ntasema kidogo juu ya hili
Katika mkutano ule tanzania ilipeleka watu 24 wasio na uwezo wowote wa kujenga hoja na pia hawakuwa wamejiandaa vya kutosha katika kukabiliana na swala hili. mkutano ulikuwa wa siku tano lakini baada ya siku tatu watanznaia walikuwa hawana hoja zaid za kuongea na kilichobaki kilikuwa ni kubisi na kusema sehemu yziwa ni mali ya tanzania.
katika kikao hicho wamalawi walihoji kwa kutumia taarifa ya membe aliyoitoa bungeni kuwa tanzania inamiliki ziwa hilo toka latitude 9 hadi 11. waliuliza hizo latitude zinaanzia wapi na kuishai wapi.katika utetezi tume ya watanznaia waliowakilisha walishindwa kuelezea jambo hilo na kulikuwa na mkanganyiko mkubwa katika majibu yao.
moja ya hoja za watanzania zilikuwa ni kwamba tanzania inamiliki ziwa hilo kwa asilimia 50 na malawi asilimia 50.. ndipo malawi wakahoji kama tunamiliki ziwa hili kwa 50/50 je msumbiji inamiliki ziwa kwa asilimia ngapi maana sehemu ya ziwa hilo iko pia msumbiji.watanzania walishindwa kujibu. na hili swali liliuzwa pia na chiume waziri wa mambo wa nje wa malawi alipokutana na membe pale serena hoteli mwezi uliopita na membe hakulijibu swali hilo.
kwa kifupi ni kwamba wawakilishi hawakuwa uwezo wa kujenga hoja , maandalizi yalikuwa duni, taarifa a membe bungeni ilileta mkanganyiko mkubwa sana..
Hapo kwenye RED, mimi ndiye niliyeleta thread ya kuhusu upotoshaji alilofanya Membe mle bungeni kwa kutaja coordinate mbovu mle bungeni. Click here.
Waliobeza thread hii haya ndiyo matokeo yake mmejifunza adabu. Binafsi nimefurahi nilichoonya kupuuzwa na kikaleta madhara.
Nahisi ziiwa si letu kwani tunaishi kwa mipaka ya wakoloni.! Haki yetu ipo wapi? I stand to be corrected. Napenda pia kujua mipaka ikoje pale ziwa victoria na Tanganyika usikute hatuna kitu tena
Huo mkataba wa Heligoland Zanzibar una kurasa kama 6 hivi, mpaka wa ziwa Nyasa umewekwa kwa robo ukurasa tu na uko wazi ziwa lote liko Malawi, sasa hawa AGs watakuja na lipi jipya? Ule mkataba hauhitaji hata cheti cha sheria kuuelewa.
Kaka sijakupata vizuri, do you mean hatumiliki hata centimeter moja ya ziwa ama?Wala usibabaike. Mipaka yote ya Tanzania iliwekwa kipindi kile na wajerumani na waingereza na asikudanganye kwamba kuna hata sentimeta moja ya mipaka hii haikuwekwa kwenye mkataba.
Zote hizi porojo za kudai eti nusu kwa nusu ni porojo ambazo ukijaribu kuzitetea lazima ujiandae kula matapshi yako na kuwafanya wamalawi waonekane wataalamu katika hili.
Kaka sijakupata vizuri, do you mean hatumiliki hata centimeter moja ya ziwa ama?
Nimejaribu ku-attach ule mkataba wa Heligoland Zanzibar ili tuone kama kuna hoja ya msingi kuendelea na majadiliano hayo ya Membe na Chiume. Issue ya mgogoro huu ipo katika article I (2) inaelezea mpaka utakavyokuwa ambapo hakuna shaka sisi kama Watanzania hatuna chetu kwa mujibu wa mkataba huu. Hata hivyo zipo loopholes ambazo tunaweza kuzitumia ili kuu-defeat mkataba huu kwa mfano sehemu ya mwanzo ina maneno haya:
'This treaty temporarily settled colonial disputes between Germany and Great Britain. It recognized Tanganyika as a German colony; in return, the Germans abstained from further encroaching into British Kenya. The agreement ceded Heligoland, an island off the coast of Schleswig-Holstein in the North Sea, to Germany. Because the treaty appeared to abandon German colonial claims to much of east Africa, it unleashed a storm of nationalist protest at home.'
Hapo kwenye nyekundu inaonekana kama ifuatavyo:
(1) Mkataba huu uliondoa migogoro ya kimipaka kati ya Uingereza na Ujerumani kwa muda (temporarily),
(2) Wajerumani walikuwa wakiendelea kuchukua maeneo kutoka koloni la Uingereza liitwalo Kenya; hivyo kwa mujibu wa mkataba huu waliacha kufanya hivyo.
Ni wazi kuwa hapakuwa na mgogoro wowote katika mpaka wa ziwa Nyasa, inawezekana Wajerumani walikuwa wamechukua eneo kubwa kutoka Kenya hatimaye walikubali mpaka wa kusini yaani huko Ziwa Nyasa upite kando kando ya ziwa, hata hivyo mkataba huu ulikuwa ni wa muda tu. Kwa kuunganisha na kijiramani cha German Osta Africa kilichoambatishwa hapa pamoja na ramani za Mwingereza zinazoonesha mpaka ukiwa ndani ya ziwa tunaweza ku-raise doubts kwa mahakama za kimataifa na hatimaye kutupiliwa mbali kwa madai ya Malawi kupitia Heligoland Zanzibar Treaty.
Lengo letu kuu sasa hivi ni kuufanya mkataba wa Heligoland Zanzibar usiwe na nguvu kwa wakati uliopo (kwa sababu huu makataba ndiyo kiini cha madai ya Malawi), tusipopata hoja za kupambana na huo mkataba hilo ziwa litakuwa limeondoka rasmi katika vitabu, ramani, nyaraka zote za Tanzania endapo Malawi watakwenda katika mahakama za kimataifa.
Mimi sio mtalaam wa sheria lakini ninachofahamu mshitakiwa hahitaji kuthibitisha mahakamani kuwa hakutenda kosa bali anatakiwa kuonesha mashaka mbele ya mahakama (to raise doubts) katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ili upande huo wa mashitaka ushindwe kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa mshitakiwa alitenda kosa.
AG na timu yako pamoja na wanasheria wote wa nchi hii bila kujali itikadi za kisiasa, unganisheni nguvu tuikomboe nchi yetu pasi na kumwaga damu.
Mimi sikuwahi kutetereka kutamka kwamba kama base ni mkataba, tusitarajie kupata hata tone moja la Ziwa Malawi.

tuwe Wazalendo, tusishabikie mapungufu yetu! tusiwape Maadui zetu faida
Mimi sikuwahi kutetereka kutamka kwamba kama base ni mkataba, tusitarajie kupata hata tone moja la Ziwa Malawi.
Malawi hawajawahi kuwa maadui zetu kwani hawajatuvunjia haki yetu yoyote inayotambuliwa na mikataba ya kimataifa.