TANZIA Malkia wa Uingereza, Elizabeth II afariki dunia akiwa na miaka 96

20220828_202940.jpg
 
Hivi ili kupata Queen mwingine inatakiwa awe ni mtoto wa nani katika familia ya kifalme na ili kutawala mwanaume King kuhitimishwe aje Tena Queen ni sifa zipi au itifaki zipi za royal family zinatumika?
 
Wanafamilia wa karibu wa Malkia waelekea Balmoral
TH

Tunasikia watoto wote wa Malkia wamefika au wako njiani kuelekea Balmoral.
Malkia ana watoto wanne, wajukuu wanane na vitukuu 12:

• Prince Charles, Prince wa Wales, ndiye mtoto wake mkubwa na mrithi wa kiti cha ufalme Amemuoa Camilla, Duchess wa Cornwall

• Princess Anne, ni mtoto wa pili wa Malkia na binti pekee. Ameolewa na Makamu wa Adm Timothy Laurence na ana watoto wawili na mume wake wa kwanza, Kapteni Mark Phillips - Peter Phillips na Zara Tindall.

• Prince Andrew, Duke wa York, ni mtoto wa tatu wa Malkia na ana binti wawili na mke wake wa zamani, Duchess wa York - Princess Beatrice na Princess Eugenie. Alijiuzulu kutoka shughuli za "kifalme " mnamo 2019 baada ya mahojiano yenye utata ya Newsnight

• Prince Edward, Earl wa Wessex ndiye mtoto wake mdogo. Ni mume wa Sophie, Countess wa Wessex na wana watoto wawili - Louise na James Mountbatten-Windsor.

• Prince William, Duke wa Cambridge, pia amesafiri hadi Balmoral leo. Mwana mkubwa wa Prince Charles na mke wake wa kwanza, Diana, Princess wa Wales, amemuoaCatherine, Duchess wa Cambridge. Wana watoto watatu - Prince George, Princess Charlotte na Prince Louis

Nicholas Witchell
Mwandishi wa habari za familia ya kifalme

Taarifa ya kasri inaashiria mabadiliko makubwa
Taarifa kutoka Buckingham Palace ni muhimu kwa sababu ni tofauti na miezi michache iliyopita, wakati Buckingham Palace ilisema machache iwezekanavyo.

Ilisema malkia anasalia katika hali nzuri vizuri Balmoral.
Lakini ukweli kwamba Buckingham Palace waliona ni muhimu kutoa taarifa, na ukweli kwamba wanafamilia wanasafiri huko, inasema kila kitu.

Kama waziri mkuu alivyosema, nchi nzima itakuwa na wasiwasi mkubwa na nadhani lazima tuchukue kuwa kuna sababu za hilo.

Kumekuwa na kuzorota kwa afya ya Malkia katika miezi iliyopita. Kwa wazi zaidi ya saa 24 hadi 48 zilizopita madaktari wamekuwa na wasiwasi zaidi.
1662655052912.gif
1662655053109.gif
 
Back
Top Bottom