Mambo 11 ya kuzingatia ili kuepuka vifo vya ghafla!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
pamoja na vifo vinavyochangiwa na stress na mazingira magumu tunayoishi vimezidi kuongezeka.

Tafadhali epuka;
i. Kukasirishwa kirahisi na mwenzi, watoto, marafiki, wafanyakazi wenzako, majirani, wasaidizi wa majumbani n.k.

ii. Epuka kujibu kwa ukali au kufoka mara kwa mara, jaribu kupunguza tabia ya ukali. Tafuta utulivu ndani ya moyo wako.

iii. Jitenge na usumbufu usiokuwa wa lazima kama vile kuishi na wategemezi wakorofi au wasumbufu nyumbani kwako.

iv. Epuka kuwaza kupita kiasi. Hata kama huna pesa au chakula ndani ya nyumba, bado maisha yanakuhitaji.

v. Tafuta njia sahihi ya kuongeza kipato. Hakikisha kila mtu mzima unayeishi naye nyumbani kwako anajishughulisha.

vi. Usikope kwaajili ya kusaidia watu walio karibu nawe, wema usizidi uwezo. Acha wakope wenyewe kwani hawatajua ulikopitia.

vii. Tengeneza mtandao wa marafiki sahihi, wanaoishi kwa malengo ya kumpendeza Mungu.

viii. Miliki furaha ya moyo wako kwani una kila sababu ya kuishi kwa furaha, bila kujali kipato ulichonacho.

ix. Afya yako ina thamani kuliko chochote ulichonacho. Zingatia lishe bora, fanya mazoezi, pima afya yako mara kwa mara bila kusahau umuhimu wa Bima ya Afya.

x. Muhimu zaidi: imarisha imani yako kwa Mungu wako, kwani Yeye ndiye sababu ya wewe kuishi duniani.

xi Jitahidi kutafuta jambo lolote la kukufanya ucheke/ utabasmu ( Hata kama unaumwa, una madeni. Bado maisha yanaendelea

Mwenyezi Mungu Atusaidie."



Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom