Malawi, Tanzania border talks kickoff, Chiume warns experts to avoid 'careless talk'

By Collins Mtika | NyasaTimes | August 20, 2012

The 24 member Tanzanian delegation is led by Dr Selassie Mayunga, Director of Surveys and mapping division in the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Developments.

Mayunga told Nyasa Times in a separate interview that the meeting is not meant to mark boundaries again but to have negotiations on the dispute as per Africa Union directive of 2007.

Chiume concurred with Mayunga saying the meeting was not an opportunity for experts from either side to seek fame or score points but rather to do what is legally right for people of both sides.
.........

Sijalipenda hilo neno "Negotiating"............ni kama vile tayari upande wetu umeanza na kushindwa ku-protect hoja za Watanzania.......no way under the sun....eti boda iwe kingoni mwa upande wa Tanzania.....kama tutakubali hii hata Wamalawi watatucheka na kutubeza kuwa hatuwezi kusimamia haki zetu........kwani wao wanafahamu kuwa wanachokisema si sahihi na ndio maana wanaendelea kusisitiza...........

African Union Directive of 2007 inasemaje?.........why and what are we negotiating for?
 
Hii kutoka fb ya balozi wetu Malawi:
Patrick Lusiano Tsere

2 hours ago

Leo mkutano wetu wa mpaka umeanza na ulifunguliwa na Waziri Chiume wa Mambo ya nje. Ujumbe wetu tulikuwa 13 wa Malawi 20 na ushee, tena mzito haswa. Hotuba ya Waziri Chiume ilikuwa nzuri na iliyojaa ushauri mzuri kwetu sote. Kila upande ulitoa hoja kuhusiana na msimamo wake. Ingekuwa tuko chuoni na kama ni thesis basi ile ya Tanzania ingestahili PHD tena with distinction ilhali ya wenzetu ilikuwa inastahili pass ya kufutia machozi! Jamani inatosha nisiseme mengi. Ila Tanzania ina hoja nzito sana. Maana jamaa baada ya kusikia wamepigwaa na butwaa na mshangao. Maana data zetu zilikuwa mpaka na hati na ramani. Hio ndio habari yenyewe. Hivi sasa kila upande unapitia hoja na maelezo ya upande mwingine ili kesho tutoe feedback!

Unfortunately mimi sikufurahishwa kabisa na post hii hasa kama imetoka kwa balozi wa nchi kwa vile ni post ya kishabiki ambayo haina hata chembe moja ya diplomasia. Mtu huyu kama balozi wetu, anatakiwa awe mtu mwenye kujua maana ya diplomasia. Post hii inaweza kusababisha stalemate ambayo ndiyo tunayohitaji kuzuia ili kumaliza mpaka. Maneno mafupi tu kuwa ".........tumeanza majadiliano, na tumeweka kesi yetu mbele ya wenzetu na kutoa ushahidi wetu kuhusu msimamo wetu, tumewaacha nao watoe kesi yao na ushahidi wao......" ingetosha sana. Siyo kujidai kuwa tumetoa Ph.D thesis ya distinctition na wao hawakutoa kitu; huo ni upuuzi mkubwa sana kufanywa na balozi. Kwanza sijui kama kweli balozi huyu anajua uzito uliomo kwenye Ph.D thesis kwa vile sina uhakika kama kweli alishawahi kuifanya au kuisimamia!!

Post hii inaonyesha jinsi gani anavyotoa hoja zake; yaani kama mabalozi wetu wanafanya kazi kama vile wako vijiweni basi njia yetu inazidi kurefuka sana.
 
Are we sure the Tsere who has posted these comments on JF is the same Tsere who is Tanzania's High Commissioner to Malawi? If it is the same person then he should go back to the Diplomatic school to learn more about diplomatic etiquete and protocols especially when one is part of a Government Delegation to sensitive meetings outside the country.
 
Nina MPDF mengi sana yanayoonyesha jinsi gani mpaka ulivyohama pole pole.

(1) Kabla ya mkutano wa Berlini, ulaya ilikuwa inataka pwani ya afrika tu; kwa hiyo kwa vile pwani yetu lilikuwa chini ya Sultani wa Zanzibar, ujerumani haikuwa na interest yoyote na nchi yetu. Wao walitaka Namibia, Cameron na Togo tu. Kuna kichaa mmoja aitwaye Karl Peters ndiye aliyetaka ujerumani iichukue nchi yetu kwa vile alikuwa keshafanya mikataba na akina Mangungo. Kwa vile Chancelor Bismark hakutaka kufanua hivyo, huyu Karl Peters akatishia kumudouble cross kwa kuuza wazo hilo kwa mfale wa ubeligiji ambaye alikuwa amshajichimbia Kongo. Kwa shingo upande ndipo Bismarck akakubali kuiweka ardhi yetu chini ya ulizi wa ujerumani lakini bila kuwa na mpaka wowote.

(2) Karl Peters aliendelea mbele zaidi na kumlazimisha Sultani wa zanzibar kuweka mkataba, tena wa nguvu, kuiruhusu ujerumani kuichukua pwani yote iliyokuwa chini yake. Mkataba huoo ndio uliosababisha vita ya Bushiri Bin Salim kule Pangani kama mnakumbuka historia ya darasa la nne. Sultani akaomba masaada kwa uingereza kumsaidia kuwazima wjerumani.

(3) Wakati Sultani akiomba msaada huo, Karl Peters alisonga mbele kwa kumshurutisha Kabaka wa Buganda naye kusaini mkataba ule ule wa akina Mangungo. Ni kutokana na hizo presha za karl Peters na maombi ya Sultani wa Zanzibar ndiyo maana Uingereza ilipokaa na Ujerumani na kupitisha Mkataba wa Heligoland-Zanzibar miaka mitano baada ya ya Mkutano wa Berlin.

(4) Kwenye mkutano wa Berlin, ajenda kubwa zilikuwa tatu:
(a) utaratibu kwa nchi ya ulaya kujitangazia eneo la Afrika bila kuingiliana, (b) utaratibu wa kushirikiana katika kutumia raslimali za maji kwa usafiri. (c) Kukubaliana kuhusu ndia ya ureno kumiliki eneo lote la kutokea Msumbuji hadi Angola (ikiwemo Malawi, Zambia na Zimbabwe)

Chini ya mkutano huo iliakubalika kuwa:

(A) Ni lazima nchi inayotaka kujimegea pande la Afrika ionyeshe kuwa inaweka utawala (law and order) na kutangaza mipaka ya eno lake pwani. Kwa vile Marekani na nchi nyingine za Scandinavia zilikuwa haziwezi kuweka talawa zao Afrika, ingawa zilihudhuria mkutano ule, ndiyo maana hazikuweka makoloni yao Afrika.

(B) Maji yote kwenye bonde la kongo hadi kwenye bahari ya hindi kati ya digrii tano kaskazini hadi mtu zambezi yakawa ya wote hiyo ikiwa ni pamoja na Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika, na Ziwa Nyanza

(5)Mwaka 1890, muda mufupi kabla ya Mkataba wa heligoland-Zanzibar kuwekwa sahihi, Uingereza iliweka tishiwa kwa ureno kuwa haiwezekani wamiliki eneo walilokubaliwa kwenye mktano wa Berlini kwa vile ineizuia Uingereza kuunganisha himaya yake kutoka cape town ahdi cairo. Kwa hiyo ureni iliwithdraw na kuavha eneo lote la Malawi, Zambia na Zimbabwe likiwa halina mmiliki isipokuwa sehemu ndogo ya Zambia na Zimbabwe ambazo zilikuwa zinamilikwa na Rhodes.

(6)Mkataba wa Heligo wa mwaka 1890 uliwekwa sahihi kwa kutambua kuwa maji yote ya ziwa Nyasa yalikuwa yanatumiwa na wote, wajerumani, wareno, wafaransa, na wabeligiji. wakati taifa la Nyasa linaundwa rasmi mwaka 1902, mfalme wa uingereza naye kwa kujua kuwa maji yale ni ya wote, alimtuma gavana kuwa himaya yake itakuwa ni magharibi na kusini ya ziwa hilo.

(7) Baada ya uingereza kutawala sehemu zote mbili- Malawi na Tanganyika, magavana wa nchi hizi walikubaliana kugawanya ziwa lile katikati baina yao kwa sababu za kiutawala, na hivyo kuondoa uhuru kwa mataifa mengine kulitumia (kufuatia mktaba wa Austria baada ya WW1). tatizo linalokuja hapa sasa ni namna mgawanyo huo ulivyobadilishwa na kufanya ziwa lote liwe la malawi, kwani jambo hilo lilifanywa na utawala wa kiingereza kwa sababu zao binafsi ambazo hazikubaliani na sheria za maji za kimataifa.

Tukijenga jukwaa la historia, nadhani tutapata uwanja mpana wa kujadili mambo haya kwa vile yanaingiliana sana.
 
Liwalo na liwe ,hakuna hili wal a lile ,mpaka ni katikati ya Ziwa ,vinginevyo patakuwa hapatoshi. Mimi nipo tayari kwenda mstari wa mbele ,je wewe ?
 
heligoland treaty haihusiani na ziwa Nyasa hata kidogo,hata Lake Chad ilikuwa hivyohivyo
 
Kichuguu,

Ziwa Malawi hebu soma hiyo Helgoland treaty halafu copy na ku-paste hapa maelezo ya mpaka wetu unapita wapi ndipo urudi hapa jamvini.

Mimi nimeyaonyesha hapa mara nyingi na sina sababu ya kuya-paste tena hapa labda unihakikishie kwamba huna au hujawahi kuyaona.

Kuhusu mpaka kubadilishwa baada ya World War I au II, hili si mjadala maana nalo ni kama hapo juu kwamba tumeshaliongea kwamba Tanganyika as mandate an trustee haikupaswa kuwa altered of anything bali kuwandaa watanganyika for self gorvenance na si kuchezacheza na mipaka yao.

Hivyo, kilichoguswa kuanzia 1920 hadi 1959 hakikuweza ku-rele out Heligoland treaty. Na hata kama hapo kulikuwa na mkataba wengi mnaotetea hili mnasema kuwa ilikuwa hivi ilikuwa vile bila kuonyesha text zilivyosema. Afadhali wewe kidogo una uelewa lakini wenzako wametumbukia katika mtego wa kusema mwaka 1929 kulikuwa na ramani fulani kisha mwaka 1938 kukawa na ramani nyingine! Hebu pima uelewa wa watetezi hawa! Toka lini kuchora ramani hii au ile kukawa justification kiasi cha kuijadili humu tukadhani ni comment itasaidia kuleta ziwa hapa.

Hivi mnapojadili humu mnadhani wamalawi hawayajui hayo yote na mnadhani ni vilaza totaly watabase kwenye hizo parctial details ambazo hata nisiye mwanasheria ninajua hazina mshiko.

Kwa wiki mbili tatu sasa, binafsi nimetafuta bila mafanikio kuona kama kuna hoja humu itatuonyesha uwezekano wa kupata ziwa Malawi.

Hebu tuleteeni hoja ambazo hata sisi humu na uelewa wetu mdogo hatuwezi kupinga ndipo tuamini kwamba ziwa tutalipata.
 
Huu mjadala wanaufanya kwa kiswahili au kiingereza? Kama ni kiingereza nina wasiwasi kuna uwezekano wa udhaifu wa watanzania kwenye hiyo lugha kutuathiri tukaishia kukubali kila wanachosema hawa jamaa. Hawa wawakilishi wa serikali ya Tanzania huwa siwaamini sana kwenye mijadala kwani huwa ni mabingwa wa kukaa kimya na kutikisa vichwa kana kwamba wameelewa.
 
Hii kutoka fb ya balozi wetu Malawi:
Patrick Lusiano Tsere

2 hours ago

Leo mkutano wetu wa mpaka umeanza na ulifunguliwa na Waziri Chiume wa Mambo ya nje. Ujumbe wetu tulikuwa 13 wa Malawi 20 na ushee, tena mzito haswa. Hotuba ya Waziri Chiume ilikuwa nzuri na iliyojaa ushauri mzuri kwetu sote. Kila upande ulitoa hoja kuhusiana na msimamo wake. Ingekuwa tuko chuoni na kama ni thesis basi ile ya Tanzania ingestahili PHD tena with distinction ilhali ya wenzetu ilikuwa inastahili pass ya kufutia machozi! Jamani inatosha nisiseme mengi. Ila Tanzania ina hoja nzito sana. Maana jamaa baada ya kusikia wamepigwaa na butwaa na mshangao. Maana data zetu zilikuwa mpaka na hati na ramani. Hio ndio habari yenyewe. Hivi sasa kila upande unapitia hoja na maelezo ya upande mwingine ili kesho tutoe feedback!
huyu balozi inabidi arudishwe nyumbani, naona diplomasia yake ni haba!
 
Kwa utajiri tulio nao, sioni ubaya tukawapa Wamalawi kale kaziwa. Nadhani tutakuwa mfano wa kuigwa.!
 
Unfortunately mimi sikufurahishwa kabisa na post hii hasa kama imetoka kwa balozi wa nchi kwa vile ni post ya kishabiki ambayo haina hata chembe moja ya diplomasia. Mtu huyu kama balozi wetu, anatakiwa awe mtu mwenye kujua maana ya diplomasia. Post hii inaweza kusababisha stalemate ambayo ndiyo tunayohitaji kuzuia ili kumaliza mpaka. Maneno mafupi tu kuwa ".........tumeanza majadiliano, na tumeweka kesi yetu mbele ya wenzetu na kutoa ushahidi wetu kuhusu msimamo wetu, tumewaacha nao watoe kesi yao na ushahidi wao......" ingetosha sana. Siyo kujidai kuwa tumetoa Ph.D thesis ya distinctition na wao hawakutoa kitu; huo ni upuuzi mkubwa sana kufanywa na balozi. Kwanza sijui kama kweli balozi huyu anajua uzito uliomo kwenye Ph.D thesis kwa vile sina uhakika kama kweli alishawahi kuifanya au kuisimamia!!

Post hii inaonyesha jinsi gani anavyotoa hoja zake; yaani kama mabalozi wetu wanafanya kazi kama vile wako vijiweni basi njia yetu inazidi kurefuka sana.

Mkuu halafu kwa nyongeza tu, balozi Tsere ndiye kiongozi wa juu kabisa kiserikali katika mkutano huo kwa upande wa Tanzania.

Kwa upande wangu nimependa yeye kutujulisha nini kinachoendela hata kama amekiuka taratibu za kazi yake.

Ametutia matumaini Watanzania kwamba kuna dalili za ushindi. Sisi tunataka pasu kwa pasu
 
All the best...tuepuke ujuaji tu utakaoleta matatizo kwenye namna ya kufikia muafaka
 
huyu balozi inabidi arudishwe nyumbani, naona diplomasia yake ni haba!

Huyu si Mwana diplomasia ni fadhila tupu hapo maana baba yake alitoa pesa mingi wakati wa uhuru,sasa wanalipa fadhila tu,ametokea ukuu wilaya ilala moja kwa moja kuwa balozi!!watu wana data zake koote alipopita ukizitaka ziombe zitamwagwa tu!ila sio mwana diplomasia!!
 
Kuhusu mpaka kubadilishwa baada ya World War I au II, hili si mjadala maana nalo ni kama hapo juu kwamba tumeshaliongea kwamba Tanganyika as mandate an trustee haikupaswa kuwa altered of anything bali kuwandaa watanganyika for self gorvenance na si kuchezacheza na mipaka yao.

Mbona Rwanda na Burundi zilimegwa wakati Tanganyika ni trustee territory? Je hazitambuliki?
 
Mbona Rwanda na Burundi zilimegwa wakati Tanganyika ni trustee territory? Je hazitambuliki?

Usichanganye mambo wewe Azipa.

Walioimega Rwanda na Burundi kutoka Germany-East Africa walikuwa ni League of Nations wala si Britain aliyepata kipande hiki tunachoishi na wala si Belgium iliyopata kipande ambacho sasa kinaitwa Rwanda and Burundi.

Hivyo, Belgium walipewa kile kipande kwa sababu tayari walikuwa wazoefu na eneo hilo kwani walikuwa wako Congo. Maana yake ni kwamba Belgium na Britain walikabidhiwa tu kuwaandaa watu kitendo kiitwacho Mandate na baadaye trusteship.

Hivyo, Belgium hakuwa na haki ya alteration of any sort kama ilivyokuwa kwa Britain hapa Tanganyika.

Najua unaweza wewe au mwingine akaniuliza, mbona Burundi na Rwanda zilikuja kwa njia ya mabadiliko wakati wa trusteeship?

Ni swali zuri na hata ulilouliza ni swali zuri, yaani maswali yanayodadisi. Hii ni JF thinkTank. Kujibu swali hili ni hivi ukweli ni kwamba hali ya utusi na uhutu ililazimisha kuwe na mataifa mawili na wakimbizi wa uadui huu walianza tangu mwaka 1959, miaka minne kabla ya uhuru tena wakati huo ikiwa nchi moja iitwayo Rwanda-Urundi!

Wazo la kutenganisha lilikuwa halikwepeki lakini Belgium haikuwa na option au haki ya kutenganisha makabila haya kuwa mataifa mawili tofauti. Ndipo ilibidi Belgium kuwavumilia Rwanda-Urundi kwamba siku ya kupata uhuru zijitenge rasmi. Hivyo juhudi za uhuru zikawa zinafanyika ikijulikana kwamba siku ya uhuru itazaa mataifa mawili.

Na kweli ikawa hivyo kwani July 01, 1962 uhuru ukatangazwa kwanza kwa taifa la Rwanda-Urundi, kama kitendo cha kwanza na kitendo cha pili kikawa kutangaza mataifa mawili tofauti yaani Rwanda na Burundi.

Hivyo bendera ya Belgium ikateremka kuashiria Belgium inaachana na utawala wa taifa liitwalo Rwanda-Urundi. Lakini kupandisha bendera zikapandishwa bendera mbili yaani za Rwanda na Burundi.

Ndiyo maana ukitazama hata historia utaona siku ya uhuru wa Rwanda ni ileile na ya Burundi yaani July 01, 1962.

Tuache uvivu wa kusoma tupekue kabla ya ku-broadcast.
 
Usichanganye mambo wewe Azipa.

Walioimega Rwanda na Burundi kutoka Germany-East Africa walikuwa ni League of Nations wala si Britain aliyepata kipande hiki tunachoishi na wala si Belgium iliyopata kipande ambacho sasa kinaitwa Rwanda and Burundi.
Unajichosha tu kuandika mambo ambayo hayapo. League of nations wamege kwasababu zipi? Ngoja nikueleweshe;

Uingereza ilimshinda Ujerumani kwenye vita ya kwanza ya dunia. Uingereza ikachukua eneo lote la Mjerumani ikiwepo Rwanda na Burundi. Kisha Uingereza ndo ilimpa Mbelgiji.

Main article: British East Africa
The mandate to administer the former German
colony was conferred on the United Kingdom under
the terms of the Supreme Council of the League of
Nations. With the concurrence of the Supreme
Council, the United Kingdom transferred the
provinces of Ruanda-Urundi, in the northwest, to
Belgium.

http://en.m.wikipedia.org/wiki/History_of_Tanzania
 
Huyu si Mwana diplomasia ni fadhila tupu hapo maana baba yake alitoa pesa mingi wakati wa uhuru,sasa wanalipa fadhila tu,ametokea ukuu wilaya ilala moja kwa moja kuwa balozi!!watu wana data zake koote alipopita ukizitaka ziombe zitamwagwa tu!ila sio mwana diplomasia!!

Skills4Ever,

..lakini kabla ya kuwa mkuu wa wilaya, Balozi Patric Tsere alifanya kazi wizara ya mambo ya nje, mambo ya ndani, na mkurugenzi mkuu AICC. baada ya aicc aligombea ubunge karatu na kushindwa na Dr.Slaa. binafsi nadhani ni kati ya mabalozi ambao wametimiza vigezo vya kuteuliwa nafasi hiyo.

..kuhusu ku-post kwenye facebook, kwa kweli hajatoa details zozote zile zaidi ya kuelezea how good he felt kuhusu hoja za Tanzania. angeanza kuchambua in details presentations za Malawi vs Tanzania then we would have something to say.

..pamoja na hayo, majadiliano yanayoendelea ni too sensitive, hivyo Balozi Tsere anapaswa kuwa mwangalifu zaidi, na matamshi anayoyatoa.
 
[h=6]Hii kutoka fb ya balozi wetu Malawi:
Patrick Lusiano Tsere
[/h]2 hours ago

Leo mkutano wetu wa mpaka umeanza na ulifunguliwa na Waziri Chiume wa Mambo ya nje. Ujumbe wetu tulikuwa 13 wa Malawi 20 na ushee, tena mzito haswa. Hotuba ya Waziri Chiume ilikuwa nzuri na iliyojaa ushauri mzuri kwetu sote. Kila upande ulitoa hoja kuhusiana na msimamo wake. Ingekuwa tuko chuoni na kama ni thesis basi ile ya Tanzania ingestahili PHD tena with distinction ilhali ya wenzetu ilikuwa inastahili pass ya kufutia machozi! Jamani inatosha nisiseme mengi. Ila Tanzania ina hoja nzito sana. Maana jamaa baada ya kusikia wamepigwaa na butwaa na mshangao. Maana data zetu zilikuwa mpaka na hati na ramani. Hio ndio habari yenyewe. Hivi sasa kila upande unapitia hoja na maelezo ya upande mwingine ili kesho tutoe feedback!

Tunashukuru kwa hoja nzuri kama upande wetu utakuwa umewasilisha kwa kiwango hicho cha Phd, ila hapo kwenye RED ninaauliza, hizo Ramani na hati nani alizikabithi kwetu? source yake ni ipi? ni ramani ya mkoloni, ya OAU, ni ya Banda au Nyerere?au Latitude na Longtude za Membe? Ila naombea presentation yetu ilete majibu ya Phd.
 
Tunashukuru kwa hoja nzuri kama upande wetu utakuwa umewasilisha kwa kiwango hicho cha Phd, ila hapo kwenye RED ninaauliza, hizo Ramani na hati nani alizikabithi kwetu? source yake ni ipi? ni ramani ya mkoloni, ya OAU, ni ya Banda au Nyerere?au Latitude na Longtude za Membe? Ila naombea presentation yetu ilete majibu ya Phd.....

Wana-JF,

Thread zote hizi na masuali tunayouliza humu hakika watu wote wa nchi hii wangekuwa wanasoma humu JF basi ndipo wajue kwamba kipindi cha kutuletea cheap answers kwa masuala yanayotakiwa hoja nzito kimepitwa na wakati.

Ona kama huyu suali lake hapo kwenye RED, unadhani unaweza kukurupuka kujibu kirahisirahisi.

Ndilo funzo kwa serikali na taasisi zake kwamba sasa kila sehemu kuna wataalamu wa jambo lake hivyo wakikurupuka wataumbuka na wao hoja yao itakuwa kusingizia watu kwamba hawana uzalendo.

Hoja ambayo nayo vilevile lazima itoke kwenye vichwa vya wavivu wa kufikiri.

Mimi naamini hata wakati ule Kamuzu Banda alipomletea Nyerere ramani halafu Nyerere akaishia kumkejeli bila kutoa wazo lolote, ingekuwa ni sasa hivi na JF ipo ninaamini watu wangeshuka na Nyerere bila kumuonea haya kama wanavyoshuka na JK sasa.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Back
Top Bottom