Malipo kulingana na sheria ya Mkataba

Nino

Member
Jun 21, 2007
38
1
WanaJF, tafadhali mnisaidie.

Mimi ninataka kuchimba kijijini fulani, kwa hiyo niliwaomba "DRILLING AND DAM CONSTRUCTION AGENCY" wanipatie makadirio.

Basi waliandika "The estimated cost has to be paid to drilling and dam construction Agency in advance and thereafter the project implementation may start immediately."

Je, kulipa kabla ya mwanzo ya kazi ni halali? Mimi nitakuwa na dhamana gani?

Asanteni sana,

Nino Unapotoa kazi kwa mkandarasi unakuwa umeshamfanyia "evaluation" juu ya uwezo wake. Kwa upande mwingine ameshakufanyia "evaluation" kuhusu uwezo wako wa kulipa. Kama ni kisima cha kijiji kinachotegema ruzuku toka serikalini, mkandarasi hana uhakika kama pesa hiyo italetwa na serikali ili alipwe, kuepuka usumbufu huu ndio maana anataka kwanza malipo ili aanze kazi. Wewe kama huamini atafanya hiyo kazi, weke kipengele cha kumtaka alete "Performance guarantee toka bank" ya kurudisha pesa endapo atashindwa kufanya kazi kama mlivyo kubaliana.

Kwa taratibu za kazi za ukandarasi, kuna malipo ya awali kwa ajili ya kuandaa vyombo na vifaa vya hiyo kazi lakini kimsingi malipo hufanywa kwa kazi iliyokwishafanyika na kuhakikiwa na "consultants".
 
Last edited by a moderator:
WanaJF, tafadhali mnisaidie.

Mimi ninataka kuchimba kijijini fulani, kwa hiyo niliwaomba "DRILLING AND DAM CONSTRUCTION AGENCY" wanipatie makadirio.

Basi waliandika "The estimated cost has to be paid to drilling and dam construction Agency in advance and thereafter the project implementation may start immediately."

Je, kulipa kabla ya mwanzo ya kazi ni halali? Mimi nitakuwa na dhamana gani?

Asanteni sana,
Nino
Hizo estimated costs ni binding kwa kiasi gani? Makubaliano yapoje kama kwenye actual implementation hizo estimated costs zitazidi au kupungua? What is fixed - performance au costs?
 
Ndachuwa, asante sana kwa jibu lako la haraka sana. Nimefurahi kuona kwamba hata kwenu malipo hufanywa kwa kazi iliyokwishafanyika na kuhakikiwa na "consultants". Kwenu kabla ya mwanzo wa kazi hulipwa "kishika mkono" tu.

Mkandarasi atalipwa na mimi mwenyewe siyo kwa serikali! Nitajaribu kufanya kama ulivyoni shauri: nitajaribu kuweka kipengele kile.

Asante sana,
Nino
 
Hizo estimated costs ni binding kwa kiasi gani?

Samahani, lakini sielewi swali lako :confused:

Makubaliano yapoje kama kwenye actual implementation hizo estimated costs zitazidi au kupungua? What is fixed - performance au costs?

Hatujakubaliana! Unanishauri niwaombe waweke vipengele hivi?

SMU, nakushukuru sana,
Nino
 
Samahani, lakini sielewi swali lako :confused:
Maana yangu ilikuwa kama hiyo waliokupa wanasema ni estimated costs, ikitokea cost halisi inazidi hiyo/au inapungua haki yao au yao ipoje? Ni vema mambo haya yakawa wazi kwenye mkataba/makubaliano.
 
Back
Top Bottom