Mama salma kikwete alaani mauaji ya raia wa china

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
[h=1]MAMA SALMA KIKWETE ALAANI MAUAJI YA RAIA WA CHINA[/h]
WEDNESDAY, 01 SEPTEMBER 2010 14:55 ADMINISTRATOR

mchina.jpg

Mke wa rais mama Salma Kikwete, amelaani vikali mauaji ya mfanyabiashara wa kigeni raia kutoka China bi Hang Bing aliyeuawa hivi karibuni jijini Dar es Salaam baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa wajambazi.
Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 11 eneo la Kurasini ambapo majambazi hao inasadikiwa walitoweka na kiasi kikubwa cha fedha.
Akizungumza waakti wa kuaga mwili wa marehemu Hang Bing Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe, Mama Salma Kikwete wameelezea kusikitishwa na tukio hilo ambapo wamemtaja mwanamke huyo kuwa alikuwa mwanaharakati wa maendeleo ya wanawake wa Tanzania kutokana na mchango wake wa hali na mali kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na jeshi la polisi.
11-+MAMA+SALMA+AKIMPA+POLE+BW%252CBING.JPG

Nae balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng pamoja na jumuiya ya wachina wanaoishi nchini ,wameomba waliohusika na mauaji hayo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova,amesema jeshi la polisi litafanya kila liwezezalo kuhakikisha waliofanya mauaji hayo wakamatwa. Aidha ametangaza zawadi ya shilingi milioni 5 kwa yeyote atakeyetoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa.
-----------------------------------
 
Na wale waliouawa na askari Arusha mbona hatukuwasikia wakilaani? Vipi waliowafukia Shinyanga? Mbona hatukuwasikia?

Inaelekea kwa huyu Mama uhai wa Watanzania hauna maana yoyote ukilinganisha na wa Mchina, vinginevyo angepaswa pia kulaani mauaji ya Tarime, Shinyanga na Arusha
 
Full kujipendekeza ila ndo miafrika tulivyo. Sijui ni lini tutajitambua na kujithamini, huyu mama hajasema lolote kuhusu mauaji ya watu Igunga!
 
Watanzania tutaendelea kuwa mazezeta hadi lini? Akiuawa Mchina mgeni serikali inafanya kila jitihada ili wahalifu wapatikane lakini wakati huo maauaji kama hayo yakifanywa na wageni kwa Watanzania wenzetu serikali huwa kimya. Ni nini tafsiri ya vitendo hivi vya serikali?
 
MAMA SALMA KIKWETE ALAANI MAUAJI YA RAIA WA CHINA

WEDNESDAY, 01 SEPTEMBER 2010 14:55 ADMINISTRATOR

mchina.jpg

Mke wa rais mama Salma Kikwete, amelaani vikali mauaji ya mfanyabiashara wa kigeni raia kutoka China bi Hang Bing aliyeuawa hivi karibuni jijini Dar es Salaam baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa wajambazi.
Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 11 eneo la Kurasini ambapo majambazi hao inasadikiwa walitoweka na kiasi kikubwa cha fedha.
Akizungumza waakti wa kuaga mwili wa marehemu Hang Bing Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe, Mama Salma Kikwete wameelezea kusikitishwa na tukio hilo ambapo wamemtaja mwanamke huyo kuwa alikuwa mwanaharakati wa maendeleo ya wanawake wa Tanzania kutokana na mchango wake wa hali na mali kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na jeshi la polisi.
11-+MAMA+SALMA+AKIMPA+POLE+BW%2CBING.JPG

Nae balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng pamoja na jumuiya ya wachina wanaoishi nchini ,wameomba waliohusika na mauaji hayo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova,amesema jeshi la polisi litafanya kila liwezezalo kuhakikisha waliofanya mauaji hayo wakamatwa. Aidha ametangaza zawadi ya shilingi milioni 5 kwa yeyote atakeyetoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa.
-----------------------------------

Du, Mama Salma ameongezeka unene kwelili kweli. Anapataga muda wa kuwawazia hao wanawake wenzake kweli?
 
Back
Top Bottom