Mama wa bibi harusi aona aibu: kwenye harusi wa binti yake. Aona aibu mbele ya wageni

Johnson12345

JF-Expert Member
May 29, 2023
206
422
Habari wiki iliyopita nilikuwa kwenye harusi moja hivi nilialikwa. Sasa nda wa ukumbini na maharusi kuingia. Sasa katika utambulisho binti aliwatambulisha wazazi wake wa kumzaa na BABA mlezi.

Iki hivi binti anawazazi wake kwenye kabisa wa kumzaa ila hawakuweza kuishi pamoja Baba alioa kwingine na mama akaolewa kwingine. Mtoto akakaa na mama yake kwa hio akalelewa na stepfather( Baba wa kufikia).

Sasa katika utabulisho nilishangaa sana reaction ya yule mama kwani alikuwa ni mtu kama muoga hivi.
Maana bibi harusi alimtambulisha baba mzazi, baba mlezi, na mama mzazi.

Ila mama hata kusimama alikuwa anona aibu falani. Hata mwishoni kwenda mbele alikuwa anaona aibu watu wengi tulishuka ila mwa upande wangu ni ile ishu ya wanaume wawili, naamini alikuwa anaona aibu mbele za watu inaonekana katembea na wanaume wawili.

Nilishangaa tuu , mimi niliona mbona wapo wengi kama hawa tuu. Ila pia nafikili pia watu labda wanavyomchukulia yule mama.

Kwa kweli katika vipengele kusimamishwa wazazi wote watatu alikuwa hata kusimama anajiumauma yule mama, mpaka watu baadhi wakawa wanacheka sana.

Alikuwa anaona aibu sana.

NB. JAMANI TUJIFUNZE KUZAA NA MTU MMOJA TUU SI KUCHANGANYA WATOTO BABA AU MAMA. NI AIBU SANA.
HASA UKIWA MTU MZIMA.
 
Inaonesha hiyo harusi hukuchanga ulidandia tu kadi ya dezo, badala ya kufata kilichokupeleka unafata umbea wa kuandika mtandaoni, aone aibu kwa lipi na ushasema aliachana na huyo baba ulitaka akae peke yake kama sanamu?
 
NB. JAMANI TUJIFUNZE KUZAA NA MTU MMOJA TUU SI KUCHANGANYA WATOTO BABA AU MAMA. NI AIBU SANA.
HASA UKIWA MTU MZIMA.
Hapo mtoto anasema huyu ni baba yangu mzazi na huyu ni baba mlezi na huyu ni mke wao ambae ni mama yangu yaan baba mlezi anakula na baba mzazi akijisikia pia anakula, kuna baadhi ya tamaduni hilo sio Jambo la ajabu ni Jambo la kawaida mwanamke kua na waume zaidi ya mmoja kwa hio Mimi sishangai
 
Inaonesha hiyo harusi hukuchanga ulidandia tu kadi ya dezo, badala ya kufata kilichokupeleka unafata umbea wa kuandika mtandaoni, aone aibu kwa lipi na ushasema aliachana na huyo baba ulitaka akae peke yake kama sanamu?
Analiwa na wanaume wote wawili hakuna kuachana hapo uwe unaelewa kidogo,
 
Sijapendezwa maneno yako ya kashfa na matusi...
Sijapendezwa kabisa tujifunze kua na stara...

Ukichukia uwe na sababu
Kasfa na dharau humu si ndo wanapenda, ndo ujanja, kumbe unaweza kutumia kauli nzuri na kuchangia tu, kauli nyingi pimbi, kilaza, kila mtu matawi au yupo vizuri.
 
Back
Top Bottom