Malkia wa Unga

Vito Ferari

JF-Expert Member
Mar 31, 2022
290
412
Sehemu ya 1:

Nyasule Suleiman, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani, alimuaga mama yake aliekuwa kwenye genge lake la kuuza nyanya asubuhi hii ya jumatatu,kuwa anaelekea shule. " Mama, mimi naenda shule, tutaonana baadae", Nyasule alimuambia mama yake ,"Sawa mwanangu, nakutakia masomo mema".
Mama Nyasule alimjibu.

Mama Nyasule akamuangalia biniti yake akielekea shule, kisha kumbkumbu ya miaka kumi na sita iliyopita ikamjia kwenye akili yake.

Mama Nyasule jina lake kamili ni Zainabu Suleiman ,mzaliwa wa Ujiji , Kigoma, kwenye kijiji cha Usawile,baba yake mzazi alikuwa mvuvi, mama yake mkulima, Zainabu alikuwa anaishi na wazazi wake hapo kijijini, baba yake mara nyingi anasafiri kwenda ziwani kuvua samaki, anaweza kukaa huko ziwani zaidi ya wiki moja , Zainabu anabaki nyumbani na mama yake.

Zainabu alipofika darasa la saba, akiwa na umri wa miaka kumi na sita akaanza kujihusisha na wanaume, alipata kijana jirani yake , aliekuwa mvuvi akamrubuni, na hatimae kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, waliendelea na yule kijana kwa muda wa miezi sita, siku moja,wiki kadhaa kabla ya kufanya mtihani wa darasa la saba, walikuja madaktari shuleni kwao, walipima wanafunzi wa kike ujauzito, Zainabu alipopimwa akakutwa na mimba.

Kesho yake asubuhi, akiwa darasani, aliitwa na mwalimu mkuu." Zainabu, mwalimu mkuu anakuita ofisini kwake", rafiki yake Anna wanaesoma wote darasa moja alimuambia. Zainabu akafunga kitabu chake alichokuwa anasoma, na kuelekea kwenye ofisi ya mwalimu mkuu. "Ingia ukae", mwalimu mkuu akamuambia. Mwalimu Mkuu akamuangalia Zainabu kisha akamuuliza, 'Una miaka mingapi"?.
" Kumi na sita", Zainabu akajibu. ""umeanza kujihusisha na mapenzi",? Mwalim mkuu akamuuliza , " Hapana", Zainabu akajibu, akamkumbuka mpenzi wake mvuvi John.

"Hapana?, sasa hiyo mimba umeipata wapi"? Zainabu aliposikia alipata mshtuko, kidogo azimie. "Sina mimba mwalimu". "Huna mimba, wakati jana umepimwa umekutwa na mimba"?. Zainabu akaanza kulia"Mimi sina mimba mwalimu". "Kwa hiyo nakusingizia sio, unadhani mimi ni mtoto mwenzio "? Mwalimu mkuu alimuambia, "Ondoka,rudi nyumbani,nenda kalete wazazi wako hapa sasa hivi, haya, tokaa, malaya we"!

Zainabu akaondoka ofisini huku analia, akarudi darasani, na kubeba begi lake,akaondoka, wanafunzi wenzake wakamuangalia kwa mshangao,huo ndio ukawa mwisho wa Zainabu kusoma.

Zainabu hakurudi nyumbani, akaenda moja kwa moja kwenye chumba cha John, mpenzi wake alikuwa nje ya chumba chake anaandaa samaki wake aliowavua kwa ajili ya kwenda kuwauza sokoni Ujiji.Akamuona Zainabu, yuko na nguo za shule anakuja .

John akashangaa, sio kawaida ya Zainabu kuja kwake na nguo za shule, " Vipi Zainabu kulikoni asubuhi hii na nguo za shule?, umetoroka shule"?, Zainabu hakujibu, moja kwa moja akapitiliza chumbani kwa John huku akilia, John akamfuata ndani, " Zainabu una nini, umefiwa"?. Zainabu hakujibu ,akaendelea kulia."

Kuna nini'? , John akamuuliza.
" Nina mimba mpenzi, nina mimba yako".
" Unasemaje"?, John akamuuliza huku akionekana amechanganyikiwa . "Nimesema nina mimba yako". Zainabu akamuambia kwa msisitizo.. " Hapana Zainabu, utakuwa umekosea,hiyo mimba sio yangu, tena unikome sikujui", unajua adhabu ya kumpa mimba mwanafunzi"? unataka nifungwe kifungo cha maisha jela"?, we mtoto tokaa,sikujui mimi na usinijue"!. Zainabu akaduwaa,ingawa alitegemea hili, " Leo unanikana mpenzi"? Zainabu akamuuliza.

"Nimesema tokaa,sikujui tokaa,unikome,"! John akaongea kwa ukali,huku hasira zikimpanda. Zainabu akamuangalia John usoni, akajua John anamaanisha anachokisema. " Niende wapi sasa"?,
"Unaniuliza mimi kweni huna kwenu"? nenda popote mimi hainihusu". Zainabu kwa hasira akasimama na kuondoka.

Baada ya Zainabu kuondoka, John akajitupa juu ya kitanda akifikiria kitu cha kufanya, alikuwa anasikia tu habari za jela, lakini sasa jela inamuita, Akamfikiria baba yake Zainabu alivyo mkorofi, na ni balozi wa nyumba kumi, "Baba Zainabu hawezi kuniacha, atahakikisha nafungwa,tena kifungo cha maisha", John akafikiria. Nifanye nini sasa? Akajiuliza.

Akamkumbuka rafiki yake Mrundi, aitwae Hizzmana, ambae kila siku anamsihi aende Burundi kumtembelea, " Labda huu ndio wakati muafaka wa kumtembelea, na sio kumtembelea kwa muda,ni kumtembelea moja kwa moja, Akaweka nguo zake zote kwenye begi, akampigia simu rafiki yake wanaevua wote samaki. " Hallo, Kabwe, naomba uje uchukue vitu vyangu hapa kwangu ukae navyo, nimepata safari ya ghafla ,sitakuwepo kwa miezi mingi, narudisha chumba" funguo utaikuta kwa mwenye nyumba", John akasema, alivyokubaliana na rafiki yake akakata simu, Akaelekea kwa mwenye nyumba na kumuambia anachia chumba, amepata kazi Mwanza, kodi iliyobaki haiitaji, atafute mpangaji mwingine, kodi ilibaki miezi minne, mwenye nyumba akafurahi,akajua atapata kodi nyingine kabla ya muda kuisha, wakaagana, John akabeba begi lake na kuelekea Burundi kwa rafiki yake, hana haja ya pasipoti, maana njia zote za panya anazijua. Na huo ndio ukawa mwisho wake kuonekana Kigoma.

Zainabu alivyotoka kwa John akatembea kwa nusu saa hajui aende wapi. Akafikiria, niende nyumbani? Hapana, baba ataniua, niende wapi sasa? Akamkumbuka shangazi yake alieko Kigoma Mjini, shangazi yake anampenda sana Zainabu,ingawa haelewani na mama yake. Nitapata wapi nauli? . Zainabu akajiuliza.

Akakumbuka mama yake anafichaga pesa zake za akiba kwenye chaga za kitanda, na akajua muda huo mama yake atakuwa shambani, baba hayuko yuko ziwani anavua samaki. Zainabu haraka akaelekea nyumbani, akakuta mlango umefungwa. Anajua funguo mama yake anaweka juu kwenye upenyo wa mlango wa jikoni.

Zainabu akaelekea jikoni, akapanda juu ya mlango,akaingiza mkono kwenye upenyo na kutoa ufunguo, Akafungua mlango na kuingia ndani. Alivyofika ndani akavua nguo za shule na kuvaa nguo za nyumbani. Akachukua begi lake akaweka nguo zake zote pamoja na viatu,na kila kitu alichokuwa nacho ,akaweka kwenye begi akaridhika hamna kitu alichosahau, akaelekea chumbani kwa mama yake, akasogeza godoro na kuangalia kwenye chaga, akaona pesa za mama yake, zilikuwa zimejaa vumbi, Zainabu akazihesabu, kulikuwa ana elfu hamsini na tano.

Akachomoa elfu arobaini akaweka mfukoni, akaacha zilizobaki, akarudishia godoro na shuka na kuelekea chumbani kwake, akabeba begi lake na kuanza kuondoka,akasita ,akamkumbuka mama yake. Akajua mama yake atamtafuta sana asipomuona, akachukua kalamu na karatasi, kisha akaandika:

Wazazi wangu wapenzi.
Mimi mtoto wenu wa pekee Zainabu, nimeamua kuondoka nyumbani,pamoja na kuacha shule,huu ni uamuzi wangu binafsi,nimefanya kosa ambalo siwezi kuwaeleza,ni kosa litakalonipa aibu mimi,pamoja na nyie hapa kijijini, siwezi kuivumilia hiyo aibu, naomba msinitafute.
Nawatakia maisha mema.

Mimi mtoto wenu
Zainabu.


Alivyomaliza akaiweka barua juu ya meza, akabeba begi lake na kuondoka, alivyofika sebuleni akaangalia juu ya ukuta, Akaiona picha ya wazazi wake iko kwenye fremu kubwa imetungikwa ukutani, akaiangalia kwa muda. Na hiyo ndio ikawa mara ya mwisho kuwaona wazazi wake.

Zainabu akaelekea stand ya Ujiji, alipofika stand, akapanda basi la kuelekea Kigoma Mjini, alipofika Kigoma Mjini akaelekea nyumbani kwa shangazi yake.Shangazi yake alikuwa ndani anajiandaa kutoka,maana anafanya biashara ya mama ntilie. " Hodi", Karibu. Shangazi yake akajibu, kisha akafungua mlango, " Zainabu? Vipi ingia ndani,karibu sana mwanangu". " Asante," Zaunabu akaingia ndani, Shangazi akampokea begi na kuliweka kwenye kabati, Shangazi yake ameachika anaishi mwenyewe, " Vipi Zainabu,kulikoni, mmefunga shule"? Shangazi akamuuliza.Akamuangalia Zainabu usoni, akagundua alikuwa analia."Hapana shangazi hatujafunga shule,bali nina matatizo". Zainabu akamjibu, kisha akamueleza ukweli.Shangazi yake baada ya kusikia alichoelezwa na Zainabu, akavuta pumzi ndefu, kisha akatafakari kwa muda, kama wazazi wa Zainabu wakigundua mtoto wao anaishi nae,watamletea matatizo, wanaweza kumshtaki kwa kumtorosha mtoto wao. "Sasa wazazi wako wakigundua uko kwangu ,si wataniletea matatizo, si unajua mimi na mama yako hatuelewani"?. Shangazi akamuuliza." Niwewaachia barua", Zainabu akajibu, alikuwa amesahau kumwambia Shangazi yake kuhusu barua."Umewaandikia barua"?. "Ndio shangazi,nimewaeleza mimi naondoka ,na ni uamuzi wangu binafsi". Zainabu akamueleza. Na hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa.

•••••••••••••••••••••
Baada ya miaka mitatu, bado Zainabu alikuwa Kigoma Mjini, lakini muda huo shangazi yake alikuwa hakai nae, shangazi yake alipata mchumba, akahama na kwenda kuishi nae, Zainabu akabaki na mtoto wake mwenyewe, lakini alikuwa anafanya kazi kwenye mgahawa wa kuuza chakula wa shangazi yake. Mtoto wa Zainabu, Nyasule alishatimiza umri wa miaka mitatu na alishaanza kuchangamka. Zainabu siku moja usiku, alifikiria sana, aliwaza kuhusu maisha yake na ya binti wake Nyasule ya baadae. Hakuona dalili yoyote ya maisha yake kuwa bora, alitamani siku moja na yeye awe na nyumba yake, nguo nzuri, na kuishi maisha bora kwa ujumla, lakini kwa kazi ya umama ntilie anayofanya ,isingempa kitu anachotaka, alikuwa anasikia habari za Dar es Salaam kuwa ni jiji kubwa, litakaloweza kumpa maisha anayohitaji.

itaendelea.......................................
 
Sehemu ya 2:

Kwa muda wa wiki mbili Zainabu alikuwa na mawazo sana,mpaka shangazi yake akapata wasi wasi.
"Una nini Zainabu, mbona siku hizi unaonekana na mawazo sana"? Shangazi yake alimuuliza.
"Hapana shangazi,niko sawa" ,Zainabu alijibu. Lakini ki ukweli hakuwa sawa, alikuwa na hamu sana ya kuelekea jiji la Dar es Salaaam, alikuwa amepata habari nyingi kuhusu Dar kutoka kwa wateja na rafiki zake. Jiji kubwa,lenye magari mengi,magorofa marefu,nyumba za kisasa, si vibaya na mimi nikajaribu bahati yangu huko, huwezi jua, ninaweza kutoboa. Zainabu aliwaza. Zainabu muda huo ,alikuwa na akiba ya pesa ya shilingi laki mbili. Akaona hizo pesa zitamtosha kumfikisha Dar es Salaam na kubaki na akiba kidogo ya kumsukuma siku mbili tatu,kabla hajapata kazi ya kufanya.
" Nisipopata kazi, hii laki mbili nitauza hata mihogo ya kukaanga", inatosha". Zainabu akawaza. Akakata shauri aelekee Dar es Salaam.
Kesho yake asubuhi akapanga amueleze shangaxi yake kuwa anaenda Dar kutafuta maisha. Alipofika mgahawani akafanya kazi kama kawaida, ilipofika jioni, baada ya wateja kuisha, wakati wanaandaa chakula cha jioni cha wateja, Zainabu akaona ndio muda mzuri wa kumueleza shangazi yake juu ya huo mpango wake.
"Shangazi yangu, nina mazungumzo na wewe". Zainabu akamuambia . "Mazungumzo gani, umepata mchumba ?"Shangazi akauliza.
"Hapana shangazi, nataka kwenda Dar es Salaam". Shangazi akashangaa.
" We mtoto wewe, unataka kwenda Dar kufanya nini? utakuweza huko? hapa Kigoma tu kwenye magari mawili,kuvuka bara bara tabu,huko Dar kwenye magari kila kona utaweza kuvuka barabara"? Shangazi yake alimwambia huku anacheka, kulikuwa na binti mwingine wa kazi wa shangazi yake nae akacheka.
"Shangazi acha utani, mimi kweli nataka kwenda Dar kutafuta maisha" , Zainabu alimuambia.
" Haya utafikia wapi, kwanza una nauli"? Shangazi akamuuliza.
" Ndio shangazi nina shilingi laki mbili za kunisaidia nauli na mambo mengine" Zainabu akajibu.
" Laki mbili? hizo hazitoshi Dar kila kitu ni pesa, hizo ni kidogo sana", Shangazi akasema..
"Najua ni kidogo, lakini nitajibana bana zinisukume siku mbili tatu wakati natafuta kazi, nikikosa nitauza mihogo ya kukaanga nipate pesa", Zainabu akamjibu, kisha akaendelea, " Nikifika dar nitatafuta chumba cha kupanga cha bei rahisi , nitapanga, nitanunua godoro la kulalia,itakayobaki nitanunua mihogo, na kukaanga na kuuza".
Shangazi akakumbuka ana godoro dogo liko chumbani kwake halitumii. "Ukinunua godoro haitatosha hiyo hela, godoro nitakupa utaenda nalo kama kweli una nia ya kwenda huko. "Nitashukuru shangazi" Zainabu akasema. Shangazi yake akafikiria hata yeye alikuwa na ndoto za kwenda dar, lakini akatokea mvuvi na viela vyake vya dagaa akamrubuni na kuolewa, hawakudumu sana wakaachana,akaamua kuwa mama ntilie.
" Haya, unataka kwenda lini huko Dar"? Shangazi akamuuliza.
" Kesho kutwa shangazi, kesho nitajiandaa kwa kufua nguo na kumuandaa mtoto, na kukata tiketi ya basi, keshokutwa naondoka" Zainabu akajibu.
" Sawa, kukikushinda urudi nyumbani, mimi ni ndugu yako siwezi kukutupa" Shangazi akamuambiwa.
"Sawa shangazi, Zainabu akajibu. Na hivi ndivyo Zainabu alivyoondoka Kigoma. Hakukanyaga tena Kigoma..

••••••••••••••••••••••••••••••••

Zainabu akafika Dar es Salaam muda wa jioni saa kumi na moja na treni akitokea Kigoma, akakaa station kidogo, hajui aelekee wapi. Nitaenda wapi sasa? Alijiuliza. Akaondoka Station na kuelekea barabani. Alipofika barabarani akapata mshtuko, akaona watu wengi na magari mengi yanaelekea pande zote, milio ya honi kutoka kwenye dala dala na bajaji. Akajiuliza hawa watu wanaenda wapi? Lakini akakumbuka aliambiwa Dar kuna watu na magari mengi, akajiuliza aelekee kushoto au kulia? Akaamua kuelekea kulia, akatembea kama nusu saa akachoka, mtoto wake Nyasule yuko mgongoni amelala, amebeba begi moja kichwani, juu ya begi ameweka godoro na kulifunga na kamba na begi lingine dogo mkononi. Akatafuta sehemu kwenye mgahawa akaingia ndani, akaweka mabegi yake chini na kukaa kwwnye kiti, akamtoa Nyasule mgongoni na kumpakata, muhudumu akaja, akaagiza soda. akaomba glasi akapewa, akammiminia Nyasule soda kwenye glasi, Nyasule alionekana kuwa mchovu sana kutokana na safari ya kigoma.Zainabu akaona ajaribu bahati yake. Akamuita yule muhudumu wa kike, muhudumu akaja, Zainabu akamwambia. "Samahani dada, mimi ni mgeni hapa mjini , natafuta kazi," " Unatafuta kazi"? labda uongee na bosi yuko jikoni anapika, ngoja nikuitie".
Yule muhudumu akaenda jikoni kwa bosi wake, na alitaka sana wapate mfanyakazi mwingine, maana wateja ni wengi, na yeye ni mvivu anajijua. Akafika jikoni akamwambia bosi wake kuna binti anataka kazi, anataka kuongea na wewe, nadhani ni bora tuongeze mfanyakazi mwingine, maana hapa naona wateja ni wengi". Yule muhudumu jina lake Prisca alimuambia bosi wake.
" Nakujua wewe mvivu unataka tupate mfanyakazi mwingine ili umtegee, kama ni mtu wa Morogoro kama wewe simtaki", bosi wake akamuambia, kisha akasimama na kuelekea kwa Zainabu. Bosi wake Prisca alikuwa anaitwa Mama Mariamu, anaishi Kawe na watoto wake watatu, pamoja na mume wake. Alivyofika kwa Zainabu, akakaa kwenye kiti mbele yake. Kwanza alipata mshtuko baada ya kumuona binti mdogo kama Zainabu ana mtoto.
"Vipi binti, nasikia unashida na mimi", Mama Mariamu akasema.
" Ni kweli mama , ninashida na kazi," Zainabu akajibu.
" Umetoka wap"?
" Kigoma".
" Umekuja Dar kufanya nini"?
" Nimekuja kutafuta kazi".
" Na huyo mtoto ni wa kwako"?
" Ndio mama".
Mama Mariamu akamuonea huruma sana Zainabu, binti mgeni, asiekuwa na ndugu Dar ,tena ana mtoto mdogo. Wakati huo Nyasule alikuwa ameanza kuchangamka baada ya kunywa soda.
" Chikamoo changazi", Nyasule alimuamkia mama Mariam kwa lafudhi ya kiha. " Marahaba,", unaitwa nani mtoto mzuri". "Naitwa Nyachule".
Mama Mariamu akaamua kumsaidia Zainabu. Akamuita Prisca, na kumuomba akakae na Zainabu mpaka atakapopata chumba chake,Prisca alikuwa anaishi mwenyewe Gongo la Mboto, Prisca akakubali. Na hivi ndivyo Zainabu alivyoyaanza maisha mapya ya jiji la Dar es Salaam.

