Mama mkwe ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi?

alitaka mkutane wapi yeye
wakati mwingine wazazi na sie tuna mastress yetu
halafu tunayahamishia kwa watoto
mpeni alichofuata aweze kurudi kwake.
Mama kama hao wakikutanaga na dada zangu wa kizaramo wanakoma kuuliza maswali pumbavu kama hayo. Nategemea hapo jibu lingekua "tulikutana chooni"
 
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?

mwambie mlikuta kwenye danguro
 
alitaka mkutane wapi yeye
wakati mwingine wazazi na sie tuna mastress yetu
halafu tunayahamishia kwa watoto
mpeni alichofuata aweze kurudi kwake.
Wazazi sometimes mbahitaji maombi


Sent from BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kuna dalili wewe ndo una matatizo! Swali la ulikutana wapi na mwenzio linakuumiza kichwa? Au hukukutana nae?. Ungeulizwa kwanini ulimchagua huyu mwenzio ungepata jibu kweli? .
Ushauri, ktk maisha usipende kuwaza kuwa hata kwa kilicho wazi kina maani iliyojificha. Utagombana na watu utaharibu mahusiano yako. Kwa taarifa yako huyo mwenzio ni mtoto wa huyo aliyekuuliza hilo swali -mtoto wa nyoka ni nyoka,tarajia mwezio atakuwa akikuuliza maswali ya hivihivi.sasa nayo yatakunyima raha?
tatizo una generalize issues!!
kwa hiyo mama mkwe aniulize swali kama hilo akiwa ana maana gani hasa? binafsi nashukuru sijawahi kuulizwa maswali ya ajabu ajabu na mama mkwe kama hili. Mama anayemuheshimu mkwe wake hawezi kuuliza swali kama hilo ndg yangu, wengine wamekutana bar, wengine disco(thank God mimi sikukutana na wangu maeneo kama hayo), imagine mtu amjibu tulikutana disco, wewe unadhani nini kitatokea hapo hasa kwa mama ambaye hapendi hata kusikia kitu kinachoitwa disco, try to to think big!!
 
Ulipaswa umjibu tu wala sio swali gumu sana na nilakawaida kabisa.Alitaka kujua kuwa mtoto wake bahati iyo ilimkutia wapi.
 
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?


yawezekana kuna tabia ameziona kwako ambazo hazimfurahishi au amependezwa na jinsi unavyoonesha tabia nzuri.
 
kaona nn mpaka anakuuliza ivo?
pengne ni kwa nia nzuri tu,afahamu wapi kijana wake alibahatikia kukuona ww.
 
Nilijibu swali kuwa, mama mkwe hatukai nae, amekuja tu katika mji tunaishi lakini anaishi mkoani. Ni moja ya mikoa ya Tanzania.
Si useme Tanga?? unarukaruka nini? ndo wenye maswali hayo, Mwambie we ni jini , ulimnasa kimazingaumbwe
 
woga wako ndio umekufanya usijibu swali hilo! mama amekuuliza hivyo sababu kubwa huna adabu, unawezaje kuishi na mwanume bila ya ndoa...?
 
Wanawake watu wa ajabu sana. Kila mmoja anasema mama mkwe ni mbaya sana, lakini akiulizwa vipi
mama yako Mzazi? Atakwambia mama yangu ni mtu mwema sana hana matatizo, anasahau mama yake
naye anaitwa mama mkwe mahali fulani.

Na ndiyo mantiki ya huyu kujishuku na kushindwa kumjibu mama mkwe wake. Na kila kitu ataishia kushuku:

1. Akiulizwa unaenda wapi? ataona anachunguzwa
2. Tunakula nini leo? ataona anazongwa
3. Naomba ukitoka mjini uje na soda....ataona anakerwa
4. Akiona mama mkwe na mtoto wake wanacheka....atahisi wanamsema.

Lakini maneno hayohayo akiambiwa na Mzazi wake hataona kero.
Wanawake mnapaswa kujua hao akina mama mkwe ndiyo haohao mama zenu, bibi zenu na shangazi zenu!
 
mbona ni swali la kawaida sana hili? au mlikutana kwenye danguro sasa unaona noma kumjibu?
 
Kuna mambo kama mawili naweza fikiri yalipelekea kuulizwa....kwanza inawezekana kuna jambo ameliona kwako liwe baya au zuri linalomwacha na maswali ya kutaka kujua mlipokutana na mwanae.....pili inawezekana ni aina ya wakwe wanaopenda story na wewe haupo kihivyo hivyo alitaka uanze kujibu swali lake ili nae afunguke alivyokutana na mumewe. Wapendwa dada zangu wenye ndoa na ambao bado tusichukulie kwamba wakwe ni watu watata wasiofaa kuishi au kuuliza jambo katika ndoa zetu, tukumbuke kama nasi tukibarikiwa na kupewa watoto na umri kama wao tutakuwa kwenye hali hii. Tujenge maisha yetu tuyatakayo baadaye kwa kuwachukulia wengine kwa jinsi yao ili nasi tupate kuja hurumiwa na kujaliwa hapo baadaye. Ni hayo tu ukipenda meza ukipenda tapika ila ukweli utabaki kama kivuli na kitu.
 
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?

Najiuliza hapa ... swali hili haliwezi kuwa limeulizwa kwa malengo chanya/kwa nia nzuri??
Nafikiri inategemea na mazingira aliyokuulizia mfano kabla ya swali hiili mlikuwa mnazungumza nini, tune yake wakati anauliza ilikuwaje.. n.k.

kuwa mpole shostito huenda hana hata nia mbaya.
 
Najiuliza hapa ... swali hili haliwezi kuwa limeulizwa kwa malengo chanya/kwa nia nzuri??
Nafikiri inategemea na mazingira aliyokuulizia mfano kabla ya swali hiili mlikuwa mnazungumza nini, tune yake wakati anauliza ilikuwaje.. n.k.

kuwa mpole shostito huenda hana hata nia mbaya.

Tone ilikuwa ya kejeli flani hivi, swali lilikuja baada ya salamu asubuhi tu.


 
Tone ilikuwa ya kejeli flani hivi, swali lilikuja baada ya salamu asubuhi tu.

diiii sasa hiyo kali..kama kalala anakuota vile daa! La muhimu.. wewe achana nae hakuna ulazima wa kuanza kumuelezea. But uwe makini tu naye(usimwonyeshe kama limeku kera... n try to ignore it).. usije ukajishushia heshima yako kwa mkweo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom