Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Kwa kweli mama huyu amefedhehesha na kuitia nchi aibu kubwa. Hivi ataendelea na ubunge wake wa Ukerewe hizi tuhuma zikithibitishwa?

Kuna baadhi ya watu wamefurahia hii dhahama lakini ukweli ni kwamba inahuzunisha sana. Poor Getrude!
 
Alifikiri bado yuko kwenye anga za kula fedha za Watanzania, safarii zitamtokea puani na makalioni.
Atakoma kulinga.
 
Hivi mtu wa Kigurunyemb, au kule Nkasi, au Mabokweni, au Ndali anaguswa vipi na mama huyo kupata nafasi ya kula na kutafuna? Tumepiga kelele ya upotevu wa mamilini benki kuu na mambo mengine je wanakijiji wenzangu wanaweza kushawishiwa vipi kuona kuwa maisha yao duni yanahusiana moja kwa moja na utawala ulio madarakani? Sasa hivi tuhuma hizi kwa wananchi wengi ni picha ya samaki tu hayawahusu.

Wengine wanaweza kufikiri hivyo hivyo kuwa kama na mimi ningepata nafasi ya kula kama mama Mongella na mimi ningetafuna vile vile. Baadhi yetu hatuoni ubaya wa matumizi mabaya ya ofisi ndio maana hakuna mwana CCM mmoja aliyejitokeza hadharani kulaani kitendo cha Mkapa kutumia ofisi yake vibaya. Sasa zikipigwa hizi kelele halafu JK akatokea na kusema "mwacheni mama huyu aendelee na utumishi wake msimsingizie" mnafikiri wananchi watakuwa interested wakati "rais kashasema"?

Kitu kimoja ambacho nakiona ni mgawanyiko uliopo kati ya "elite" wa Tanzania na wale ambao ni wananchi wa kawaida tu. Walio elite wanataka kupata nafasi za "kutumbua" na wale walioko mtaani wanatamania nafasi za kutumbua.
 
Hivi mtu wa Kigurunyemb, au kule Nkasi, au Mabokweni, au Ndali anaguswa vipi na mama huyo kupata nafasi ya kula na kutafuna? Tumepiga kelele ya upotevu wa mamilini benki kuu na mambo mengine je wanakijiji wenzangu wanaweza kushawishiwa vipi kuona kuwa maisha yao duni yanahusiana moja kwa moja na utawala ulio madarakani? Sasa hivi tuhuma hizi kwa wananchi wengi ni picha ya samaki tu hayawahusu.

Wengine wanaweza kufikiri hivyo hivyo kuwa kama na mimi ningepata nafasi ya kula kama mama Mongella na mimi ningetafuna vile vile. Baadhi yetu hatuoni ubaya wa matumizi mabaya ya ofisi ndio maana hakuna mwana CCM mmoja aliyejitokeza hadharani kulaani kitendo cha Mkapa kutumia ofisi yake vibaya. Sasa zikipigwa hizi kelele halafu JK akatokea na kusema "mwacheni mama huyu aendelee na utumishi wake msimsingizie" mnafikiri wananchi watakuwa interested wakati "rais kashasema"?

Kitu kimoja ambacho nakiona ni mgawanyiko uliopo kati ya "elite" wa Tanzania na wale ambao ni wananchi wa kawaida tu. Walio elite wanataka kupata nafasi za "kutumbua" na wale walioko mtaani wanatamania nafasi za kutumbua.[/QUOTE]

Haswa! Hiki ndicho Askofu Tutu alikiita kupoteza moral bearing! Vibaka, wezi, con artists etc. tunawaita "sharp". Wazazi hatushangai utajiri wa haraka haraka wa wanetu bali tunamlaumu yule anayefuata ethics kuwa amezubaa! Itakuwaje leo tushangae kwa hili kama ni kweli! Uozo umeanza mbali kwenye jamii. Tumefikaje hapa?
 
Fundi Mchundo, suala la undugunization tumelikubali kama "haki"; tunapozungumzia mgongano wa maslahi tunaonekana "hatuwapendelei" watu na tunawaonea wivu. Tukisema turudishe misingi ya miiko ya uongozi tunaonekana tunatka kurudisha Azimio la Arusha. Wanataka tukubali kuwa Ubepari tuliooupokea hauwezi kutiwa pingu na tuukumbatie jinsi ulivyo. Na hapa ndipo naona ugumu wa mapambano haya ya kifikra ambacho tunayachochea. Hadi tubadilike kifikra kwanza ndio tutaweza kubadilika kivitendo!
 
Kweli tupu Mkuu! Imekuwa kama the Tanzanian Dream. Iko siku na mimi au ndugu yangu ataingia katika sehemu ya ulaji. Tunataka mafanikio ya haraka haraka bila ya kuyatolea jasho wala kuangalia athari zake za muda mrefu. Tumekuwa wavivu wa kuhoji kwa kuogopa kutoalikwa/kufukuzwa kwenye karamu.

Ni wepesi mno kushangilia badala ya kusema, hebu tuvute pumzi kwanza,hivi haya unayoyasema yanawezekana kweli. Tumekuwa mafundi wa kuiga bila kuuliza. Tumekuwa wapenzi wa kusifiwa bila kuuliza azma ya huyo anayetusifia. Tu rahisi kuvikwa vilemba vya ukoka. Iko kazi kweli!
 
Hivi mtu wa Kigurunyemb, au kule Nkasi, au Mabokweni, au Ndali anaguswa vipi na mama huyo kupata nafasi ya kula na kutafuna? Tumepiga kelele ya upotevu wa mamilini benki kuu na mambo mengine je wanakijiji wenzangu wanaweza kushawishiwa vipi kuona kuwa maisha yao duni yanahusiana moja kwa moja na utawala ulio madarakani? Sasa hivi tuhuma hizi kwa wananchi wengi ni picha ya samaki tu hayawahusu.

Wengine wanaweza kufikiri hivyo hivyo kuwa kama na mimi ningepata nafasi ya kula kama mama Mongella na mimi ningetafuna vile vile. Baadhi yetu hatuoni ubaya wa matumizi mabaya ya ofisi ndio maana hakuna mwana CCM mmoja aliyejitokeza hadharani kulaani kitendo cha Mkapa kutumia ofisi yake vibaya. Sasa zikipigwa hizi kelele halafu JK akatokea na kusema "mwacheni mama huyu aendelee na utumishi wake msimsingizie" mnafikiri wananchi watakuwa interested wakati "rais kashasema"?

Kitu kimoja ambacho nakiona ni mgawanyiko uliopo kati ya "elite" wa Tanzania na wale ambao ni wananchi wa kawaida tu. Walio elite wanataka kupata nafasi za "kutumbua" na wale walioko mtaani wanatamania nafasi za kutumbua.

Aisee kama una macho hauna haja ya kushawishiwa na mtu mwingine. Utajionea tu mwenyewe na kama hupendezwi na unachokiona basi unakiondoa. Hakuna ugumu kabisa hapo. Wanakijiji wanajua tofauti ya right and wrong ila sijui kwa nini hawafanyi kweli wakati wa uchaguzi. Wakati wa kampeni hawa watawala si huwa wanatembelea Tanzania nzima na kutoa mi ahadi kibao? Sasa kama wakishapata hayo madaraka halafu wanaishia kuwasahau wanavijiji nani wa kulaumiwa?
 
1.
haindoi ukweli umekuwa ukiwatetea sana jamaa zako waliopo Foreign kwa amna mbali mbali na saa zingine huwa unaomba threads zihamishwe pale tuhuma zinapokuwa nzito zaidi na mfano ni ule wa Caro wa Ubalozi wetu London na mumewe kuuza bwimbwi na ulipoambiwa ulikuja juu.

Madai kuhusu Caroline, kwamba amerushwa vyeo hayakuthibitishwa sio mimi niliyeihamisha ile thread, mmiliki wa hii forum alisema wazi kuwa zitolewe evidence na akatoa muda maalum, hazikutolewa akaamua kuihamisha ile thread, mimi sio mmiliki wa hii forum huo ubavu nitautoa wapi mkuu?

Mimi siko hapa JF kufuata mkumbo na sitegemei kuwa kuna wanaofuata mkumbo wa wengine, yaani kushambulia tuu wananchi wengine bila sababu ya msingi, ili mradi kushambulia tuu waonekane wanajua na kuchafua majina ya wengine no mkuu, na wala sina jamaa foreign kama unavyodai,

However, Walter mume wa Caroline, ni mwanasheria wa kujitegemea tena kijana anayeheshimika sana Dar, kutokana na kazi zake za kisheria na yeye ni mshiriki wa umiliki wa Law Firm na baba yake, kuna vijana wengi sana wa rika lake ambao wamebobea kwenye sheria, kama kina Masha, Margai, Mujulusi, Ishengoma, na hawa kina Walter, hawa vijana ni matajiri sana kwa standard zetu za bongo na wameupata kwa haraka haraka kutokana na kufunguliwa milango ya kiuchumi hivi karibuni, sasa kama Walter anauza bwimbwi basi ina maana hawa wote niliowataja hapo juu mpaka kina Mkono wanauza hilo bwimbwi, that is a big lie kama sio a pure nonesense, wanachi ni lazima tukubali kuwa wanasheria walibanwa sana zamani, lakini sio sasa milango imefunguliwa sasa tusishangae kuwaona wanatanua ni haki yao mkuu, wao na madaktari wanatakiwa kutanua katika nchi yoyote ile yenye maendeleo.

2.
Kuhusu wakina Mahiga ndio usiseme

Kuhusu suala la Mahiga, ni yale yale kuna mtu ana chuki naye binafsi akaamua kuja hapa kumchafulia jina tu bila sababu ya msingi, mkombwa data hamna sasa hivi mkuu mnatakla tuje tu hapa na kuanza kuwatukana viongozi na wananchi bila sababu?

3.
Mzee sie wengine tunao hao jamaa huko huko CCM lakini hatuishi kuwatoa nishai kila kukicha maana nchi yetu wote na hatuwezi kujidai tunaitakia mema nchi huku tunakuwa na double standards jamaa zetu wakituhumiwa kwa ubadhirifu

Kama ni kweli basi mkuu weka ukweli hapa sio kuharibu majina ya viongozi bila sababu za msingi, mimi sina jamaa yoyote huko CCM kama wewe, lakini msimamo ni very clear kwa kila mjumbe hapa kuwa mnyonge mnyongeni lakini haki apewe, ukweli uwekwe hapa hakuna sababu ya kuleta viroja, hoja hujibiwa kwa hoja ila mimi msimamo wangu ni ule ule siwezi kushambulia wananchi wasiokuwa na makosa ili tu nionekane nimo kwenye crowd, hapana mkuu!


4.
Nakuheshimu sana lakini saa zingine huo moyo wako wa kuwatetea hawa watu huwa inaboa haswa

Nimekusikia mkuu, lakini kwenye hoja hakuna boa nia na madhumuni hapa ni kuweka hoja na kupingana kihoja, anything else ni lazima iboe maana hakuna ukweli ndani yake sasa si lazima iboe!
 
Kama ni undugunization records zinaonyesha kuwa huyu mama (Mongela) ana undugunization. Alipokuwa UN miaka ya 90 ali m-hook up dada yake pale UN (I have nothing agaist that) na mpaka leo yule mama bado yupo UN.

Mtoto wa dada yake anayefanya kazi pale ubalozi NY aliajiriwa kwa muda wakata TZ ikiwa baraza la usalama UN lakini kile kitengo kilivyokwisha ubalozi ulimuomba yule binti aendelee kwani ana sifa nzuri. Amefanya shahada yake ya kwanza International Studies - CUNY, halafu akaenda UDSM kufanya postgraduate kwenye masuala hayohayo ya kimataifa.

Mzee FM, Mimi ninavyofahamu mke wa mtoto wa Malecela, former baharia anafanya kazi ubalozi wa TZ pale NY. Huyu mama ndiyo huyo mtoto wa Malecela mwenye BA ya India? Naomba usawazishe hapa mzee.
 
Mzee FM, Mimi ninavyofahamu mke wa mtoto wa Malecela, former baharia anafanya kazi ubalozi wa TZ pale NY. Huyu mama ndiyo huyo mtoto wa Malecela mwenye BA ya India. Naomba usawazishe hapa mzee.

Mkuu heshima mbele, mke wa baharia alikuwa ubalozi wetu Belgium kwa miaka sita, ambako pia alisomea lugha mbali mbali kama kijerumani na kifaransa, yaani fluent huko Brussles, baadaye akaolewa na huyo mkuu Baharia na kuhamia NY, baadaye akajiriwa hapo ubalozini for the last 8 years kama local staff, mwenye BA ya India, amekuwa posted huko miezi kama sita iliyopita baada ya kujiunga na foreign miaka mitatu iliyopita, I hope nimekusawazishia mkuu!
 
Mkuu heshima mbele, mke wa baharia alikuwa ubalozi wetu Belgium kwa miaka sita, ambako pia alisomea lugha mbali mbali kama kijerumani na kifaransa, yaani fluent huko Brussles, baadaye akaolewa na huyo mkuu Baharia na kuhamia NY, baadaye akajiriwa hapo ubalozini for the last 8 years kama local staff, mwenye BA ya India, amekuwa posted huko miezi kama sita iliyopita baada ya kujiunga na foreign miaka mitatu iliyopita, I hope nimekusawazishia mkuu!

Are you trying to say that we have two family members in one station? Who is protecting my interest?
 
Are you trying to say that we have two family members in one station? Who is protecting my interest?

Usishangae sana bana! ... mbona Karume (balozi) aliomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM. Ina maana kama angekubaliwa na jina lake kupitishwa basi leo hii Karume mmoja angekuwa Ikulu ya Dar pale Kivukoni na Karume mwingine angekuwa Ikulu ya Zenji. Kwani kuna ubaya?

Unataka walinde interest zako zipi tena jamani?
 
Usishangae sana bana! ... mbona Karume (balozi) aliomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM. Ina maana kama angekubaliwa na jina lake kupitishwa basi leo hii Karume mmoja angekuwa Ikulu ya Dar pale Kivukoni na Karume mwingine angekuwa Ikulu ya Zenji. Kwani kuna ubaya?

Unataka walinde interest zako zipi tena jamani?

Interest zangu mimi kama mtanzania (maslahi ya taifa) kwani suala ni comflict of interest. Ndiyo maana huyo Karume alipigwa chini kwenye kinyang'anyiro cha urais.
 
Are you trying to say that we have two family members in one station? Who is protecting my interest?

Hizo nafasi za ubalozi kama local staff mbona sio deal kabisa jamani? Labda hao wanaotumwa toka nyumbani lakini kama ni hizi kazi ambazo hata foreigners kibao wanapewa, mimi naona sio kitu cha kushikana mashati.

Huu upendeleo upo na utaendelea kuwepo kwasababu hao ndio wanakuwa na habari kama kuna kazi na hivyo rahisi kuwaambia ndugu zao waombe kuliko kijana mwingine ambaye hana hili wala lile. Hiyo inatokea hata kwenye private companies. Hata huku majuu tunaamini 60% ya kazi zinapatikana kwa kujuana. Kadri unavyokuwa na wafanyakazi wengi wa makampuni mbalimbali unaokunywa nao bia, kucheza nao golf, au uliofanya nao kazi zamani, ndivyo inavyokuwa rahisi kupata kazi mpya ukiamua kuhama au ukipoteza kazi uliyo nayo.

Conflict of interest ni zaidi ya hao wana ndugu wawili kufanya kazi shirika moja. Sheria za kimataifa zinaeleza wazi juu ya hilo. Ni tofauti na hili la mama Mongela kumwajiri mke wa mtoto wake kama msaidizi. Hata kwenye maadili ya kawaida tu, huwa inakatazwa kuajiri ndugu yako wa karibu kama msaidizi.
 
Wanakijiji wenzangu especially wale watoto wa wakulima inabidi tuyakubali mabadiliko ingawa ni machungu. Siku hizi kazi bwana ni kupambanisha vyeti, haijalishi mtoto wa Sumaye alisoma US na mtoto wa Masanja alisoma Mzumbe, kikubwa ni uwezo na elimu. Kama ES alivyosema, enzi hizi hatuwezi kulalamika tuu kwamba kuna undugunization, hilo halitaisha milele, popote pale utakapoenda hilo lipo. Kikubwa tuitafute ELIMU kwa udi na uvumba. Ni dhahiri wengi wa watoto wanaoajiriwa mfano kwenye mabenki au foreign cos. Dar ni wale waliosoma nje wanaojua kizungu vizuri, sasa sisi tuliosoma shule za sikinde tufanye nini? ni kujitahidi kuwa competent, maana kuna vitu vingine havizuiliki. kama hukuweza kwenda UK, basi tumia elimu yako ya mlimani kuprove kwamba you can deliver. Period. hata huko UN, kumbuka wanaapply kazi watu waliosoma Harvard na mzumbe, Oxford na Mkono au Eldoret University, ndo globalization yenyewe, sasa hapo ni jukumu lako wewe wa Eldoret uonyeshe kwamba unaweza kufanya kazi kwa umahiri kuliko hata yule aliyesoma shule bora zaidi. Ndo challenge za dunia ya leo na inabidi tuzikabili tuu.

Uzuri wa kazi za mataifa bwana siku hizi unasukuma makaratasi kwenye mtandao na kama unafaa wanakuchukua. Tuache kulalamika, kuna mambo hata angerudi Kristo yataendelea kuwepo. Undugunization ukiwa mojawapo. Ukienda BOT uka-question ajira ya mtoto wa Rupia au Lowassa utaambiwa ana bachelor na masters za UK au US!?? hapo huna hoja tena maana kuwa BOT ni elimu na uwezo na wala sio kuajiriwa kwa quarter! Its hard but its the bitter truth.

Kuhusu Foreign mimi sina experience napo lakini as any other governement office, ni kupambana nao, unajua inafika point hata wanaotoa kazi inakuwa vigumu kukunyima kama una qualifications na experience sahihi. Ndo maana nasema kila siku ukombozi wa kweli ni wa elimu mengine ni kudanganyana tuu. Hebu jiulize wewe uliye UK au US mtoto wako anasoma, international school, anatumia laptop akiwa chekechea, I mean mazingira ni saaafi, wakati mtoto kama huyo huyo yuko Ludewa au Kasulu mpaka anamaliza Form six hajaiona compyuta, na wengine mpaka wanamaliza chuo hawana email account, harafu hawa wawili unategemea wakapambane kwenye soko la ajira! Waungwana tuwe serious jamani.

Uzuri wa kazi kama za UN uki fanya madudu, basi watakwambia na kweli kama mama Tibaijuka alifanya ujinga wake pale UNON Nairobi, basi ajue kwamba dawa yake wanaichemsha!
 
Interest zangu mimi kama mtanzania (maslahi ya taifa) kwani suala ni comflict of interest.

Mkuu eti John Kennedy akiwa rais wa US, huku Bobby Kennedy akiwa mwanasheria mkuu wake, kulikuwa na conflict of interest? Bush kuwa rais, huku Jebb Bush akiwa Gavana, na Baba mtu akiwa rais mstaafu kuna conflict of interest? Paul Boman akiwa waziri na mdogo mtu Mark Bomani akiwa mwanasheria mkuu wa serikali kulikuwa na conflict of interest? Masha akiwa waziri na baba yake mbunge wa EAC kuna conflict of interest? Rosemary Nyerere alikuwa mbunge wa viti maalum, na huku Makongoro Nyerere kaka yake akiwa mbunge wa kuteuliwa na rais kulikuwa na conflict of interest? Aman Karume rais wa visiwani, Ali Karume balozi wetu Germany eti kuna conflict of interest?

Eti mkuu unasema kuwa hapo kuna tatizo na masilahi yako wewe au ya wengine? Eti haya ya conflict of interest ni ya kweli au ni fitina tu? Hivi labda sielewi maana kamili ya conflict of interest vipi mkuu ukituweka sawa on hilo?

Ndiyo maana huyo Karume alipigwa chini kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Ndio maana Karume alipigwa chini, lakini ikawa sawa kwake kuwa balozi huku kaka yake akiwa rais wa visiwani? are you serious mkuuu? Yaaani hii sijawahi kusikia mkuu labda uniweke sawa!
 
Masanja,

Mzee nakubaliana na wewe kwa sababu moja kubwa - Reality, lakini nje ya hapo sidhani kama itakuwa vizuri kulipokea hili la Undugunazation kama ndio globalization.

Mimi nakubaliana sana na ajira za undugu ktk sekta binafsi za biashara na ndizo wengi wetu tunazitumia kama kigezo cha hali halisi na inayotakiwa ktk dunia hii ya Utandawazi. Lakini nimejaribu kufanya utafiti mdogo sana ktk taasisi za serikali na mashirika ya Umma kama vile benki na kadhalika, nimeambiwa kuwa hairuhusiwi kabisa KISHERIA mwajiri hasa kiongozi kumpa kazi ndugu yake ndani ya shirika moja hata kama amesoma kupindukia tena basi hata mashirika binafsi yameanza kutokubali ndugu kufanya kazi sehemu (branch) moja ila mnaweza ajiriwa na kampuni moja lakini mkifanya kazi maeneo tofauti.

Pamoja na sheria zote hizi undugunatization hauwezi kwisha na watu bado hutafuta njia za kuvutana ndani ya mashirika ya kazi lakini inapobainika kuwepo kwa uvunjaji wa sheria hiyo basi mtu nyote hufukuzwa kazi. Hili ndilo lililomkuta mama yetu Mongella na wala tusifikirie kuwa kosa lake kubwa ni kuvuta hizo dollar pekee bali hata kuajiri ndugu zake ni kosa pekee ambalo lingemwondoa ktk nafasi alokuwa ameishika.

Nafikiri ni vema tukjifunza toka kwa wenzetu na kufahamu ubaya wa maswala haya ya Undugunization kwani kesho ndugu yangu unaweza pata nafasi kama ya mama Mongella kisha bila kufahamu ukamwajiri jamaa yako ukifikiria kuwa ni haki yake kutokana na CV yake nzito - Utaipoteza kazi.

Kibongo Bongo ajira kiundugu sii kosa na hakuna sheria inayolinda maslahi ya shirika dhidi ya ajira kama hizi na ndio maana tunahalalisha vitendo vya baadhi ya viongozi wetu lakini hata siku moja tusijidanganye kuwa tabia hii inafanya kazi vizuri hasa ktk taasisi za serikali. Undugunization unabomoa ethics za kazi kutokana na hisia za kibinadamu ambazo hazina cheti wala digree kama nyege. - Ooops! mtanisamehe!
 
Waheshimiwa mnaosema Dk Shein ni Dull.. hebu waulizeni wanaotoa Daily Briefings Pale ikulu.
Ni bora wakutane na Muungwana JK mwenyewe kuliko Shein maana Dk Shein ni msomaji mahiri na hingia in details kwenye kila report inayopitia kwake bila unafiki wala woga.. unlike Muungwana!
So.. kwa ndugu mnaosema kwamba Nchi haiwezi ku-afford kuwa na mtu "Dull" kama Shein siwaelewi!
Labda kinachomponza ni ukimya na kutokuwa kimbelembele!
The Guy is Clean, Intelligent & Patriot!

I believe siku ikitokea mtu wa dizaini ya Dk Shein kuwa President ndo siku Nchi yetu na CCM vitabadilika!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake Mpeni!
He is one of the bests in our current administration!

BRUTUS ..you are very right ..the other friend of mine told me the same..dr shein ndio at least anasaidia serikali kuwa hapo ilipo [behind the scene] at least unlike muungwana yeye anasoma sana reports as you said na aningia details..wanasema ukienda breafing ya muungwana inakuwea na jokes nyingi za hapa na pale..kama mnavyomjua..kila kitu anachukulia simple na hana haraka...

kingine kizuri au kibaya kwa shein ni is kind hana makundi ...hana pilika zaidi ya kazini,msikitini ,nyumbani basi...ana maadili mema..kwa maana hiyo si mfujaji wa pesa kabisa..hata kwenye ziara zake za nje pesa anazotumia ni kidogo ukilinganisha na watu kama BOYS 11 MEN..ambao mara nyingi hupenda ku host luncheon.,dinners..parties wakiwa viwanja..na kufanya shopping za hapa na pale..

THE only thing ninachoshangaa kama ni weakness ya PRESS TEAM YA VP..kina PENZI NYAMNGUMI na wenzake au ni uamuzi wa BOYS 11 MEN ..ni wazi kuwa habari za shein hazitangazwi sana..hii humfanya aonekane kama hayupo....unless ni mahitaji ya kiutawala kuwa VP iwe low profiled job...bu i can view kuwa wakati wa mkapa shein ziara zake zikikuwa zinakuwa well covered kuliko ilivyo sasa ..ambako covering kubwa inafanyika kwa lowassa na kikwete...yaani kuna mawaziri kama MIZENGO PINNDA ambaye PRESS TEAM yake inafanya covering kubwa kuliko hata ya VP ...ITS AS if he is tipped of big job in future........
 
Back
Top Bottom