Malipo ya Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption

Status
Not open for further replies.
Unashangaa kwa nchi maskini,watu wanaamua kujilipa mamilioni bila tija yoyote na mamlaka za juu ziko kimya..,watu wakipiga kelele kuonesha kukerwa na hali hiyo 'wanahatarisha usalama wa nchi'..,nani kawaambia nchi hii ni ya kwao peke yao..?
 
Usiwe hivyo kukubali hasara, peleka madai yako utalipwa ni haki yako yote 20% utarudishiwa. Wahi, ukichelewa zitaisha

Nilikuwa mfanya kazi wa shirika la umma kwa kipindi cha miaka 16 hivi, lakini niliondoka na kuanza shughuli zangu mwenyewe. Kipindi hicho nilikuwa nakatwa michango ya PPF kutoka kwenye mshahara wangu kila mwezi, lakini baada ya kuondoka sikurudishiwa michango yangu hiyo eti kwa vile wanadai niliacha kazi kwa hiari yangu mwenyewe, hivyo sikuwa na haki na hela zangu zilizokatwa kama michango ya PPF; uonevu gani huo jamani, ile ilikuwa nji hela yangu! To the best wangenirudishia hela yangu halisi hata bila interest wakabaki na ile contribution ya mwajiri wangu. Kumbe hivyo ndivyo wanavyotumia pesa zetu?
 
Mimi bado nasubiri comments za wale waliokuwa wanamshambulia Mwanakijiji kuwa anaishambulia NSSF kwa sababu kiongozi wake ni mwislamu.
 
hatuwez kuchukua hela kwa kutumia keyboard. kimsingi ni kwamba tumevamiwa na wakoloni-wazawa. lazima tujikomboe. na bila kufa mtu katu hatutapata ukombozi. lakini mitanzania ilivyokuwa mioga najua itasema "anza wewe".[/QUOTE]

haya bwana anza wewe sasa.
 
Mwanakijiji Asante sana na hapo sasa unatenda haki ulizidi kuiandama NSSF mkuu. Ndio naweka msisitizo wa kauli yangu nyuma kwamba Pension funds za Tanzania zinatumika kama shamba la bibi na zikija kuanguka tutalia na kusaga meno maana uchumi wetu utayumba vibaya sana na nchi kupoteza mwelekeo. Nasubiria kwa hamu malipo ya mzee Erio maana inaelekea ni kitita cha nguvu yeye na wapambe wake. Maskini wachangiaji wa PPF.
 
Nisaidieni tumwondoe CAG na NAO yake yote. Hana analofanya huyu baba pamoja na mshahara mkubwa. Kwenye Halmashauri/manispaa/miji fedha zinahamishwa si kawaida. Madaraja yanajengwa kwenye makaratasi tu. Serkali Kuu, BOT, Mashirika ya UMMA usiombe.
 
Wild Car,

Tatizo halipo kwa CAG kwasababu yeye anafanya kazi yake vizuri tu. Tusingeliweza kuyagundua madudu haya bila yeye we have to give Mr Utouh a credit for that. Ishu hapa ni accountability na uadilifu kazi. Mambo yanatajwa na CAG, ila utekelezaji hakuna ndio hivyo tena watu wanajichotea vitubilioni vyao kwa mgongo wa our hard earned money.
 
Ahsante Mwanakijiji kwa post yako. Ila suala la corruption hapo hakuna. Therefore, your headline kwenye hii post may be misleading. Mimi sioni rushwa hapa. Kwa taarifa yako, haya malipo ni jambo la kawaida kwa mashirika ya umma. Kusema kuwa PPF is rewarding corruption is both inaccurate and unfair kwani PPF ina Board of Trustees ambayo inawakilisha wadau wote -- ikiwemo serikali na wafanyakazi kupitia trade unions. For your information, haya malipo yamepitishwa na Bodi ya PPF kwa wafanyakazi wa menejimenti na yamekuwa yakifanyika miaka mingi wanapostaafu nk.

Ieleweke kuwa malipo haya hayafanyiki PPF tu bali kwenye taasisi zote au mashirika yote makubwa serikalini yenye pesa nyingi mfano Benki Kuu (BoT), NSSF, PSPF, Tanzania Ports Authority, TRA, Tanzania Investment Bank, TANAPA na kwingineko.
Juzi Director General wa PSPF amestaafu, hebu fuatilia PSPF wamemlipa milioni mia ngapi kama kifuta jasho chake uone mambo.

Hapa unahitajika mjadala mpana zaidi kuhusu mafao (remunerations) ya manejimenti ya mashirika ya umma kulinganisha na ya wafanyakazi wa kada za chini. Vingenevyo kuendelea kuitaja NSSF mara PPF kuwa eti zina matumizi mabaya ni kama withchunting au kuziandama taasisi hizi na viongozi wake.

Hebu jaribu kufuatilia BoT, TRA, PSPF au hata Daily News (TSN) uone menejimenti wanalipana pesa ngapi.

Naomba tufanye mjadala uwe mpana zaidi kwa kuangalia mashirika yote makubwa ya umma wanalipana vipi ili tuweze kufanya comparisons na kujua ukweli uko wapi kuliko kila siku kuwanyooshea vidole NSSF na PPF na to jump to conclusions kuwa kuna corruption.

Tupo pamoja!...
 
Warofo,

Wazo lako zuri ila kuna shida mmoja tukianza kulinganisha malipo ya menejiment tutakuja kukwama katika performance yao kiutendaji. Na hii ni kwasababu performance ya NSSF, PPF, PSPF, Daily News, BOT na TRA wanatofautiana. Labda ungelikuwa specific kusema tulinganishe kitu gani?

Umezungumzia malipo yameidhinishwa na Board of Trustee kumbuka jiulize ni kina nani wamo ndani ya board of trustee katika hizi pension funds. Utakuta board zao zimejaa wanasiasa, wafanyabiashara na management yenyewe. Sasa unavyofikiri uhuru wa maamuzi ya board upo? Mfano mwaka 2006 Chairman wa Board alikuwa Gray Mgonja (Katibu mkuu wa Ministry for Finance), Members walikuwa Monica Mbega (MP), Ramadhan Khijja (Katibu mkuu wa wizara siikumbuki), Elvis Musiba (Chairman TCCIA), Professor Bertha Koda, Samwel Lwakatare, na William Erio. Hapa tunaona kabisa board imeongozwa na utashi wa wanasiasa na behind the closed door serikali je maamuzi yao yatakuwa huru? Pia ukiichunguza zaidi board unaona CEO au DG wa PPF yupo ndani ya Board na hivyo basi akifahamu haya malipo yanamnufaisha mwenyewe unafikiri atayapinga? Binafsi DG alitakiwa asiwe board member kama ni member basi asiwe na voting right kuzuia ufisadi. Vile vile wanasiasa wasiwemo katika board maana watatekeleza matakwa ya chama tawala.

Usisahau impact ya kuanguka kwa pension mkuu kutaathiri uchumi wa Tanzania kwani kuna pesa za wavuja jasho na serikali itabidi iwabail out . Sasa serikali yetu yenyewe haina hela na inadaiwa na hizo pension mabilioni kwa matrilioni unafikiri kitakachofuatia hapo ni nini???
 
Hakuna Mjadala wowotekuhusiana na ushenzi huu maadam kuna watu wanadai pension zao toka kufa kwa EAC,walimu na wafanyakazi wengi walioachishwa kazi a wengine kustaafu baada ya mashirika mengi ya serikali kubinafsishwa.. Haki yao inatangulia mbele ya kila kitu..
Hii ni dhulma na haiwezi kubeba kwa kutumi vigezo ambavyo havi apply sawa na kesi hii...
 
Nisaidieni tumwondoe CAG na NAO yake yote. Hana analofanya huyu baba pamoja na mshahara mkubwa. Kwenye Halmashauri/manispaa/miji fedha zinahamishwa si kawaida. Madaraja yanajengwa kwenye makaratasi tu. Serkali Kuu, BOT, Mashirika ya UMMA usiombe.

Shika adabu yako wewe unataka NAO ifutwe ili tuje kula kwako au??! Chunga sana aise
 
punguza muda wa kushangaa uanze kutoa ideas za kupambana na matukio yanayoaibisha taifa kama haya

Hayani hii habari imeniudhi mpaka nasikia kichefuchefu. Nchi yetu ni nchi masikini na hakuna sababu yeyote inayoweza kujustify upumbavu huu, kwa nini walipwe hela zote hizi?
 
Ahsante Mwanakijiji kwa post yako. Ila suala la corruption hapo hakuna. Therefore, your headline kwenye hii post may be misleading. Mimi sioni rushwa hapa. Kwa taarifa yako, haya malipo ni jambo la kawaida kwa mashirika ya umma. Kusema kuwa PPF is rewarding corruption is both inaccurate and unfair kwani PPF ina Board of Trustees ambayo inawakilisha wadau wote -- ikiwemo serikali na wafanyakazi kupitia trade unions. For your information, haya malipo yamepitishwa NA BODI ... .............

[/B]Hebu jaribu kufuatilia BoT, TRA, PSPF au hata Daily News (TSN) uone menejimenti wanalipana pesa ngapi.

Naomba tufanye mjadala uwe mpana zaidi kwa kuangalia mashirika yote makubwa ya umma wanalipana vipi ili tuweze kufanya comparisons na kujua ukweli uko wapi kuliko kila siku kuwanyooshea vidole NSSF na PPF na to jump to conclusions kuwa kuna corruption.

Tupo pamoja!...

Haya ni malipo ya kawaida?! Jamani hivi ukawaida unakuja wakati huu wa awamu ya nne? Mkuu tuletee takwimu ... .... .. hata nchi zilizoendelea hawalipani kinyemela namna hii. Bring the evidence please you will do us a favour.
 
Mimi bado nasubiri comments za wale waliokuwa wanamshambulia Mwanakijiji kuwa anaishambulia NSSF kwa sababu kiongozi wake ni mwislamu.

Hii hapa chini naona chacha maona menyewe anza kunawa mikono khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee

Mwanakijiji Asante sana na hapo sasa unatenda haki ulizidi kuiandama NSSF mkuu. Ndio naweka msisitizo wa kauli yangu nyuma kwamba Pension funds za Tanzania zinatumika kama shamba la bibi na zikija kuanguka tutalia na kusaga meno maana uchumi wetu utayumba vibaya sana na nchi kupoteza mwelekeo. Nasubiria kwa hamu malipo ya mzee Erio maana inaelekea ni kitita cha nguvu yeye na wapambe wake. Maskini wachangiaji wa PPF.

Khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee Mdondoaji aka ... .... ...... ... pole kaka/dada Oooops JF Senior Expert member ugonile? (salaam tu hizo za kumpelekea baba)
 
Mwanakijiji Asante sana na hapo sasa unatenda haki ulizidi kuiandama NSSF mkuu. Ndio naweka msisitizo wa kauli yangu nyuma kwamba Pension funds za Tanzania zinatumika kama shamba la bibi na zikija kuanguka tutalia na kusaga meno maana uchumi wetu utayumba vibaya sana na nchi kupoteza mwelekeo. Nasubiria kwa hamu malipo ya mzee Erio maana inaelekea ni kitita cha nguvu yeye na wapambe wake. Maskini wachangiaji wa PPF.

Ndio tatizo; kwa hiyo unafikiri kwa kufanya hivi maana yake imehalalisha sasa mimi kuendelea kufuatilia NSSF? This is sad.
 
Hakuna Mjadala wowotekuhusiana na ushenzi huu maadam kuna watu wanadai pension zao toka kufa kwa EAC,walimu na wafanyakazi wengi walioachishwa kazi a wengine kustaafu baada ya mashirika mengi ya serikali kubinafsishwa.. Haki yao inatangulia mbele ya kila kitu..
Hii ni dhulma na haiwezi kubeba kwa kutumi vigezo ambavyo havi apply sawa na kesi hii...

Mkandara; kumbukeni hatujaangalia malipo ya mashirika mengine kwa wakurugenzi. Karibu sheria zote zinazoongoza Bodi za mashirika ya umma zina kipengele ambacho kinasema kuwa malipo (compensantion) ya wana bodi zitapangwa na Waziri baada ya kupokea mapendekezo toka kwa bodi... This is true PPF, NSSF, na "Fs" nyingine zote..
 
Warofo,

Wazo lako zuri ila kuna shida mmoja tukianza kulinganisha malipo ya menejiment tutakuja kukwama katika performance yao kiutendaji. Na hii ni kwasababu performance ya NSSF, PPF, PSPF, Daily News, BOT na TRA wanatofautiana. Labda ungelikuwa specific kusema tulinganishe kitu gani?

Umezungumzia malipo yameidhinishwa na Board of Trustee kumbuka jiulize ni kina nani wamo ndani ya board of trustee katika hizi pension funds. Utakuta board zao zimejaa wanasiasa, wafanyabiashara na management yenyewe. Sasa unavyofikiri uhuru wa maamuzi ya board upo? Mfano mwaka 2006 Chairman wa Board alikuwa Gray Mgonja (Katibu mkuu wa Ministry for Finance), Members walikuwa Monica Mbega (MP), Ramadhan Khijja (Katibu mkuu wa wizara siikumbuki), Elvis Musiba (Chairman TCCIA), Professor Bertha Koda, Samwel Lwakatare, na William Erio. Hapa tunaona kabisa board imeongozwa na utashi wa wanasiasa na behind the closed door serikali je maamuzi yao yatakuwa huru? Pia ukiichunguza zaidi board unaona CEO au DG wa PPF yupo ndani ya Board na hivyo basi akifahamu haya malipo yanamnufaisha mwenyewe unafikiri atayapinga? Binafsi DG alitakiwa asiwe board member kama ni member basi asiwe na voting right kuzuia ufisadi. Vile vile wanasiasa wasiwemo katika board maana watatekeleza matakwa ya chama tawala.

Usisahau impact ya kuanguka kwa pension mkuu kutaathiri uchumi wa Tanzania kwani kuna pesa za wavuja jasho na serikali itabidi iwabail out . Sasa serikali yetu yenyewe haina hela na inadaiwa na hizo pension mabilioni kwa matrilioni unafikiri kitakachofuatia hapo ni nini???

Malipo ya NSSF kwa Wakurugenzi wake na Bodi ni kiasi gani kulinganisha na yale yale ya PPF kwa mfano?
 
Mzee Mwanakijiji, wewe una nzi wengi wanakupatia taarifa. Waambie wakupe taarifa za mikopo, mishahara, marupurupu, na benefits zingine wanazolipwa watu walioko kwenye menejimenti ya mashirika ya umma mengine Tanzania ili tufananishe na hizo invoice za PPF ulizoweka.

Hoja yangu ni kuwa wakati wewe umesema malipo hayo ni "corruption", ukweli ni kuwa malipo ya aina hiyo ni jambo la kawaida sana kwenye mashirika ya umma yote makubwa hapa nchini. Ndiyo maana nasisitiza kuwa tukikaa kuwanyooshea kidole PPF na kuwashutumu eti kwa "rushwa", watu wanaofahamu yanayojiri kwenye mashirika ya umma Tanzania wanabaki kutucheka.

Tupanue mjadala. Kama tunaangalia malipo ya menejimenti kwenye mifuko yote ya pensheni hilo ni jambo zuri. Tuangalie NSSF, PSPF, GEPF, NHIF, LAPF na ZSSF pia wanalipana kiasi gani. Si kurukia malipo ya PPF peke yao na kuwapa jina la mafisadi.

Tukitoka kwenye mifuko ya pensheni tuangalie pia mashirika mengine ya umma kama BoT, Bandari, TANAPA, TRA, TIB na wengine tuone malipo yao na tufanye comparison na mafao ya wafanyakazi wengine wa mashirika ya umma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom