Mama Kanifichia paja!!!

mama ni mama, mkeo asingelikujua bila mama, bali mke ana nafasi yake , na mama ana nafasi yake. kimsingi ongea na mkeo awe karibu na mkwewe , ajifunze sio kununa wala kuanza hila. huyo ni mama yako, mtoto kwa mama hakui, achukue hizo changamoto kama somo atamuelewa mkwe wake na kama akishindwa basi avumiliue na wala asionyeshe kukerwa, kwani mama kahamia hapoooo, si amekuja kusalimia tu!!!! bali akumbuke kesho yeye naye ni mama hivyo atajukuta hili linalotokea sasa likahamia kwake. ndio maisha.
 
mama mama mamaa...

Upendo wa kukulipa cna...

Kwa taabu ulininyonyeshe...
By böni mwaitege
 
Kheeee!Huyo mkeo ananuna badala ya kubadilika na kuanza kukuachia chakula kizuri walacho mchana?!Mwambie akue na aache uchoyo.
 
Kheeee!Huyo mkeo ananuna badala ya kubadilika na kuanza kukuachia chakula kizuri walacho mchana?!Mwambie akue na aache uchoyo.

Mi naona si mchoyo ila alikuwa anamkarimu mama mkwe zaidi(mama mkwe alikula hizo kuku mchana).................nafikiri kwa kuwa ni mgeni aliamua amtoe kwa kuku na pengine hakuwa anatosha kwa wote.................tafsiri ya mama mkwe ndio ilikuwa mbaya..........

Mara ngapi tunawakarimu wageni huku sisi tukishinda bila kula kama chakula hakitoshi?................si ndio utamaduni wetu??........

Hivi mume hata kama mmegombana utamfanyia uchoyo???...........sina hakika na hili......................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom