MduduWashawasha
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 1,653
- 601
hiyo sehemu iko Njombe tena pembeni ya barabara ya Njombe Songea. Katika ziara ya mwisho rasmi ya Prince Charles Tanzania alilala hiyo sehemu
Egongos, japo sijui kuhusu Iringa, ila kwa taarifa too, mali zote za serikali ya Uingereza duniani kote, kisheria zinamilikiwa na Malkia, na zimeorodheshwa kama HM properties, hivyo nyumba zote za wanabalozi wa Uingereza ni mali ya Malkia.Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Baba_Enock kaeleweka! Soma sentensi yake tena na tena, halafu ukimaliza mwombe samahani. lol!
Ni mashamba ya miwati na chai huko Lupembe na Njombe kama sikosei inaendeshwa chini ya kampuni iitwayo Crown(sorry nimesahau jina)
Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Matumizi makubwa ya product inayotokana na miwati ni kwenye viwanda vya ngozi' kubadili skin(animal) kuwa leatherNi kweli ni shamba la hiyo miti na watu wa kule walisema ni tangu kipindi cha ukoloni tulikuwa huko juzi juzi tunafanya baseline survey ya mambo ya kilimo,by the way miti hiyo inatumika kutengeneza kiwi za viatu.na lease waliyopewa ni ya miaka mingi tu.
Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.
Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.
Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)
Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.
Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.
Ni kweli wana mkataba wa miaka 99hivi na lile la wa saud arabia nilisikia liko kule loliondo bado wanalimiki??
naskia huwa wanatua na nduge zao na kuondoka bila kuulizwa na yeyote-ni kweli?