Malumbano ya hoja ITV: Madaraka ya Rais katika katiba mpya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Kipindi ndio kimeanza.
Wachokoza mada ni hawa,
1. Godwin Kunambi toka ccm
2. Julius Mtatiro toka cuf
3. Stanley Temba toka TCD.
 
naona huyo mwanasheria wa ccm, yeye anasema haya madaraka yaendelee tu, na anasema kuwa rais hateui majaki hivihivi.. anapitia kwenye tume ya majaji.... huyu jamaa sijui anawaza nini haya mambo lissu alishayasema, hao wajumbe wenyewe kwenye hiyo kamati ni wateuzi wake sasa unategemea hiyo tume itampinga?? kweli ukiwa sisi emu hata uwezo wa kufikiri, na utu hupungua pia
 
matatiro, anakili kuwa hayo madaraka ni makubwa sana na hayanabudi kupunguzwa ili kuleta uchumi na taifa imara, huyo mzee wa TCD naye amekili kuwa ni makubwa,... naona huyo kada wa sisiemu anajidai ni mwanasheria leo atapata shida sana katika hiki kipindi
 
Kipindi ndio kimeanza.
Wachokoza mada ni hawa,
1. Godwin Kunambi toka ccm
2. Julius Mtatiro toka cuf
3. Stanley Temba toka TCD.

Mkuu Mwita sioni mwakilishi wa chama chetu kulikoni? au katiba haituhusu?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kunambi wa ccm anaunga mkono madaraka ya raisi yaendelee kuwa kama yalivyo. Anatoa mfano wa suala la ardhi kuwa chini ya raisi kwamba yakiondolewa kuna wananchi wengi watashindwa kuimiliki.

Temba wa TCD anapendekeza madaraka ya raisi yapunguzwe. Anatoa mfano wa raisi kutolazimika kupokea ushauri wa mtu yeyote katika kutekeleza majukumu yake. Mfano raisi anaweza akaamua kuanzisha mkoa ama wilaya ili kuwapa nafasi marafiki zake.

Mtatiro wa cuf anapendekeza madaraka ya raisi yapunguzwe. Kiuhalisia raisi si taasisi kwakuwa kikatiba haimlazimishi kupokea ushauri wa mtu na anazungumzia madaraka ya raisi kuteua kila kiongozi kuanzia mawaziri, majaji na hata tume ya uchaguzi ambayo inasimamia uchaguzi ambao yeye raisi anakuwa mshindani hivyo kutokuwepo na kutendewa haki wagombea wa vyama vingine.
 
Makada wa ccm wanaongea upuuzi nashindwa kuelewa huyu jamaa anayesema ni wakili wa kujitegemea alishawahi kushinda kesi mahakamani!
 
Mwita chacha mwikabe,anakili kuwa nguvu bado ziko upande mmoja, anampiga vikali yule kada wa ccm aliyesema kuwa eti ukisha mchagua raisi eti yeye ndiye anakuwa na mari ya mwisho, mwikabe anasema hata USA hakimu anapigiwa kura na wananchi, so anaonyesha matatizo yaliyopo
 
Wanasheria wa ccm wameamua kuwakilisha kile ambacho wamekisambaza nchi nzima kama mwongozo kwa wanachama wao.
Hawataki madaraka ya raisi yaguswe.
 
pia kuga mzirai anasema, raisi wa tz anamadaraka hata kuliko malikia wa uk au waziri mkuu wa japani, anasema waziri mkuu wa tz hana mamlaka yoyote anapendekeza, madaraka ya rais yapunguzwe, hata kinga ya raisi anasema ibara ya 36 raisi anakinga hata akifanya nini hawezi kufanywa lolote kwa makosa ya jinai... hiyo ndiyo shida hasa
 
Mkuu kama uko jirani na tv yako utakuwa umemuona kamanda Waitara.

Mkuu nipo karibu na tv naangalia cnn huku siipati tbc labda kama utanipa web address yao, nilimaniisha sioni kwa maana ya orodha ya uliyotoa sikuona mwakilishi wa chetu; utagombea wapi chaguzi zijazo?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Naona kumbe hapa tume ya katiba mpya inajidanganya tu, na watz tunapoteza muda, kumbe ccm wameshatoa waraka wakuhakikisha madaraka ya rais yasipunguzwe, hapo ndio naanza kunusa harufu ya matatizo mbeleni
 
Pia Rais ni sehemu ya Mbunge.HII NAYO HAIJAKAA SAWA.RAIS ASIWE SEHEMU YA MBUNGE
 
Makada wa ccm wanaongea upuuzi nashindwa kuelewa huyu jamaa anayesema ni wakili wa kujitegemea alishawahi kushinda kesi mahakamani!
hawazungumzii uhalisia yaani reality wanazunguzia siasa za kihafidhina yaani coservatism. hawa ni watu rigid
 
Makaidi anasema hakuna katiba mpya watanzania tunadanganywa.
Anasema raisi wetu ni ''imperial president'' kwamba anaweza kuanzisha na kufuta eneo la kiutawala na kumteua mshikaji wake kuiongoza.
Anasema tunahitaji raisi kiongozi si raisi mtawala.
 
unajua hata wakati wa kuamua tuwe na vyama vingi au hapana wanafiki wachache walisisitiza chama kimoja mwalimu akasema hapana. baadae walisimama majukwaani wakimba unaona CCM tumeamua kuwa na vyama vingi japokuwa ni 20% tu walitaka hivo. si unafiki huo. sasa tunasema madaraka ya raisi yapungue wanajifanya hawataki lakini ukweli wanauona
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mwakilishi wa nccr mageuzi anasema raisi kutoa msamaha kwa wafungwa ambao majaji wametumia taaluma na weledi wao kuwatia hatiani kwa makosa waliyotenda.
Kwa kufanya hivyo anakuwa anaingilia uhuru wa mahakama.
Pia anasema raisi kuwa na uwezo wa kulivunja bunge inapotokea halijapitisha bajeti ya serikali inasababisha bunge kutokuwa huru kufanya maamuzi yake.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom