Makubaliano ya ovyo hayawezi kuleta mikataba mizuri

Moyo wa nchi

Member
Jun 21, 2023
81
127
Habari zenu,

Ingawa sikubaliana na hoja za utetezi za viongozi wa serikali na ccm yao kwamba huu SI mkataba Bali ni makubaliano.

Ni ujuha kusubiria embe chini ya mkorosho, Hawa wapuuzi wanaamini kwamba hata kama haya Wanayoyaita makubaliano yatakuwa ya kijuha basi matokeo yake yatakuwa mazuri hivi hizi ni akili au matope?

Tangu lini bunge linajadili na kupitisha au kuridhia makubaliano?
Hivi kisheria nini tofauti kati ya makubaliano na mkataba?
Je, Haya makubaliano ukomo wake ni lini?

Hivi ni makubaliano ya aina Gani ambayo hayavunjiki hata kikitokea kikwazo chochote?

Je, Haya makubaliano ni kati ya Tanzania na nchi Gani?
Kwanini makubaliano haya yavunje sheria mbalimbali za nchi?
Hivi ni mikataba mingapi tumeingia kama nchi na hatujawahi kuisikiawala kuiona kwani nini huu tulazimishwe kupewa elimu ambayo tumekataa?

Hawa viongozi wetu wasaliti wameamua kutumaliza kabisa, na kwa umoja wetu tumekataa huu ujuha.

Kuna watanzania wachache wako nyuma ya uhaini huu kama wataendelea kukaza mafuvu tutaanza kuwataja mmoja baada ya mwingine.

Kwa moyo wangu wote napenda kumpongeza au kuwapongeza wale wote waliosaidia kuvuja kwa hii takataka ya mkataba wa bandari.

Watanzania tutawaombea ingawa hatuwafahamu, mmefanya uzalendo, mmeiokoa Tanganyika nanyi MUNGU atawaokoa na kuwalinda.
 
Kwa moyo wangu wote napenda kumpongeza au kuwapongeza wale wote waliosaidia kuvuja kwa hii takataka ya mkataba wa bandari.
Yaani unaonesha huna uelewa wa lolote.
Mkataba Haukuvuja, uliwekwa hadharani na kupelekwa Bungeni.
Bunge limeupitisha.
Lakini vichwa maji kama mimi na wewe tunawatukana viongozi.
Nashindwa kujua udhubutu huu munaupata wapi?
Serikali inawajibu kwa taifa kutafuta njia za kuendesha nchi na kuongeza mapato.
Kutafuta na kuleta muwekezaji si kazi nyeopesi.
hakuna Muwekezaji anayetowa sadaka pesa zake, n lazima iwepo win win
Unadhani mambo haya ya kitalamu yanajadiliwa kama unavyojadili wewe?

Mimi nadhani uwe na ADABU tuu kuwaheshimu wale Viongozi walioko Juu ambao wana Uwezo kukusaka na kukuchukulia hatua ,wakitaka.
 
Toka October 2022 mkataba ulisainiwa huko Dubai kama ni uwazi kwanini sio tangu kipindi hicho?. Matokeo yake June 2023 ndio bunge linapekekewa mkataba ambao tayari umesainiwa?
 
Back
Top Bottom