Mama Mariamu alimpenda sana Zainabu kutokana na uchapakazi wake, hakuwa mvivu kama Prisca, alikuwa anajua kupika, na kufanya kazi zote bila kulalamika, na kwa kuwa alikuwa na uzoefu na kazi za mama ntilie kutoka kwa shangazi yake Kigoma, alifanya kazi kwa umahiri mkubwa, wateja walimzoea kwa muda mfupi, Mama Mariamu muda mwingi alikuwa anacheza na Nyasule, kazi nyingi alifanya Zainabu na Prisca, kipindi hicho Zainabu alishahama kwa Prisca, alipata chumba Tandika. Aliishi na mtoto wake Nyasule. Zainabu alikuwa analipwa shilingi elfu nne kwa siku, pamoja na chakula . Alikuwa anaingia kazini alfajiri saa kumi na mbili na nusu, kutoka saa mbili usiku, alikuwa anakula huko huko kazini, nyumbani ni kulala tu, aliishi mbali kidogo na kazini, ikabidi awe anapanda dala dala, kwa siku kwenda na kurudi nauli anatumia elfu moja, anabakua na elfu tatu. Kwa muda wa mwaka mmoja alimudu kununua kitanda, pamoja na kuchonga meza, na nyingine kununulia nguo zake na za mtoto wake.Akalinganisha na maisha aliyokuwa anaishi kwa shangazi yake, akaona bora angebaki Kigoma kwa shangazi yake.Dar shida tupu, maji ya kununua, bado pesa ya luku kila mwezi elfu kumi, nauli ya dala dala, kuamka saa kumi usiku kila siku kujiandaa kwenda kazini, kurudi usiku umechoka, nafanya kazi kama punda, bora ningebaki Kigoma, Zainabu aliwaza.Nyumba aliyopanga ilikuwa na vyumba sita, vyumba vingine viwili waliishi mabinti kama yeye ,walikuwa hawana watoto,wala hawajaolewa, waliishi wenyewe, na vyumba viwili waliishi familia ya mke na mume, walipanga vyumba viwili, kimoja walikaa wenyewe, mume na mke, kingine walikaa watoto wao wawili wadogo, na mfanyakazi.chumba kilichobaki alikaa kijana mmoja kondakta wa dala dala.Maisha ya wale mabinti wawili waliokuwa hawajalewa yalimshangaza Zainabu, walikuwa wanaondoka usiku na kurudi asubuhi alfajiri, walikuwa na maisha mazuri, kwenye vyumba vyao kuna tv kubwa flat screen, friji, kabati kubwa , makochi sofa,na muziki mkubwa, chini kapet zuri.
" Nafuu hawa jirani zangu wana maisha mazuri kidogo, mimi mwaka mzima nimefanikiwa kununua kitanda tu, tena kwa shida", Zainabu aliwaza.
" Iko siku nitawauliza wanafanya wapi kazi na mimi wanitafutie kazi huko".

itaendelea........................................
 
Mkianzaga mnakua na speed kweli kubandika episodes uzi ukishapendwa sasa ndio dharula za ndugu zenu kumeza shoka zinaanza.
 
Nipo dawati la Tano kutoka mbele upande wa kulia nafuatilia kinachoendelea
 
Sehemu ya 3:

Ilikuwa siku ya jumapili, siku ambayo Zainabu haendi kazini, muda huo wa kupumzika anautumia kwa kufua, na kufanya usafi chimbani kwake, alikuwa nje anafua, wale mabinti jirani zake walikuwa nje kibarazani wanachat na simu zao kubwa za kisasa, huku wanapiga stori, Zainabu akaona ndio muda wa kuwauliza wanakofanyia kazi wamtafutie na yeye kazi huko.
" Shoga zangu kwa nini atupeani michongo"? nyie mna maisha mazuri , tv ,sofa, friji ,na ni mabinti kama mimi, mimi mwenzenu sina chochote zaidi ya kitanda tu, tena nimechonga kwa shida, nitafutieni kazi huko mnakofanya jamani shoga zangu".
Wale mabinti wakaangaliana, kisha wakaangua kicheko cha nguvu.
"Haloo, shoga etu tulikuwa tunakushangaa binti mrembo,mwenye shepu yake ,tako hiloo unaenda kuungua na moto wa mikaa kwenye migahawa una akili kweli" ? hili jiji shoga angu akili kichwani".
" Mbona kashfa tena shoga zangu" , si mniambie vizuri niwaelewe"!. Wale mabinti wakaangaliana, kisha wakacheka tena.
"Zainabu hebu niangalie mimi teddy", sina shepu kama wewe,sina tako kama lako, lakini nina maisha mazuri kukushinda, changamka mama" Teddy ndio jina lake, mmoja wa wale mabinti akamuambia.
"Sasa shepu na tako langu linahusiana nini na kazi "? Zainabu akawauliza kwa mshangao, akina teddy wakacheka na kugongeana mikono,kisha teddy akamuambia, "Ukimaliza kufua uje chumbani kwangu nikupe dili", kisha wakanyanyuka wale mabinti, na kuelekea chumbani kwa Teddy.

Zainabu akafua haraka haraka nguo zake na za Nyasule na kuzianika kwenye kamba, akasafisha chumba, na kuelekea chumbani kwa Teddy, mtoto wake Nyasule alikuwa anacheza na watoto wa jirani yake chumba cha pili, Zainabu akaingia chumbani kwa Teddy.
"Hodi mpaka ndani", karibu Zai,karibu ingia", Zainabu akaingia ndani na kukaa kwenye sofa.
"Unatumia kinywaji gani" ? Akaulizwa na Grace.
" fanta".
" Hapa hatuna soda, wewe ukinywa soda na mtoto wako Nyasule atakunywa nini? mpe redd's huyu" Teddy akajibu.
" Mi sinywi pombe", Zainabu akawaambia.
" Sio pombe hii, ni tamu kama fanta, onja kiddogo uone", Teddy akamuambia. Zainabu akaichukua ile pombe, huku mikono ikitetemeka,akaonja,akaonaa ina utamu, akanywa tena, kisha akaweka kopo la reddds chini, akina teddy wakaangaliana, kisha wakacheka na kugongeana mikono , wakajua Zai ameshaingia kwenye anga zao.
" Zainabu shoga etu, sisi tunaishi kwa kutegemea wanaume", Teddy akamuambia.
Zainabu akapata mshtuko, akamkumbuka mpenzi wake mvuvi John alivyomfukuza alipomwambia ana mimba, toka kipindi hicho hajawahi kuwa na mwanaume, na anawachukia sana wanaume. Na alishaapa hatakuja kumpenda tena mwanaume yoyote. Akajua wakina Teddy wanajiuza, ni machangudoa, lakini inakuwaje wanapata pesa nyingi hivyo? hilo likamshangaza, alivyomaliza ile redds akapewa nyingine, akanywa tatu, wakina teddy wakamueleza jinsi wanavyopata pesa kwa wanaume .
"Hamuogopi kupata mimba na ukimwi"? Zainabu akawauliza. Teddy akafungua kabati, kulikuwa na paketi za kondomu zimejaa kwenye maboksi.
" Tunatumia hizi" Teddy akanyoosha mkono kumuonesha Zainabu paketi za kondomu. Zainabu aliwaeleza na yeye historia ya maisha yake ,jinsi alivyopewa mimba na John na kufukuzwa shule. Akina Teddy wakampa pole, wakaendelea kupiga story, mara Zainabu akahisi kizunguzungu. Naona zile redds zimeanza kufanya kazi,Zainabu akawaza. Na akina Teddy wakawaza hivyo pia, akawaaga na kwenda chumbani kwake, alivyofika chumbani kwake akajitupa kitandani na kupitiwa na usingizi. Usingizi wa pombe.


Alikuja kushtuliwa na Nyasule aliekuwa anamtingisha kwa nguvu. Zainabu akazinduka usingizini, akamwangalia Nyasule pembeni yake aliekuwa anakunywa maziwa na kula chips na mishikaki, akakumbuka hakupika mchana
" Hizi chips Nyasule amezitoa wapi"? Teddy akaingia chumbani kwa Zainabu.
" Tulivyokuona umelala tukamnunulia Nyasule chips, tulijua haujapika, na chips zako hizo hapo kwenye mfuko", Zainabu akaangalia kwenye meza akaona mfuko. "Asante Teddy, nashukuru sana". " Usijali shoga angu tuko pamoja," Teddy akajibu na kuondoka.

Usiku ulipoingia Zainabu hakulala, akafikiria sana mazungumzo yake na akina Teddy, akafikiria jinsi walivyomwambia kuhusu majumba ya starehe, Club na Hotel wanazoenda , habari za kumbi za disco na starehe wanazofanya. Zainabu aliwaza sana. Kwani mimi nina kitu gani cha muhimu zaidi ya Nyasule? Kwanza Nyasule kashakuwa mkubwa. Tatizo toka apewe ujauzito na mvuvi John na kumkana, anachukia sana wanaume. Nitaanzaje kuwapenda tena wanaume? Alijiuliza. Kwanza sina haja ya kuwapenda, nitakachofanya ni kuwalia tu pesa zao, na ikiwezekana kuwaibia, Lakini vipi kuhusu mimba na ukimwi? Nitatumia kinga, kama wakina Teddy wanavyofanya, na sitakubali kamwe,milele kulala na mwanaume bila kinga. Akapitiwa na usingizi.

