Mamba au Kenge, yoote ni sawa Uchina

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
293735_471124002915115_772359462_n.jpg
 
duh, eeeh wachina hakuna ki2 wanaacha, neno msamiat haram haupo kwa wenzetu hawa. Nyama ni nyama
 
duh, eeeh wachina hakuna ki2 wanaacha, neno msamiat haram haupo kwa wenzetu hawa. Nyama ni nyama

ulisha anza udini hapa. haramu hata hivyo haijawhi kuwepo kwa wanadamu wote, ni kwa baadhi ya watu tu. maisha ya walahi usihamishe kwa wengine, wabenjamini na waebrania. Mungu alikuwa na malengo yake tu kwa kundi dogo la watu.

soma hapa kama una uelewa.

Mungu Aweka Agano na Noa (MWANZO 9:1-5)

Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, '‘Zaeni mkaongezeke kwa
idadi na mkaijaze tenaa dunia. 2Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 3Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.
4"Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 5Hakika damu ya uhai wenu nitadai. Nitadai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitadai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.
 
Sasa kinge si sehemu ya zawadi nzuri ya mungu kwa wanadamu? Nguruwe sungura na wengine si halali ya mwanadamu?
 
Ndiyo maana hawa jamaa wana miili mizuri hawa nenepi ovyo na wanaishi miaka mingi.
 
Really misosi ya hawa jamaa inanipa presha, kuliko niende nyumbani kwa Mchina anikaribishe supu ya chura, bora niondoke na njaa yangu
 
Nilisikia Wachina hawako na imani kama hizi za kwetu, ukristo, uislamu, afadhali hata India kuna mchanganyiko wa imani, mpaka na hiyo ya kuabudu ng'ombe, sijajua Wachina wanamuabudu nani hasa
ulisha anza udini hapa. haramu hata hivyo haijawhi kuwepo kwa wanadamu wote, ni kwa baadhi ya watu tu. maisha ya walahi usihamishe kwa wengine, wabenjamini na waebrania. Mungu alikuwa na malengo yake tu kwa kundi dogo la watu.

soma hapa kama una uelewa.

Mungu Aweka Agano na Noa (MWANZO 9:1-5)

Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, ‘‘Zaeni mkaongezeke kwa
idadi na mkaijaze tenaa dunia. 2Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 3Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.
4“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 5Hakika damu ya uhai wenu nitadai. Nitadai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitadai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.
 
Wengi tumekuwa tukidharau sana utamaduni na mafanikio mengineyo walitopata wachina; nafikiri wakati umefika na kubadili mtazamo na kuanza kujifunza kutoka kwao. Hawa jamaa maisha yao katika swala la chakula hayasumbui maana wanaelewa kwamba vitu vyote Mungu aliweka kwa ajili ya matumiza ya mwanadamu, sasa sisi tunajua kula KUku, ng'ombe na mbuzi tu; ambapo tunajikuta tunaongeza gharama ya maisha kwani uzalishaji wa wanyama ambao tunakula unakuwa mdogo. Niliwahi kuzungumza na jamaa hawa wakaniambia nyoka ni chakula sana kwa mwanaume kwani inaongeza nguvu za kiume. Tunahitaji kubadili mtazamo na kula vyakula kwa ajili ya kuboresha afya zetu, wa-china kuna magonjwa ukiugua wanaita magonjwa ya kigeni na wanakuambia nenda katafute dawa za kigeni (yaani hizi kemikali tunazotumia sisi) maana wao wanaamini sana katika vyakula kwamba ndio tiba ya mwili.
 
Nilisikia Wachina hawako na imani kama hizi za kwetu, ukristo, uislamu, afadhali hata India kuna mchanganyiko wa imani, mpaka na hiyo ya kuabudu ng'ombe, sijajua Wachina wanamuabudu nani hasa

asilimia kubwa ni wabudha, lakini wakati wa MAO, dini zote zilipigwa marufuku, na aya za MAO, zikisisitiza ujamaa ndo ilikuwa dini yao kubwa. Na mao aliwambia wanyama wpte wale, isipokuwa ndege wa angani. ni wachina wachache wanakula ndege wa angani, anayeruka tofauti na hawa wa kufugwa.
 
Back
Top Bottom