Njaa ni swala la kujitakia! Kama serikali inavyoshindwa kutekeleza mipango ya maendeleo na leo hii bado tupo ktk umaskini ndivyo wananchi wanavyoshindwa kutekeleza vipaji vyao na njaa imekuwa matokeo ya mfumo huu wa maisha ya kuiga..Umaskini na njaa ni vitu vya kujitakia!
Tanzania hatukuwahi kufa njaa ktk Ujamaa wa Nyerere pamoja na adha zote za ukosefu wa mali za viwandani kama sukari, sabuni na kadhalika ambavyo takwimu zinaonyesha wazi kuwa viwanda vyetu havikuzalisha kulingana na kiwango chake na hata ile mali chache ilopatikana iliporwa na kuuzwa na walanguzi nchi za jirani. Hata kilimo cha cash crops kilishuka baada ya mashamba kushindwa kusimamiwa vizuri na wataalam wetu. Ujamaa wa Nyerere ulishindwa kwa mchango mkubwa wa UVIVU wa watanzania wenyewe (viongozi na wananchi).
Kwa hiyo, baada ya kuingia Ubepari Watanzania kwa uvivu wetu tumekimbia kabisa kilimo na kusema kweli Kilimo Kwanza kimechukua mkondo wa kilimo cha kukodisha, ardhi ikiuzwa kwa wageni wakati wananchi wakikimbia vijijini kwenda mijini kujishughulisha na biashara za Umachinga (uchuuzi wa finished product). Kifupi watanzania tumeshindwa kujituma wenyewe ktk uzalishaji na leo hii tunazungumzia KILIMO KWANZA kwa uchungu ni kwa sababu tu tunaona ardhi yetu ikipewa wageni lakini sisi wenyewe hatuwezi kurudi ktk kilimo.
Kama navyosema siku zote kabla hujafikiria mkakati wowote ni muhimu sana kutazama WATU na MAZINGIRA. Watanzania ktk mazingira haya ya utandawazi wametupa zana zao, wametupa vipaji vyao na kwa asili ni wavivu wa uzalishaji tumejikita zaidi ktk biashara rahisi za umachinga. NI vigumu sana kuondoa njaa nchini ikiwa sisi wenyewe tunataka tukabidhiwe ardhi ambayo hatuna mawazo ya kulima bali kuihodhi kibiashara na pengine sisi wenyewe ndio tutaiuza kwa wageni badala ya kulima.
Mwisho nasema kwamba viongozi wetu ni reflection yetu, wao hawana akili na wavivu kama sisi kiasi kwamba ktk uvivu wao swala la Uzalishaji ni la wageni na wananchi watajikita ktk biashara rahisi za umachinga. Kwa mtaji huu hatutaweza kuondoka ktk umaskini wala kuondokana na njaa! Isipokuwa siku wananchi wenyewe wakiweza kusoma alama za wakati wakaondoa uvivu wa akili na kimwili warudi vijijini na kuanza KULIMA mashamba kwani hiki ndicho kipaji kikubwa cha Mbatu Mtanzania na pekee ndicho kitamwondoa ktk umaskini..