Jumatatu Zainabu akaenda kazini kama kawaida, kila inapofika jumapili ,lazima aende chumbani kwa Teddy na Grace kupiga stori, Habari zao ni zile zile jinsi wanavyostarehe na wanaume kwenye sehemu mbali mbali za starehe, habari za maclub, casino, makumbi ya muziki ndio zilikuwa habari zao. Zainabu akaanza kuvutiwa na hizi habari, na wakawa wanakunywa pombe huku wakiendelea na stori , Zainabu anakunywa redds, wakina Teddy wanakunywa bia castlle lite, siku moja akajaribu kunywa bia, akaona chungu, wakina Teddy wakamwambia aendelee kunywa atazoea, Akanywa chupa nzima, hivyo hivyo kidogo kidogo mpaka akazoea.Zainabu akawa mlevi, kila jumapili lazima anywe pombe na akina Teddy, Akaona sasa ni muda wa kwenda kwenye viwanja vya akina Teddy. Jumatatu ilipofika akaenda kazini mgahawani kama kawaida akiwa mnyonge na mwenye mawazo.
"" Una shida gani Zainabu, mbona unaonekana mnyonge sana"? Mama Mariamu amamuuliza.
"Shangazi yangu anaumwa Kigoma, nataka kwenda kumuona", Zainabu akamjibu, alijua anadanganya, shangazi yake hakuwa mgonjwa, wala hakuwa na mpango wa kwenda Kigoma, alitaka kupata ruhusa ya kwenda kwenye sehemu za starehe na akina Teddy.
"Pole sana", kwa hiyo unataka kwenda Kigoma lini"? " Keshokutwa mama, shangazi hana mtu wa kumuhudumia , inabidi niwahi kumuangalia", Zainabu akajibu.
" Sasa una pesa za nauli"? Mama Mariamu amamuuliza" , Ndiyo mama, ninazo", Zainabu akajibu.
Ilipofika usiku, wakati wanafunga mgahawa, Mama Mariam akampa Zainabu elfu ishirini ya kumsaidia kumnunulia dawa shangazi yake , kisha wakaagana.
"Haya Zainabu, safari njema, usichelewe kurudi, shangazi yako akipata nafuu urudi, hata kama huna nauli ,piga simu nitakutumia", Mama Mariamu alimuambia.
" Sawa mama" Zainabu akajibu.
Na huo ndio ukawa mwisho wa Zainabu kukanyaga mgahawani kwa Mama Mariamu.

•••••••••••••••••••••••••••••••

Baada ya miaka mitatu, Nyasule, mtoto wa Zainabu alikuwa kashaanza kusoma, Alikuwa anasoma Shule ya Msingi Jitegemee, kipindi hicho Zainabu alishahama Tandika, alihamia Sinza, kwenye nyumba kubwa ya vyumba viwili vya kulala, jiko, choo ndani na sebule, Maisha yake yalikuwa mazuri, ndani kuna kila kitu tv flat screen kubwa, sofa zuri, friji ,jiko la gesi na mfanyakazi wa ndani,n.k. Zainabu hakuna jumba la starehe,bar, hoteli wala casino asiyoijua, alikuwa amekubuhu kwenye ukahaba, kwake pesa mbele, mambo mengine baadae ,alitembea na wanaume wa kila aina, na wengine wakipitiwa na usingizi kwa pombe, au kuwapa madawa anawaibia. Zainabu alikuwa hashikiki, hata mashoga zake akina Teddy walikuwa hawampati, Shepu, tako,na sura yake kama ya kinyarwanda iliwachanganya wanaume, wakawa anawapanga kama mafungu ya nyanya. Kuna waliomlilia kutaka kumuoa, aliwatukana na kuwafukuza kama mbwa, Zainabu alikuwa anachuki sana na wanaume, jeraha la moyo alilopewa na mvuvi John lilikuwa bado halijapona. Kwa Zainabu , mwanaume ni chombo cha kumpatia pesa,basi, hakuwa na mapenzi na mwanaume yoyote yule.

Siku ya kwanza kwenda na akina Teddy kwenye viwanja vyao vya starehe ilikuwa ni jumatano, siku mbili baada ya kuagana na mama Mariamu jumatatu usiku. Siku ya jumanne aliitumia kwenda saluni, alitumia elfu ishirini aliyopewa na mama Mariamu kwa ajili ya kumnunulia shangazi yake dawa kwenda saluni kusuka rasta, kesho yake jumatano akapewa vipodozi vya kujipodoa na akina Teddy, ilipofika saa moja usiku wakaelekea kumbi mbali mbali za starehe mijini, wanaume walimgombea Zainabu, walizuzuka na uzuri wake, akina Teddy wakamchagulia mwanaume asiekuwa na matata, mteja wao wa kawaida, alikuwa ni mwarabu, mfanyabiashara wa nguo kariakoo, Alivutiwa sana na uzuri wa Zainabu, asubuhi akampa shilingi laki moja. Zainabu hakuamini,...laki moja kwa siku moja! Tena baada ya kupewa pombe,na chakula cha maana chips kuku, arudi kwa mama Mariamu kuungua na moto wa mkaa na kula ugali dagaa na kisha kupewa elfu nne kwa siku ana kichaa!
Zainabu akawa changudoa wa mjini, tena shangingi haswa.

••••••••••••••••••••••••••••••••••

Nyasule akamaliza darasa la saba, akachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kwenye shule ya wasichana Jangwani. Zainabu alifurahi sana, pamoja na uchangudoa wake wote, Zainabu alikuwa anampenda sana binti yake Nyasule, Nyasule kwake ndio kitu pekee cha thamani hapa duniani alichokuwa nacho. Nyasule hakuwahi kuwaona ndugu zake, zaidi ya kuongea na shangazi yake alioko Kigoma kwenye simu, kila siku shangazi yake anamsihi Zainabu aende kuwaona Kigoma, Zainabu anatoa ahadi tu bila kutekeleza, kila akimkumbuka mvuvi John alichomfanyia, anaishiwa hamu ya kwenda Kigoma,. Nyasule kuna wakati anamuuliza mama yake kuhusu baba yake, Zainabu anabaki kimya, au anabadili mada. Mwisho Nyasule akaamua kujikalia kimya.

Ilikuwa ni siku ya jumapili, Zainabu kama kawaida alielekea kwenye viwanja vyake vya starehe, Siku hiyo usiku polisi waliendesha msako wa kuwasaka machangudoa kwenye sehemu mbali mbali za starehe. Zainabu akakamatwa, katika purukushani za kukamatwa akapoteza simu, akaingizwa kwenye karandinga la polisi na kupelekwa rumande, kesho yake jumatatu Nyasule akaelekea shule asubuhi, ni kawaida kwa mama yake kutokuwepo nyumbani asubuhi, siku nyingine mpaka saa tano asubuhi au saa sita mchana ndio anarudi, Nyasule hakushangaa. akamuaga mfanyakazi wao wa ndani na kuelekea shuleni, Akarudi jioni mama yake alikuwa bado hajarudi, na sio kawaida yake, akamuambia dada wa kazi ampigie simu mama yake, " "Nimemtafuta toka asubuhi kwenye simu sijampata", Dada wa kazi aitwae Adela akamjibu .
" Mmh sasa turafanyaje "? Nyasule akamuuliza.
"Sijui, tumsubiri tu hatuna na la kufanya". Adela akajibu.
"Sasa kuna ela ya matumizi" Nyasule akamuuliza Adela.
."Vyakula vya wiki nzima vipo", na aliniachia elfu kumi", nimetumia elfu nne kununulia mboga, bado elfu sita", Adela akamjibu .
"Sawa,basi tumsubiri".Nyasule akasema.
Zainabu akajua akina Nyasule watakuwa wanamtafuta , ilipofika jumanne wakapelekwa mahakamani, baada ya kusomewa mashtaka kesi ikaahirishwa, Wakashindwa masharti ya dhamana, wakarudishwa rumande, Zainabu akawa na wasi wasi sana juu ya akina Nyasule na mfanyakazi wa ndani Adela, watakuwa wanamtafuta, akamuona rafiki yake mmoja ameenda kuwatembelea rumande, akamuomba aende nyumbani kwake akawaambie wasiwe na wasi wasi nae, amepata safari ya ghafla atarudi, wasimtafute, pesa za matumizi waangalie chumbani kwake kwenye droo ya kabati watazikuta, watumie.

itaendelea...................................
 
Sehemu ya 4:


Rafiki yake Zainabu akaenda nyumbani kwa Zainabu, akagonga mlango.
" Hodiii,"
"Karibu" , Adela, mfanyakazi wa ndani wa Zainabu akajibu.
"Asante", yule dada akaingia ndani. Akamuulizia Nyasule,Adela akamuambia Nyasule ameenda shule. Yule dada akamuambia Zainabu amepata safari ya ghafla, wasiwe na wasi wasi atarudi muda si mrefu.
" Kwani ameenda wapi,? na mbona simu yake haipatikani" Adela akamuuliza. "Amepoteza simu ndio maana hamumpati, hajaniambia alikoenda." Yule dada akaaga na kuondoka. Nyasule baada ya kurudi kutoka shule, Adela akamuambia alivyoambiwa na yule dada rafiki wa mama yake, Nyasule hakujibu kitu alichukia mama yake kuondoka bila kuaga.


Ilikuwa ni ijumaa usiku, Nyasule alijisikia vibaya ghafla usiku baada ya kula chakula cha usiku, akaanza kutapika, akahisi mwili umepata joto sana, na kuhisi kizunguzungu, walikuwa wenyewe na dada wa kazi Adela, Nyasule akadondoka chini,akazimia, Adela akakimbia kwa jirani yao na kuwapa taarifa, jirani yao akaita teksi na kumpeleka Nyasule hospitali akiwa hajitambui. Walivyomfikisha hospitali akapelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, daktari akaja,akampima, akakutwa na malaria kali, akalazwa na kutundikiwa dripu, Adela akakaa na Nyasule hospitali mpaka asubuhi, mama yake bado alikuwa hajarudi. Asubuhi ilikuwa ni jumamosi, Adela akarudi nyumbani kwa ajili ya kumuandalia mgonjwa chai, wakati yuko njiani, akakutana na rafiki yake Nyasule anaeitwa Maria, ni rafiki mkubwa wa Nyasule, akamtaarifu Maria kuhusu kulazwa kwa Nyasule.
"Rafiki yangu kalazwa"?, ndio nilikuwa nakuja kumuona, ngoja nielekee hospitali kumuona" , Maria akasema.
"Mimi naelekea nyumbani kumuandalia chai, nitakuja muda si mrefu" Adela akajibu.
Maria akaenda hospitali kumuona rafiki yake, alikuwa bado hajitambui, siku ya tatu ilikuwa ni jumatatu, Nyasule alikuwa bado hospitali, hali yake ilibadilika na kuanza kuwa nzuri, alipata fahamu sasa, bado mama yake hajarudi, alikuwa anahudumiwa na majirani, dada wa kazi Adela,pamoja na rafiki zake wapenzi, Maria na Monica, hawa ni marafiki wakubwa wa Nyasule, wanasoma wote darasa moja, wanapendana sana mpaka shuleni wanawaita mapacha watatu,kila sehemu wako pamoja kama mapacha. Wakaenda kutoa taarifa shule juu ya ugonjwa wa Nyasule, Zainabu bado alikuwa rumande mpaka jumatano akafanikiwa kupata dhamana na kurudi nyumbani.

Zainabu alipofika nyumbani, akakuta nyumba imefungwa akagonga mlango akajua labda dada wa kazi Adela amelala.
"Adelaaa,Adelaa! akaita. "Adela hayupo, ameenda hospitali",mama wa jirani akamuambia.
Zainabu akashtuka na kumgeukia yule jirani yake.
"Hospitali"? kuna nini"?
" Ina maana hujui mwanao Nyasule amelazwa toka ijumaa usiku"?
Zainabu akahisi kama kisu kimemchoma moyoni, akashtuka kidogo azimie, akamkimbilia yule mama mikono ikiwa kichwani.
"Niambie mama angu Nyasule amepatwa na nini,"? Zainabu aliongea huku analia kwa uchungu.
"Amelazwa Amana hospitali, alipata malaria ghafla ikab.........." Zainabu hakusubiri yule mama aendelee kuongea, haraka akakimbilia barabaran na kusimamisha boda boda huku akilia kwa kwikwi, "Nipeleke Amana hospitali haraka" tena ufanye haraka", Kabla yule boda boda hajajibu, Zainabu alikuwa ameshapanda, yule boda boda alivyomuona Zainabu kwenye hali ile, hakuongea, aliwasha boda boda kwa mwendo wa kasi na kuelekea Amana hospitali, ndani ya dakika tano walikuwa wamefika, akamlipa yule boda boda na kukimbia mapokezi.
"Nataka kumuona mwanangu Nyasule", Zainabu aliongea huku analia kwa uchungu.
" Dada hebu tuliza presha, Nyasule anaendelea vizuri , amepata fahamu leo siku ya tatu", nesi alimuambia Zainabu. " "Ina maana alipoteza fahamu"?, Zainabu aliuliza huku akizidisha kulia.
"Ndio aliletwa akiwa hajitambui". Zainabu alilia kwa sauti mpaka watu wote pale hospitali wakawa wanamshangaa wakajjua labda mgonjwa wake amefariki.
" Nipeleke kwa Nyasule wangu, Nyasule wangu yuko wapi nesi"! .
"Nenda wodi namba sita mkono wako wa kulia , yule nesi alimuelekeza Zainabu alipolazwa Nyasule.
Zainabu akakimbilia wodini.Akaingia ndani ya wodi, Akamuona Adela anampa uji Nyasule, huku bado akiwa na dripu mkononi, Zainabu akamkimbilia mtoto wake huku analia, akamkumbatia mwanae, Nyasule nae alipomuona mama yake akaanza kulia huku amemkumbatia
mama yake, Zainabu alilia sana kwa uchungu.
" Nisamehe mwanangu, " niko chini ya miguu yako, "Nyasule wangu nisamehe,nimekosa "Nisamehe, " ."".tafadhali nisamehe, "nimekosa sitakuacha tena mwanangu,"" nisamehe," Zainabu alilia kwa uchungu sana. Baada ya siku mbili Nyasule aliruhusiwa, wakarudi nyumbani.
Na huo ndio ukawa mwisho wa Zainabu kufanya uchangudoa na kunywa pombe, akaachana na starehe zote na kukaa nyumbani na mwanae.

••••••••••••••••••••••••••••

Mwezi mmoja baadae Zainabu na Nyasule wakahama Sinza, Wakahamia Mbagala, wakapanga nyumba ndogo chumba na sebule, dada wa kazi Adela allirudi kwao na kupelekwa na wazazi wake chuo cha veta kusomea ufundi cherehani, Nyasule akabaki na mama yake. Walipohamia Mbagala, Zainabu akauza baadhi ya vitu vya ndani, akachanganya na akiba yake kidogo, akafungua genge la kuuza nyanya, na mboga nyingine mbele ya nyumba waliyopanga, Akaishi na mwanae kwa amani na furaha, Nyasule akitoka shule, anaenda gengeni kumsaidia mama yake kuuza genge.

"Naomba nyanya za mia tano", sauti ya mama wa jirani ikamshtua Zainabu kutoka kwenye mawazo yake. "Unaonekana una mawazo sana leo mama Nyasule, vipi, kulikoni" yule jirani alimuuliza.
"Acha tu ,shogaangu" , Mama Nyasule akamjibu na kuendelea kumuhudumia.


••••••••••••••••••••••••••••••


Mark Chiluba ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mbili, mrefu, mtanashati, mwenye umbo kubwa lililojengeka kimazoezi, bosi wake Biggie anapenda kumuita " Chilly boy".

Wazazi wa Chilly boy ni wenyeji wa Nakonde, Zambia, waliondoka Nakonde Zambia, na kuhamia Uyole Mbeya kutafuta maisha wakati Chilly boy hajazaliwa. Chilly boy akazaliwa Uyole, Mbeya, akawa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, huku wazazi wake wakiwa raia wa Zambia. Chilly boy akapata elimu yake ya msingi kwenye shule ya Uyole Primary School, na Sekondari kwenye shule ya Sangu Sekondari . Alipomaliza kidato cha nne akarudi Uyole, baada ya muda wazazi wake wakarudi kijijini Zambia, Chilly boy hukupenda kurudi Zambia, akaelekea Msumbiji kwenye jimbo la Cabo Delgado kwenye machimbo ya madini ya rubi. Na huo ndio ukawa mwisho wa kuonana na wazazi wake.

Chilly boy alikaa mwaka mzima Msumbiji anatafuta rubi, siku moja usiku wakati wakiendelea kuchimba rubi, Chilly boy akiwa mgodini akasikia kelele watu wanakimbia hovyo huku wanapiga kelele, Chilly boy akapanda haraka juu, alivyofika juu akauliza kuna nini, akaambiwa magaidi wamevamia migodi wanachinja na kupiga watu risasi hovyo hovyo, Chilly boy alishasikiaga habari za hawa jamaa, hakushangaa, na yeye alikimbia na kwenda kujificha kichakani, akapanda juu ya mti akatulia. Akawaona wale magaidi wamefika mgodini kwao, wakamkamata rafiki yake mmoja anaitwa Dilunga, wakampigisha magoti kwa nguvu, huku wakimpiga awape madini, Dilunga hakuwa na madini, akatokea gaidi mmoja nyuma ya Dilunga, akanyanyua jambia na kumkata nalo Dilunga kichwa.Chilly boy akafumba macho, hakuamini kama kuna binadamu wenye roho mbaya kiasi hicho, wale magaidi wakawachukua na wachimbaji wengine sita waliowakamata,na kuwakata vichwa na majambia, kama walivyofanya kwa Dilunga, Chilly boy mwili ulikufa ganzi, akawa haamini anacho kiona, walivyomaliza kuwaua, wale magaidi wakapanda kwenye gari zao land rover ziko wazi nyuma, wakapiga risasi hewani huku wanashangilia na kuondoka na magari yao kwa kasi.

Chilly boy alivyoona wale magaidi wameondoka, akashuka juu ya mti huku akitetemeka, hakurudi tena mgodini, akaondoka na kuelekea mjini, alitembea usiku kucha, huku picha ya rafiki yake Dilunga, na wale wachimbaji wakikatwa vichwa ikimjia mara kwa mara.Chilly boy akajisachi mfukoni, alikuwa na chenga kadhaa za madini ya rubi, na passport, alishukuru kipindi anasoma sekondari Sangu Mbeya, likizo moja walienda na wazazi wake Zambia kuwatembelea ndugu zake, wakamkatia passport, toka kipindi hicho, anatembea na passport yake mfukoni muda wote.

Wakati yuko njiani anatembea,alikuwa anafikiria mahali pa kwenda, Nirudi Mbeya? Hapana, huko hakuna dili lolote la maana,labda nikawe mkulima, Niende Zambia kwa wazazi wangu? Kufanya nini? huko nako hapafai. Akakumbuka rafiki zake mgodini walivyokuwa wanakusifia sana Afrika Kusini, hasa rafiki yake aliechinjwa na magaidi, kila mara alikuwa anamuambia akipata madini kidogo atauza na kwenda kufanya biashara Afrika Kusini. Akakata shauri la kwenda Afrika Kusini. Nikifika kwenye mji niuze haya madini yangu ya rubi, najua nitapata pesa ya kuniwezesha kufika Afrika Kusini, Chilly boy aliwaza. Chilly boy akafika kwenye mji mdogo wa Montepuez, akaulizia wanunuzi wa madini ,akapata, jamaa mmoja ana ofisi yake ya kununua madini hapo mjini, akatoa madini wakafanya biashara, akapewa miti cash elfu kadhaa za kumuwezesha kufika Afrika Kusini, akamuuliza yule mshkaji anaeuza madini, kama ataweza kupata usafiri wa kwenda Afrika Kusini.
" Dah, ni kama una bahati vile, kuna jamaa zangu ni watanzania wenzako, wanaenda na gari la mizigo Afrika Kusini kuchukua mzigo huko, watapita hapa muda si mrefu, labda masaa kama mawili hivi mbele, wasubiri nitakuunganisha nao, mradi uwape hela" yule jamaa mnunuzi wa madini akamuambia Chilly boy.

Chillly boy akawasubiri. Baada ya masaa kama mawili hivi kupita, Chilly boy akaona gari ya mizigo Scania yenye kontena nyuma inapaki dukani kwa yule jamaa, Chilly boy alikuwa bara barani anakula miwa , Yule mshkaji akamuita, Chilly boy akaenda,
"Jamaa wamekubali, wape miti cash elfu tano wakupeleke, Chilly boy alikuwa na miti cash elfu thelasini alizouza madini yake, akatoa miti cash elfu tano na kuwakabidhi.
" Una passport"? Dereva akamuuliza, Alikuwepo dereva na utingo wake.
" Ndiyo ninayo". "Basi hautapata shida kuingia Afrika Kusini," yule dereva akamuambia Chilly boy.
Chilly boy akapanda kwenye gari, akasalimiana na utingo, kisha akaenda kwa nyuma ya siti ya dereva na utingo kuna kitanda kidogo, kwa jinsi alivyochoka kutembea porini usiku kucha siku mbili Chilly boy hakukaa hata dakika tano, akapitiwa na usingizi.
Na hivi ndivyo safari yake ya kwenda Afrika Kusini ilivyoanza.

itaendelea...........................................
 
Sehemu ya 5:

Chilly boy alilala kwenye gari kwa muda wa masaa nane, muda wote huo gari ilikuwa safarini, haikusimama, dereva akichoka,anamuachia utingo wake usukani, walivyofika Harare, Zimbabwe, Chilly boy akashtushwa na kelele za honi za magari, Chilly boy akaamka.
" Dah, mshkaji umelala mpaka tukahisi umekufa", utingo akamuambia.
"Ungejua nilivyochoka jamaa angu, we acha tu".
Walipofika Harare wakasimama kwa ajili ya kupata chakula, wakashuka kwenye gari ,wakaelekea hotelini kula, walivyomaliza kula wakarudi kwenye gari kuendelea na safari.
Walifika Berth Bridge, mpaka wa Zimbabwe na Afrika Kusini saa nane usiku, wakashuka na kuelekea uhamiaji, Dereva alikuwa anajuana na wale wafanyakazi wa uhamiaji, akamtambulisha Chilly boy kama utingo wake mpya, Chilly boy akatoa passport, akagongewa kukaa Afrika Kusini miezi mitatu, walivyomaliza wakarudi kwenye gari na kuendelea na safari.
"Karibu kwa Madiba mshkaji". Dereva wa lori alimuambia Chilly boy.Wakaingia Johanesburg jioni.
"Oyaa mwanangu tumefika Jo" burg , haya ,kazi ni kwako" , yule utingo alimuambia Chilly boy.
"Sisi tunaelekea kiwandani kuchukua mzigo, ni bora ushukie hapa" Dereva akamuambia Chilly boy.
" kila la heri, kisha akampa kadi yake yenye namba zake za simu,, Chilly boy hakuwa na simu.
"Kama ukipata tatizo nipigie simu, huwezi jua ninaweza kukusaidia" yule dereva akamuambia Chilly boy, Chilly boy akashuka kwenye gari, wakampungia mkono na kuendelea na safari.


Naam! Nimeshafika kwa Madiba, niende wapi sasa? Chilly boy alijiuliza.Chilly boy akaanza kuzunguka zunguka mjini, hajui pa kwenda, wakati anazunguka alishangaa jinsi jiji la Johanesburg lilivyo zuri, magorofa marefu, barabara pana, magari ya kisasa, wanawake wa kizulu wenye maumbo na matako makubwa. Huku kama Ulaya , Chilly boy aliwaza. Chilly boy akakumbuka ana pesa ya Msumbiji, miti cash, hana rand ya Afrika Kusini, amatafuta bureau de change ya pesa, akaiona, akaingia, akatoa miti cash alizokuwa nazo.
"where is your passport"?Chilly boy akaulizwa, akaonyesha passport, yule dada akaiangalia akamrudishia na kupokea miti cash, akampa rand, Chilly boy akaondoka.
Chilly boy akaona mgahawa, akaingia na kuagiza chakula ,alivyomaliza kula, akatoka na kuendelea kutembea tembea mitaani, akazunguka kama masaa mawili hivi, kigiza kikaanza kuingia ,ilikuwa ni mida ya saa moja kasoro, akaenda mwenye kituo cha basi akakaa, akakaa kama nusu saa hivi, anafikiria cha kufanya, giza limeshaingia, mara wakaja vijana wawili wamevaa kisharobaro wakakaa pembeni yake, wakaanza kuongea kiswahili.
" Mbona Davi hajaja mpaka sasa hivi"? Kijana mmoja akamuuliza mwenzake.
"Sijui, atakuwa bar anakunywa pombe,si unajua Davi anavyopenda pombe"? Yule mwenzake akamjibu.
Chilly boy hakuamini anachokisikia, kwa ile lafudhi alijua ni watanzania. Akawasalimia.
"Vipi washkaji, nyie ni watanzania"? Wale vijana wakashtuka, wakamuangalia Chilly boy.
" Ndio sisi ni wabongo, kwani vipi"? mmoja akamjibu. Chilly boy akajieleza. Wale washkaji walivyosikia ametoka Cabo Delgado Msumbiji kwenye madini, wakamsikiliza kwa makini, Chilly akawaeleza kuhusu magaidi walivyomchinja rafiki yake, Wakampa pole.
"Kama huna pa kulala twende ukalale geto", utajua huko huko cha kufanya". Chilly boy hakuwa na pingamizi.

Wakasubiri kidogo, mara Davi akaja,wakamtukana kwa kuwachelewesha, akawaomba msamaha, wakamtambulisha Davi.
" Davi, huyu mshkaji ni mbongo mwenzetu, ni mgeni hana ramani, ndio ameingia leo, sio mbaya tukimuingiza kwenye ngome yetu", Davi akamuangalia Chilly boy kwa muda, kisha akampa mkono. Karibu sana Afrika Kusini.

Wale wabongo wakaondoka na Chilly boy kuelekea wanapoishi., wakakatiza mitaa ya jiji la Johanesburg, kila wanapopita walikuwa wanasalimiana na jamaa zao.
"Inaonekana washkaji ni wenyeji sana huku", Chilly boy aliwaza. Baada ya kutembea umbali kidogo, wakaingia kwenye jengo moja la gorofa, wakapanda mpaka gorofa ya sita, kisha Davi akatoa funguo, akafungua mlango, wakaingia ndani, ndani kulikuwa na sebule, jiko ,choo na vyumba viwili, sebuleni kuna tv kubwa flat screen na masofa, jikoni kuna jiko la gesi, vyumbani kuna magodoro yamewekwa chini, hakukuwa na vitanda. Wakakaa sebuleni, wale washkaji wengine walikuwa ni Hamisi na Mohamed, wote kutoka Tanga, na Davi ametoka Mbeya.

Mohamed na Hamisi wakatoa bahasha na kuweka mezani, Davi nae akatoa bahasha na kuweka mezani, Davi akazichukua bahasha za Mohamed na Hamisi, akazifungua na kutoa pesa, rand za Afrika kusini, akazihesabu zile rand, akatoa na pesa zilizoko kwenye bahasha yake na kuhesabu.
" Leo biashara haikwenda vizuri, itabidi tutoke usiku tukamalize mzigo ,Biggie hatatuelewa", Davi akawaambia jamaa zake.
Hamisi akatoa sigara, akaiwasha, "Tuanzie Club Go-Go , pale kuna Tamasha la Muziki, tunaweza kumaliza mzigo wote pale, kuna wateja wangu wameniambia niwapelekee mzigo". Davi akatingisha kichwa kukubali.
" Hebu toeni mzigo tuhesabu, tujue umebaki kiasi gani", Davi akawaambia huku akiingiza mkono mfukoni, na kutoa paketi zilizokuwa na unga mweupe, akaanza kuzihesabu, zilikuwa sita, Hamisi akazihesabu zake,zilikuwa tisa, na za Mohamed zilikuwa saba.
" Sio nyingi sana, kama kuna tamasha la muziki leo, tutazimaliza",Davi akawaambia, kisha wakazichukua paketi zao za unga na kuzirudisha kwenye makoti yao.
" Jamaa angalia jikoni kwenye kabati kuna mkate, na kwenye chupa ya chai kuna maziwa, chukua ule, hapa hakuna mpikaji muda huu", Davi akamuambia Chilly boy.
Chilly boy akaenda kwenye kabati la jikoni, akatoa mkate, akamimina maziwa kwenye kikombe na kunywa, Muda huo Mohamed na Hamisi waliingia chumbani kulala, sebuleni alibaki Davi mwenyewe anaangalia t.v. Chilly boy alivyomaliza kula akarudi sebuleni, akakaa kwenye kochi, pembeni ya Davi.

Walikaa kimya kwa muda, kisha Davi akamuuliza Chilly boy.
" Kwa hiyo wewe Tanzania ulikuwa unakaa wapi"?.
"Mbeya, Uyole," Chilly akajibu.
"Kumbe home boy kabisa"? Mimi kwetu Tukuyu, lakini Mbeya mjini nimeishi, nilikuwa nakaa Kabwe".

Wakapiga stori za Mbeya kwa muda mrefu, wakikumbushana maeneo ya Mbeya, kisha Davi akamuuliza Chilly boy,
" Kwa hiyo una mpango gani hapa Sauzi"?.
" Mi sina mpango wowote, ndio nimekuja kutafuta mchongo", Chilly boy akamjibu.
" Kwa nini usijiunge na sisi, kwenye mishe zetu", Davi akamuuliza.
"Kwani nyie mnapiga mishe gani, maana mimi nimeona mnahesabu pesa, mara mnatoa dawa kwenye paketi, mnauza dawa za kienyeji"? Davi akamuangalia Chilly boy kwa mshangao, kisha akacheka.
" Acha masihara dogo, ina maana hujaelewa kitu mpaka sasa"? Chilly boy akafikiria kidogo halafu akasema,," Au ni madawa ya kulevya"?
" Kumbe unajua,? Ulikuwa unanichora tu?".
Kisha Davi akaanza kumueleza mambo yanavyokwenda huko Afrika Kusini. " "Hata mimi nilivyokuja Afrika Kusini sikujua kama nitadondokea kwenye kuuza madawa ya kulevya, nilikuwa na ndoto ya kupata kazi nzuri, ya kuniwezesha kuishi maisha mazuri na ya furaha,rafiki yangu, ambae yuko jela huku huku Afrika Kusini ndio alinipokea, na yeye alikuwa anauza unga, akakamatwa na polisi na kufungwa jela ,ndio aliniingiza kwenye hii biashara, akanitambulisha kwa bosi wake Biggie, ambae ndio bosi wangu mpaka sasa hivi, sikua na jinsi yoyote ya kufanya, ikabidi nikubali tu, na huku Afrika Kusini kama huna ujuzi ni ngumu sana kupata kazi ya maana.

Akamueleza jinsi wanavyosambaza mzigo kwa wateja wao, kwenye saluni za kike na kiume,kwenye supermarket, kwenye ofisi za serikali ,na za watu binafsi, kwenye mashule, magereza, nyumbani kwa watu , maduka ya watu na vyuoni. Tunawatumia mpaka wanafunzi kusambaza mzigo, tena wanafunzi wa kike wa shule za sekondari na vyuo ni wasambazaji wetu wazuri na waaminifu sana. Malipo sio mabaya, bosi wetu Biggie analipa vizuri, ukifanya kazi nzuri na kuwa mwaminifu. Kama uko tayari kesho nikakutambulishe kwa Biggie, hana noma ananiamini sana, nikisema wewe ni rafiki yangu kutoka Tanzania, umekuja kutafuta mchongo huku, na unataka kujiunga na sisi atakubali.
"Au unasemaje mshkaji"? Davi akamuuliza.
" Davi, nitakupa jibu kesho, leo nina uchovu sana wa safari, acha nitafakari mpaka kesho nitakupa jibu." Chilly akamuambia Davi.
" Umesema kweli, nenda chumba hicho hakina mtu ulale, tutaonana kesho ,sisi usiku huu tuna kazi ya kufanya.".Davi akamuambia Chilly boy.

Kesho ikafika, ilikuwa ni siku ya jumatano, asubuhi muda wa saa moja , akasikia mlango unagongwa, Davi akaamka nakwenda kufungua mlango, akasikia sauti za kike, kisha wakaingia ndani, Chilly boy akaenda kuwaangalia wageni, walikuwa ni mabinti wa sekondari sita, wako na sare zao za shule, walikuwa wasichana warembo mno, Chilly akaduwaa, akakambuka maneno ya Davi aliyomuambia jana usiku.
"Tunawatumia mpaka mabinti wa sekondari na vyuo, tena ni wasambazaji wetu waaminifu", akakumbuka haya maneno., bila shaka hawa ni mojawapo wa wasambazaji wa unga, akashangaa sana. Wabinti warembo namna hii wanauza unga? tena mabinti wa shule? Chilly boy alishangaa sana, wale mabinti wakawa wanamuangalia Chilly boy kwa wasi wasi.
" Msiogope,huyu ni rafiki yangu kutoka Tanzania amekuja jana , tutakuwa nae ni mgeni, msimuogoppe, tena mumpe kampani". Davi akawaambia wale wanafunzi, wakamsalimia Chilly boy kwa uchangamfu sana, kisha Davi akawapa mzigo, kila binti na mzigo wake, zilikuwa pakiti za unga zimewekwa kwenye bahasha ,wakafungua mabegi yao ya shule na kuweka mzigo wa unga ndani, wakasimama na kuelekea mlangoni,
"Mjitahidi kumaliza mzigo leo, tutaonana jioni", Davi akawaambia,kisha akaenda kufunga mlango na ufunguo, Hawa ni wasambazaji wetu wakubwa wa unga, na wanachapa kazi kweli kweli, Davi akamuambia Chilly boy, kisha akarudi chumbani kulala. Chilly boy akakaa sebuleni mwenyewe baada ya kunywa chai, Kama hawa mabinti,tena wa shule wanafanya hii biashara bila uoga wa kukamatwa, mimi mwanaume nitaogopaje, si nitaonekana mjinga? Chilly boy akaamua kujiunga na akina Davi.

Baadae mida ya saa nne Davi, Hamisi na Mohamed walikuwa wameshaamka, wameshajiandaa baada ya kunywa chai na kuoga , walikuwa wanataka kutoka, " "Vipi mshkaji, umeshafanya maamuzi"?Chilly boy akamuambia amekubali kujiunga nao, hakuna namna nyingine anaweza kuishi Afrika Kusini zaidi ya hiyo,hana ujuzi wwa fani yoyote, alikuwa ameingia kwenye mtego, na hana namna ya kujinasua. Davi akaenda kumtambulisha kwa Biggie. Na hivi ndivyo Chilly boy alivyoingia kwenye biashara ya unga.

itaendelea......................................
 
Sehemu ya 6:

Ni takribani miaka mitatu toka Chilly boy afike Afrika Kusini, maisha yake yalikuwa mazuri sasa, alikuwa anamiliki gari aina ya BMW na kuishi kwenye apartment ya peke yake katikati ya jiji la Johanesburg, mambo yake yalikuwa mazuri, alikuwa ndio msambazaji mkuu wa unga wa bosi Biggie,. Bosi Biggie alitokea kumpenda na kumuamini sana Chilly boy. Chilly boy alifanya kazi kwa uaminifu mkubwa, na kila mzigo wa unga aliopewa na bosi Biggie, alihakikisha anauuza kwa wakati, na kuwasilisha pesa kwa bosi bila usumbufu wowote. Na hata siku alipovamiwa na wazulu na kuporwa mzigo bosi Biggie hakupoteza uaminifu kwake. Anaikumbuka viziri siku hii.

•••••••••••••••••••••••••••••

Ilikuwa ni siku ya jumamosi usiku majifa ya saa sita, wakati ametoka Club Go-Go anaelekea Club 007, alikuwa anatembea kando ya barabara, alikuwa na miezi sita tokav awasili Afrika Kusini, aliona gari ambayo haikumbuki sawa sawa inakuja nyuma yake kwa mwendo wa taratibu, wakati anageuka kuiangalia, ghafla walishuka watu wawili kutoka siti za nyuma, na mmoja aliekuwa amekaa siti ya mbele,pembeni ya dereva, wanashuka kwenye gari kwa kasi ya umeme, wakamvamia, mmoja alikuwa nyuma yake akampiga na kitako cha bunduki, wakamshambulia kwa mangumi na mateke mpaka wakapoteza fahamu, alikuja kuzinduka siku ya tatu akiwa hospitali, kando yake ya kitanda cha hospitali, alikuwa amesimama bosi wake Biggie na Davi.
'" Vipi Chilly boy unajisikiaje", bosi Biggie alimuuliza kwa sauti ya upole iliyomshangaza.
Baada ya siku tatu alipata nafuu kabisa na kuruhusiwa kutoka hospitali, Bosi Biggie akamuita ofisini kwake.
" Itabidi upate mafunzo ya kujihami, Chilly boy, na mafunzo ya kutumia silaha," Biggie alimuambia.

Baada ya mwaka mmoja, Chilly boy alihitimu mafunzo ya kujihami, karate na judo, na mafunzo ya kutumia silaha,na kulenga shabaha, Biggie akampa Bastola, Sasa hivi Chilly boy ni mtu hatari na nusu, kuna wazulu watatu walitaka kumpora tena mzigo wake, wawili waliishia hospitali, na mmoja akaishia kaburini. Chilly boy anaogopeka, habari zikasambaa kwenye viunga vya Johanesburg, Chilly boy hakusita kuondoa uhai wa yoyote atakaejaribu kumsaliti, kwa Chilly boy kuua binadamu aliemsaliti, au kumkwamisha kwenye kazi zake ni sawa na kuua panya tu, habari za ubabe wa Chilly boy,zilitapakaa kila mtaa wa Johanesburg, wahuni wote wa mjini walikuwa wanamuogopa ,kila anapoenda, watu wanamheshimu na kumuogopa, na wengine wakimuona wanabadili njia. Ubabe na uaminifu wa Chilly boy ulimfurahisha sana bosi Biggie, sababu Chilly boy alikuwa hatumii unga, wala haakuwa mtu wa starehe na wanawake, alikuwa na mwanamke mmoja tu wa kizulu, anaefanya kazi supermaket, hakuwa mlevi, zaidi ya kunywa pombe mara moja moja siku za mapumziko akiwa na mwanamke wake. Tangia Chilly boy ajiunge nae, faida ya kwenye biashara yake ya unga imeongezeka maraduffu, Biggie akampa Chilly boy zawadi ya gari BMW nyeusi siku wa mwaka mpya.

Biggie ndani ya miaka mitatu amekuwa tajiri kupindukia, Biggie ana uhusiano wa karibu wa kibiashara na kundi hatari kwa biashara ya madawa ya kulevya Zetas la Al Chapo alieko jela Marekani, la Mexico. Mzigo wa unga anaouza Afrika Kusini, anautoa kwenye hili kundi, kila baada ya miezi sita, mzigo mkubwa wa unga kutoka Mexico unaingia Afrika Kusini kwa Biggie, wanamuamini sana Biggie, wanamtumia mzigo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni saba za Kitanzania kila baada ya miezi sita.

Biashara hii ilimfanya Biggie kuwa tajiri mkubwa, anamiliki magari ya kifahari na apartments za kupangisha za kutosha Afrika Kusini, na apartment moja ya Biggie ndiko anakoiishi Chilly boy, kwani mbali na kuuza unga, pia Biggie anajihusisha na wizi wa magari, anapora magari afrika kusini na kuyauza nchi za nje ya Afrika Kusini. Biggie akataka kupanua wigo wa biashara zake, Akaamua kuanzisha tawi la biashara zake za kuuza unga na magari ya wizi Afrika Mashariki, na vile vile iwe njia rahisi ya kupitisha mzigo wa unga kutoka Mexico.

Akaazimia kufungua tawi Tanzania, na hakuna mtu mwingine anaemuamini, mwenye uwezo wa kusimamia biashara zake kwa umahiri na uaminifu mkubwa zaidi ya Chilly boy.
Akamuita Chilly boy nyumbani kwake, "Njoo nyumbani leo saa nne kamili usiku, nina mazungumzo muhimu na wewe".
" Sawa bosi", Chilly boy akaduwaa kwa muda , anamjua vizuri bosi Biggie, kama anamuita nyumbani kwake usiku, basi kuna jambo la muhimu sana anamuitia, kuna nini"? Akajiuliza, ilikuwa ni majira ya saa tisa mchana wakati bosi Biggie alipompigia simu, Chilly boy akarudi nyumbani kwake, na kujipumzisha, akasubiri saa nne usiku aende kwa Biggie.

Ilipotimia saa nne usiku, Chilly boy akaenda nyumbani kwa Biggie, aliishi kwenye hekalu la gorofa, lenye walinzi zaidi ya kumi, bwawa la kuogelea, bustani safi, kwa ujumla ilikuwa nyumba ya kifahari sana. Chilly boy akaingia ndani, akamkuta bosi Biggie anamsubiri.
"Kwanza nikupe shukrani zangu kwa kunifanyia kazi zangu vizuri na kwa uaminifu mkubwa", Biggie akamuambia, ,akaendelea, " Ninampango wa kupanua wigo wa biashara zangu Afrika Mashariki, na Tanzania ndio itakuwa Makao Makuu, kutokana na uaminifu wako na uchapakazi wako, nimekuchagua kuwa kiongozi wa tawi langu jipya Afrika Mashariki, nimeshakuandalia nyumba ya kuishi Dar es Salaam maeneo ya Mbezi Beach, na tiketi ya ndege ya kesho jioni, nenda kajiandae maelekezo mengine nitakupa ukiwa huko huko Tanzania", Chilly boy akashangaa, " Mimi kiongozi wa tawi"? alijiuliza, habari hizi zilimfurahisha sana Chilly boy, maisha ya hatari ya kukoswakoswa kupigwa risasi na wazulu na magenge mengine ya kihalifu sasa yamefika mwisho hatimae narudi nyumbani Tanzania, tena sio kwa kuparamia lori, narudi kwa ndege. Na huo ndio ukawa mwisho wa Chilly boy Afrika Kusini.

••••••••••••••••••••••••••••••

Ilikuwa imepita miezi sita toka Chilly boy awasili Tanzania kutokea nchini Afrika Kusini, Bosi Biggie alimpangishia nyumba ya kifahari Mbezi Beach, mpaka muda huo , biashara yao ya unga ilikuwa inaenda vizuri, alivyoingia nchini, Chilly boy hakuwa na haraka ya kutafuta watu wa kumsambazia mzigo wake, Ana uzoefu wa kutosha wa usaliti kwenye hii biashara. Chilly boy akaamua kufanya biashara mwenyewe, ana uzoefu mkubwa wa kujua wateja wa hii biashara na tabia zao, akaanza kuzunguka kwenye macasino makubwa ya kifahari na hoteli kubwa za kitalii, huko akakutana na wafanyabiashara wakubwa wa kiarabu, kihindi,kizungu na waafrika wenzake, na watoto wa matajiri, Kwa uzoefu aliokuwa nao na kwa jinsi bosi Biggie anavyompa pesa nyingi za kazi hii, haikuwa ngumu kujenga urafiki na wafanyabiashara matajiri, wasanii wa muziki, wanamichezo, na wanasiasa, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali, na watoto wa matajiri, walimtambua Chilly boy kama kijana mdogo muuza magari mwenye mafanikio makubwa, alikuwa kila siku anabadili magari ya kifahari ya wizi aliyokuwa anatumiwa na bosi wake Biggie kutoka Afrika Kusini, kwa ajili ya kuyatafutia wateja, pesa alizokuwa anapewa na Biggie alizitumia kuwapa ofa na kufanya sherehe kwenye jumba lake la kifahari Mbezi Beach, akiwaalika wafanyabiashara wakubwa,wasanii,wanamichezo ,wanasiasa, watoto wa matajiri, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali, na watu wengine maarufu,kwa uzoefu wake haikuchukua muda kuwajua watumiaji wa unga, akawashawishi wakawa wateja wake, kwa kipindi kifupi alichofanya hii biashara Dar es Salaam, akawa mmoja wa wasambazaji wakubwa wa unga katika jiji la dar na vitongoji vyake. Alikuwa anawasambazia mzigo mwenyewe, hakuwa na wasaidizi, Chilly boy hakumuamini mtu mwenye hii biashara, ameshakumbana na kila aina ya usaliti na kudhulumiana kwenye hii biashara alipokuwa Afrika Kusini, ana kila kitu, pesa, ujuzi wa kupigana na kujihami, uwezo mkubwa wa kutumia bastola na kulenga shabaha, Amuogope nani? Chilly boy alijiamini sana.


Baada ya miezi kadhaa biashara yake ya unga ikazidi kushamiri, wateja wakawa wengi mpaka wakaanza kumshinda. Akafikiria kutafuta wasaidizi, hata bosi wake Biggie alimuambia atafute wasaidizi. Hakuwa na namna, inabidi awe na watu watakaomsaidia kusambaza mzigo kwa wateja wake.
Chilly boy akafikiria watu wa kumsaidia kazi, Lakini vipi kuhusu usaliti? Alijiuliza.
Alipokuwa Afrika Kusini alifanya kazi na watu wengi sana, akatafakari kati yao ni wapi walikuwa waaminifu, akawakumbuka mabinti wa shule wa sekondari na vyuo alivyofanya nao kazi kwa uaminifu, hawakuwahi kumsaliti, walikuwa waaminifu sana kwenye biashara, hawakuwa na tamaa. Ndiyo! hawakuwahi kumsaliti, inabidi atafute mabinti wa sekondari wakumsaidia kusambaza mzigo, tena wakisambaza mzigo wakiwa na unifomu zao za shule hawatagundulika na polisi kamwe!, Chilly boy akapata ufumbuzi wa tatizo lake. Lakini aanzie wapi mpango wake?Akachagua aanzie kutafuta kwenye shule ya wasichana ya sekondari Jangwani. Na hapa ndipo matatizo yalipoanza.

•••••••••••••••••••••••••••••••••


Ilikuwa ni siku ya ijumaa jioni, Chilly boy alikuwa amekaa ndani ya gari yake aina ya Toyota Prado ya wizi aliyotumiwa na bosi wake Biggie kutoka Afrika Kusini ili aitafutie wateja, alikuwa ameipaki gari nje ya barabara karibu na geti la shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani.Akawaona wanafunzi wanatoka getini na kuelekea nje ya geti, kati yao kulikuwa na mabinti watatu wameshikana mikono wanatembea na kucheka kwa furaha, alikuwa amewafatilia hawa mabinti kwa muda wa wiki tatu, na akawa anajua ni marafiki wakubwa sana, wanasoma darasa moja, kidato cha nne, na majina yao ni Nyasule, Maria na Monica.


Chilly boy alianza kwa kumfatilia Monica. Monica Anderson anaishi na wazazi wake Mwenge. Siku moja baada ya kutoka shule, Monica, Nyasule na Maria kama kawaida yao walielekea kwenye kituo cha dala dala pamoja, walipofika wakakaa kusubiri dala dala, Chilly boy alikuwa ndani ya gari yake Mercedes Benz ya wizi kutoka kwa Biggie Afrika Kusini amekaa kwenye usukani wa gari anawaangalia, dala dala za kuelekea Mwenge zilipofika, Monica akawaaga wenzake na kupanda, Chilly boy akawasha gari yake na kuifuatilia ile dala dala, kwa nyuma, hakuwa na haraka, dala dala ikisimama kusubiri abiria, na Chilly boy anasimamisha gari mbele na kusubiri, Monica akashukia Mwenge, karibu na kanisa la Kakobe, Monica alivyoshuka akaanza kutembea kwa miguu kuelekea kwenye barabara ya vumbi, Chilly boy akapaki gari yake pembeni ya barabara, akashuka na kumfuata Monica kwa nyuma, baada ya kutembea kwa muda, Monica akaingia ndani ya nyumba moja yenye geti la mbao. Kwa hiyo Monica anaishi hapa, Chilly boy akawaza. Baadae akaja kugundua Monica anaishi pale na wazazi wake, Baba yake ni mchungaji wa kanisa la K K K T na mama yake ni nesi Mwananyamala Hospital. Wanaishi kwenye nyumba ya Kanisa.


Siku inayofuata, kama kawaida ikawa zamu ya Maria Jackson, kama kawaida aliwasubiri jioni kwenye kituo cha dala dala wanakopandia dala dala karibu na shule, Maria akapanda dala dala ya Manzese, Chilly boy akiwa ndani ya gari yake nyingine ya wizi aina ya Subaru Forrester aliifuatilia ule dala dala kwa nyuma mpaka kituo alichoshuka Maria maeneo ya Manzese. Maria akaelekea nyumbani kwao kwa miguu, Chilly boy akapaki gari yake na kumfatilia, Maria akaingia kwenye nyumba moja ya kizamani ndani, haikuwa na geti, nje kulikuwa kuna mama anauza maandazi, baadae Chilly boy alikuja kugundua yule ni mama yake mzazi Maria, baba yake anauza kahawa, hapo hapo maeneo ya Manzese, wanaishi kwenye nyumba ya urithi ya babu yake mzaa baba, ndani kuna wapangaji watano.


Siku inayofuata ikawa zamu ya Nyasule Suleimani, kama ilivyo kawaida, aliwasubiri kwenye kituo cha daladala, Nyasule akapanda dala dala ya Mbagala, akaifuatilia ile dala dala aliyopanda Nyasule, siku hii Chilly boy alikuwa na gari aina ya BMW aliyopewa kama zawadi na bosi wake Biggie kwa kazi nzuri, dala dala ilipofika Mbagala, Nyasule akashuka, Chilly boy akapaki gari yake pembeni, na kumfuatilia Nyasule, baada ya kutembea kwenye kichochoro kidogo kwa muda, Nyasule akasimama mbele ya genge la nyanya, akaongea na yule mama pale gengeni kama dakika mbili, kisha akaingia ndani ya nyumba iliyoko nyuma ya lile genge la nyanya, baadae Chilly boy aligundua yule mama anaeuza genge ni mama yake Nyasule, na wanaishi wenyewe Nyasule na mama yake kwenye nyumba ya kupanga aliyoingia Nyasule.

itaendelea.............................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom