Mama na Baba Wazozana, Mtoto Wao Aruhusiwe Kufariki au La

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
</SPAN>




Tuesday, November 03, 2009 9:21 AM
Mahakama nchini Uingereza ina wakati mgumu kuamua kama mtoto wa kiume ambaye anapumua kwa kutumia mashine lakini ana uwezo wa kusikia na kuona aruhusiwe kufariki au aendelee kuishi hivyo hivyo kwa kutegemea mashine.


Mama na baba wa mtoto mmoja nchini Uingereza wamefikishana mahakamani kufuatia mzozo wa haki ya kuishi ya mtoto wao wa kiume.

Mtoto wao aliyetajwa jina lake kwa kifupi kama RB alipatwa na matatizo ya kupumua tangia siku aliyozaliwa kutokana na ugonjwa unaowatokea watu wachache sana duniani unaoitwa congenital myasthenic syndrome (CMS ).

Ugonjwa huo umemfanya mtoto RB ashindwe kufanya kufanya kitu chochote kutokana na mishipa yake ya fahamu kushindwa kuwa na mawasiliano na misuli ya mwili wake.

Alipozaliwa alitumia dakika 40 tu kupumua mwenyewe kabla ya kuanza kupumua kwa kutumia mashine hadi leo.

Ubongo wake unafanya kazi kama kawaida na ana uwezo wa kusikia, kuona na kutambua vitu vinavyomzunguka lakini misuli ya mwili haina uwezo wa kufanya kitu chochote na hawezi hata kutabasamu.

Hospitali anayopatiwa matibabu na mama mzazi wa mtoto huyo wanaitaka mahakama iruhusu mtoto RB aondolewe kwenye mashine zinazomsaidia kuishi ili aweze kufariki aondokane na mateso anayopata.

Lakini baba mzazi wa mtoto huyo hataki mtoto wake aachwe afariki kwani anaamini mtoto wake anaweza akaendelea na maisha yake iwapo atafanyiwa matibabu yanayoitwa tracheotomy, ambapo tundu litatobolewa kwenye shingo yake ili kumruhusu apumue mwenyewe bila kutegemea mashine.

Mahakama inategemea kuanzisha uchunguzi mpya wa kidaktari kuangalia kama kweli njia hiyo ya tracheotomy ni sahihi kwa mtoto huyo na itaweza kuokoa maisha yake.

Kama mama huyo kwa kushirikiana na hospitali watashinda kesi hiyo na mtoto huyo kuachwa afariki basi itakuwa ni mara ya kwanza nchini Uingereza mashine ya kumsaidia mgonjwa kuishi kuzimwa ili kumruhusu mgonjwa afariki wakati mgonjwa akiwa hana matatizo yoyote ya ubongo.

Wakili wa mama huyo alidai kuwa kila siku inayopita mtoto wake amekuwa akiteseka kwa maumivu makali hivyo inabidi aruhusiwe kufariki ili aepukane na mateso hayo.

Wakili wa mama huyo aliendelea kusema kuwa mtoto huyo ameishapelekwa kwa madaktari wakubwa duniani lakini hakuna tiba iliyopatikana.



Source: News Agency
 
naona aruhusiwe kufariki!

i can imagine how painful it is
 
Back
Top Bottom