kwa mantiki ni kuwa sekretariati imevunjwa wakati CC ikiandaa agenda za kikao cha NEC kwa taratibu za CCM.
CC wanaingia wajumbe wa kuchaguliwa na wale wanaoingia kwa heshima zao kama marais wastaafu.
NEC wanaingia wajumbe wa kuchaguliwa na wale wa heshima kama mawaziri wakuu wastaafu.

Kikao cha NEC cha Butima kiligubikwa mjadala mkali sana wa ufisadi. Kabla ya kikao, wenyeviti wa CCM wa mikoa chini ya mwenyeji wa mkutano Makongoro Nyerere waliazimia wale wanaokichafua chama wafukuzwe. Hoja yao iliungwa mkono na wazee wastaafu wakiwamo mawaziri wakuu na wanafunzi wa kweli wa Mwalimu Nyerere. Hoja ilizimwa kibabe na mwenyekiti ili kuokoa wanamtandao waliomsaidia kufika hapo.

Uchaguzi uliopita pamoja na viongozi kuficha ukweli kwa maneno ya kejeli umewatisha sana CCM. Kuingiliwa ngome za Dar, Mbeya na Mwanza haikuwa dalili nzuri. Hii imelazimisha baadhi yao wakubali ukweli kuwa ufisadi na kashfa kama za Richmond na Dowans vimechangia sana, na kibaya zaidi wahusika ni viongozi ndani ya chama na kuharibu taswira nzima ya chama.
Wajumbe wengi wa NEC wamedhamiria kukinusuru chama wakiungwa mkono kichini chini na wastaafu maarufu. Nguvu ya kundi la mafisadi ndani ya NEC imepungua.

Uwezekano wa NEC kujadili hoja za kushindwa kwa chama unaweza kuleta mpasuko na uwezekano wa watuhumiwa kupoteza nyadhifa zao kichama au kufukuzwa. Ili kupunguza jazba,mwenyekiti amevunja sekretariati inayolaumiwa kwa utendaji mbovu kama njia ya kuua agenda hiyo kwa vile suala limeshughulikiwa (pre-emptive strategy). Hii itawaokoa watuhumiwa kutojadiliwa mbele ya NEC kwa kina kuzuia jaribio kama la Butiama kuweza kujirudia kwa nguvu zaidi.

Kuwafukuza uanachama kundi lenye nguvu kifedha ni jambo lisilowezekana ikizingatiwa kuwa limeshajipanga vema ndani ya CC, NEC na bunge. Jambo linalofanyika hapa ni 'funika kombe mwanaharamu apite'. Ni mbinu ya hali ya juu sana kuwanusuru watuhumiwa kwa kupunguza nguvu za hoja iliyoko mbele kwa majibu kuwa chama kipo mbioni kujiunda upya na kipewe nafasi.
Mabadiliko hayatalenga kujivua gamba bali kufunika kombe. Hii itakuwa sawa na kunywa 'asprin' homa ipungue bila kutibu tatizo.
Kwa maoni yangu kama hatua kali hazitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa au kufukuzwa, hakutakuwa na mabadiliko yoyote na itakuwa ni njia rahisi ya kukipeleka chama kule UNIP na KANU zilipopunzika.

You have said it all Nguruvi nimekugongea na thanks hapo, kimsingi wanachokifanya CCM, au tuseme huu ujanja walioutumia CC nia yake sio kuwaondoa au kuwapunguzia nguvu hawa jamaa wanaodai wamejiuzulu but rather kuwaokoa na panga kubwa zaidi "Heri nusu shari kuliko full shari" na sitshangaa ama huu uamuzi umefikiwa kwa kitu wanaita COMPROMISE, meaning hawa watuhumiwa wamekubali kujiuzulu huku wakijua,au pengine wakipewa na njia kabisa ya kujinasua out of that mess! So naweza guess kuwa mbio za Lowassa towards 2015 ndo kwanza zimeanza na tusitegemee kuona retaliation yoyote kutoka kwenye hilo kundi lake kwasababu sasa ndo watakua wamejiunga kabisa kuwa kitu kimoja! All CC members for Lowassa and co.

Hivi kajadiliano ya CC ni TOP SECRET?? Ingekua njema sana kama tungeona walichokiongea humo! Haswa njia walizotumia" kuwashawishi" hawa watu kujiuzulu kwasababu am sure hapo ndo tumeuzwa mazima
 
Duh! hii thread moto kwelikweli, hadi vumbi litulie tutakuwa tumesahau y BABU na Mswada wa katiba!

There are currently 372 users browsing this thread. (91 members and 281 guests)
 
hakuna lolote nyoka anabaki yule yule na gamba litaota tena ........halafu msiseme jk amefanya maamuz mazito....huyu nae alipaswa kutumia kikao hiki kuwaaga wanachama na kuachai ngazi............eti chama kinajivua gamba lipi hilo?
 
Wanachokifanya ni kuchagua baadhi ya mayai viza yasiyonuka zaidi.

HAYA MAMBO HAWANA
avatar24815_79.gif

WANA
images
 
Hata wakiweka vijana,cc haituhusu 2nachotaka ni mabadiliko ya dhati na kweli,na wale walioiba wapelekwa mahakaman na c kutolewa huko kwenye kamati kuu 2.
 
Umewataja nchimbi na lukuvi. Hawa kaka ni mawaziri. Wasimamia sera na ilani yao iliyowaweka madarakani. Wasipofanya hivyo kwa umahili mkubwa chama kiwabane. Sasa kwa nafasi ya ukatibu mkuu watabanwa vipi. Hili pia ni kosa linalokitafuna chama. Mawaziri hao hao,nec hao hao, cc hao hao!

Kama Nchimbi naye anaonekana kufaa kushika nafasi hiyo basi chama kimewashinda, kwa uwezo gani? au huo u dokta wa kujipachika! akipewa yeye utakuwa ni msimu mzuri kwa wapinzani maana jamaa atakivuruga kuliko makamba. Huyo yumo ndani ya makundi tayari and too ambitious. Lukuvi!... shule je intosha kwa mazingira ya sasa?
 
Ndugu Zangu,

TAARIFA zimetufikia, kuwa Mwenyekitiki wa CCM, Jakaya Kikwete amevunja CC na Sekretariati nzima ya CCM.

Tafsiri yangu; haya ni mabadiliko makubwa ndani ya CCM tangu kuundwa kwake mwaka 1977. Mabadiliko makubwa ya kichama yalifanyika mwaka huo wa 1977, wiki mbili tu baada ya CCM kuundwa.

Kuvunjwa kwa CC na Sekretariati kuna tafsiri kadhaa za haraka. Angalia hapa, ina maana; CCM imeondokana na Rostam na Chenge kwenye CC. Wawili hao hawarudi tena kwenye CC mpya itakayoundwa. Ndio, CCM wana namna zao za ’ kufukuzana’ wanapoacha ' kulindana'.

Na hiki ndio kile tulichoambiwa; Chama Kujivua Gamba, au labda magamba. Na kuna changamoto kwa Mwenyekiti wa Chama hicho- Unafanyaje na magamba yaliyovuliwa? Unayafukia, au unayaacha yakitapakaa? Na Magamba mengine hayaozi!

Ndio, Uchaguzi uliopita ulikuwa na ujumbe mmoja mkubwa kwa CCM kutoka kwa wapiga kura. Ni huu; MABADILIKO. Ndio, Watanzania wanataka mabadiliko. Kilichotokea Dodoma jana usiku ni jaribio la CCM kujibu matakwa ya wananchi. Je, wamefaulu? Tuna sababu ya kusubiri huku tukipima upepo unavyovuma.

Kuna maswali pia ambayo hatujapata majibu yake. Moja ni hili; Je, Mabadiliko haya ndani ya CCM yana ukubwa na athari gani kwa wakati huu na ujao?

Yepi zaidi yanakuja?
Tegemea - Kuwa asubuhi hii JK atakuwa ’busy’ akishauriana na ’ wazee’ akina Msekwa, Mwinyi, Malecela, Mkapa na hata Spika Makinda. Wamsaidie mawazo katika kupendekeza majina kama 26 hivi yatakayopelekwa kwenye NEC ili yapigiwe kura na kupatikana wajumbe 18 wa CC.

Tegemea- Kuwa mengi ya majina hayo yakayopendekezwa yatatokana na wajumbe vijana wa NEC.

Nani atakuwa Katibu Mkuu?
Tegemea - Kuwa Katibu Mkuu atakuwa ama kijana au ana sura ya kijana. Jina kama Emmanuel Nchimbi si la kulibeza, William Lukuvi si ana sura ya kijana?

Kwa yanayotokea Dodoma CCM itakuwa imemaliza kazi ya ’ kujibua’ au kujivua gamba?

HAPANA. Kazi hiyo lazima iendelee. Kwa vile Sekretariati itaundwa upya, basi, kutakuwa na sura nyingi mpya. Tegemea, kuona vijana wengi zaidi wakipewa nafasi kwenye Sekretariati. Makatibu Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya watapanguliwa. Na vijana wenye fikra za ’ kizamani’ nao watapotea, na hapa, Tambwe Hizza laweza kuwa ni jina la ’ vijiweni’ kule Temeke Mikoroshini. Na kuna wengi ndani ya CCM wanaofanana na Tambwe Hizza.

Na upi ni mtihani mgumu kwa JK kwa sasa?
KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA….. ! Ndio, Watanzania wengi wa sasa na hususan vijana wanataka MABADILIKO, na Katiba kwao ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo. Watanzania wameshaamka na kubaini, kuwa KATIBA yao ya sasa nayo ni ’ Maghumashi’. Neno hilo la mitaani lina maana ya mambo ya kiini macho na ubabaishaji.

Kwa vile JK ameshawajengea matumani ya kuwasaidia kupata Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya wakati uliopo na ujao, basi, nao wanataka iwe hivyo. Na kama JK atataka abaki akikumbukwa hata na vizazi vijavyo, basi, awe na ujasiri wa kuwasaidia Watanzania kupata KATIBA MPYA itakayolifanya taifa hili liwe la kisasa na lifanye mambo yake ikiwamo chaguzi katika mazingira ya kistaraabu. JK ana lazima ya kuacha kuiangalia kwanza CCM na bendera yake, badala yake aingalie kwanza Tanzania na bendera yake. Maslahi ya Nchi Kwanza. Maana, tunakokwenda, hata ndugu wa JK wanaweza wasiipigie kura CCM.

Na walioandaa Muswaada wa Sheria ya Kuanzisha Mchakato wa Katiba kimsingi wamechangia kumpunguzia JK heshima yake. Muswaada ule ni wa kiwango cha chini sana. Na JK akikubali kuasisi mchakato wa Katiba kwa kufuata ’ ramani’ ile tulioletewa juzi na kuambiwa tuitolee maoni, basi, nahofia, kuwa kuna watakaosema mitaani; ” Na JK naye ni Maghumashi!”

Maggid
Iringa,
Jumapili, Aprili 10, 2011
0788 111 765

Wee kibaraka wa mafisadi wacha kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa hapa... yaani huu usanii unaofanywa wa cc kujiuzu ndio maamuzi magumu....
Kwa taarifa yako watu tumeshapata siri zote zilizojificha nyuma ya huu usanii...
 
Mi sio mdau sana wa politics ila ni observer mzuri wa mambo yanavyokwenda:

Hapa kuna mambo mawili (2): (i) ushindi kiduchu wa JK umesababishwa na secretariet/cc ya CCM au (ii) Utendaji mbovu usioleta matumaini wa Serekali from 2005 - 2010 na from 2010 up to now?

Ki ukweli uchaguzi ulifanyika mambo mengi yakiwa hayako sawa kiutendaji! (1) Uchumi ulidorora (2) Mfumuko wa bei (3) Tatizo la nishati ya umeme (mpaka sasa lipo lisha ya mapesa kutolewa) (4) Ukosefu wa Ajira kwa vijana .............................

Mtazamo wangu ni kwamba huwezi kuwa hauja perform kwa kiasi kile alafu wananchi wakupe kura tu hivihivi. Sasa issue hapa sio Makamba au CC ila utendaji wa kiwango cha chini serikalini pengine ndo ulisababisha kura kuwa kiduchu.

Badala ya kupangua secretariet ingeanza kupanguliwa watendaji serikalini kwanza!!!
 
Tunaweza kwenda mbali zaidi na kujiuliza iwapo tatizo la CCM kama chama linaishia kwa Lowassa,Rostam na Chenge pekee.Tunapaswa pia kujiuliza imekuwaje wanasiasa hao watatu wameibuka kuwa na nguvu ya kutisha ndani ya chama hicho na kwenye serikali kwa ujumla (hata kama si watendaji wa kiserikali).Na katika hili la pili,ni muhimu pia kujiuliza iwapo "kuwavua" madaraka wanasiasa hao kutamaliza kabisa nguvu,ushawishi,uwezo na malengo yao ya baadaye.

Tunaweza kutumia muda mwingi na nguvu kubwa kujadili MATUKIO.Hilo si tatizo except mjadala wa matukio utakaposhindwa kuhusisha masuala (issues) zilizopelekea kutokea kwa tukio husika na faida/athari zake kwa jamii.Je tunaweza kujiuliza,kwa mfano,kuondoka kwa Lowassa,Rostam na Chenge kwenye Kamati Kuu kunamaanisha mwisho wa mfumo wa kifisadi ndani ya CCM?

Na je kama kuwawajibisha kichama kunaishia kuwavua madaraka tu,which in itself speaks volumes kuhusu uadilifu wao in the first place,pasipo kuvishirikisha vyombo vya dola kushughulikia "makosa" yaliyopelekea "waonekane mzigo ndani ya chama" hakuwezi kupelekea wanasiasa hao kupotea katika rada za Watanzania huku wakijijenga kwa nguvu kubwa "kizani"?

Wote-Lowassa,Rostam na Chenge- wanaendelea kuwa wabunge wa CCM.Kwa Lowassa,anaendelea kuwa mwenyekiti wa kamati influential na powerful ya Ulinzi na Usalama (inayompa access ya kuwa karibu na mashushushu wetu-key players kwenye manoeuvres za siasa za Tanzania)Je katika mazingira ya kawaida tu,watatu hao watashindwaje kuendelea na ajenda zao za kifisadi hata kama wamevuliwa vyeo ceremonial ndani ya CCM?

Kuhusu Katiba,mwanzo na mwelekeo si mzuri.Ni muhimu kutambua kuwa shinikizo la mabadiliko ya katiba limetoka nje ya CCM,na kwa namna flani linaweza kutumika kama turufu ya kuonyesha kuwa chama hicho kinasikia vilio vya Watanzania.Hiyo to-down model of constitutional reform itaturejesha hapa hapa tulipo.Katiba si kwa manufaa ya watawala pekee.Ni suala linalomhusu kila Mtanzania.Ni mzaha kwa mjadala huo muhimu kupewa muda mfupi na unaowashirikisha watu wachache tu.Kibaya zaidi,suala hilo limeachwa kuwa linalotegemea matakwa ya Rais.Let's be honest.Kikwete anajua kuwa anamaliza muda wake madarakani takriban miaka minne kutoka sasa.Kumwachia afanye atakavyo katika zoezi zima la mabadiliko ya Katiba-ilhali tunajua hana muda mrefu madarakani,na anahitaji kinga kwa "madudu" yote aliyofanya katika utawala wake ni hatari.

Jambo zuri lakini lenye matokeo fyongo ni sawa kabisa na jambo baya
 
mAKAMBA KESHA JIUZURU AU BADO?

Kikwete amemtimua Makamba. Kwa kuitufa Sekretariat ya chama, JK amemfukuza kazi Makamba kwani Makamba kama Katibu Mkuu wa CCM ndiyo mwenyekiti wa Sekretariat ya chama. Kwa maana hiyo kikao cha NEC kitapitisha majina ya wanachama wapya wa Kamati Kuu pamoja na Katibu Mkuu mpya na Seretariat yake.

Alichofanya JK kwa kuwatosa Kamati Kuu na Secretariat alikuwa analenga kuwaondoa kina Makamba, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye nafasi za uongozi CCM.

Bado Edward Lowassa sasa. Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, yeye anakuwa mwanachama wa Kamati Kuu na NEC kwa nafasi yake kama Waziri Mkuu wa zamani. Issue hapa kuwa Lowassa si PM mstaafu, ni PM aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, hivyo dawa ni kumuondoa na yeye Kamati Kuu na NEC.
 
CCM hawawezi kumaliza kwa kuwashughulikia wakina chenge, bado kuna mkapa na kiwira, bado kuna wakina meghji na kagoda, mambo bado kabisa dawa ni kukipeleka hiki chama kinakostahili
 
- Wakulu tupo pamoja sana, hali sio shwari Dodoma the dataz ni makundi ndani ya CCM yakirushiana mawe, lakini kundi lenye nguvu ya kushika Urais 2015 ndilo linaloelekea kushinda.

- Mafisadi time is up, wameshikwa pabaya sasa maana hawana pa kupitia tena Six holds the big key to the changes which are coming ndani ya CCM kutoka hiki kikao!

......Stay Tuned.....!


FMes! - Wazee Wa Sauti Ya Umeme!

Wow.............At last umetokea mkuu......Lete dataz kamanda wangu.......Ni furaha iliyoje kukuona kipindi hiki ambacho unahitajika jukwaani kwa udi na uvumba..............:smile-big::smile-big::smile-big:
 
Mi sio mdau sana wa politics ila ni observer mzuri wa mambo yanavyokwenda:

Hapa kuna mambo mawili (2): (i) ushindi kiduchu wa JK umesababishwa na secretariet/cc ya CCM au (ii) Utendaji mbovu usioleta matumaini wa Serekali from 2005 - 2010 na from 2010 up to now?

Ki ukweli uchaguzi ulifanyika mambo mengi yakiwa hayako sawa kiutendaji! (1) Uchumi ulidorora (2) Mfumuko wa bei (3) Tatizo la nishati ya umeme (mpaka sasa lipo lisha ya mapesa kutolewa) (4) Ukosefu wa Ajira kwa vijana .............................

Mtazamo wangu ni kwamba huwezi kuwa hauja perform kwa kiasi kile alafu wananchi wakupe kura tu hivihivi. Sasa issue hapa sio Makamba au CC ila utendaji wa kiwango cha chini serikalini pengine ndo ulisababisha kura kuwa kiduchu.

Badala ya kupangua secretariet ingeanza kupanguliwa watendaji serikalini kwanza!!!

JK, anapaswa kuachana na wazee wenye mawazo ya kikoministi. Inabidi safu hiyo aweke vijana wenye umri wa miaka 30-39.
 
Back
Top Bottom