Makubaliano ya kutumika kusajili health facility

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
156
Wadau habari zenu?
Naomba ushauri wenu.
Mimi nafanya kazi katika kampuni fulani kama Medical Officer.
Nimekuta health facility haijasajiliwa, nimefuatilia ili isajiliwe na mchakato ulipofika ni pazuri.
Moja ya requirement ya registration ya health facility ni kumtumia Medical officer (ambaye atajulikana kama Medical Officer in charge) ku-justfy registration na huyo Medical Officer in charge hatakiwi kuwa anafanya kazi serikalini na hatakiwi kuwa registered kuwa mdau wa health facility yoyote ile.
Nami ndiye Medical Officer pekee katika hiyo health facility ya kampuni hiyo.
Hadi hapo ni dhahiri kuwa mimi nd'o nitatumia Qualification yangu kusaidia katika usajili wa hiyo health facility.
Swali (ambalo nd'o kiini cha kuomba ushauri): Niwaambie wanilipe kiasi gani kila mwezi kama gharama ya kunitumia kusajili hiyo health facility? Kwa sababu nisipotumika mimi atatumika mwingine ambaye itabidi wawe wanamlipa kila mwezi, au ningekuta kuna mwingine alishatumika kusajili hiyo health facility mimi ningefikia kutibu na kushughulikia masuala mengine ya afya.

Nikishatumia jina na vyeti vyangu kusajili ujue siku nikihitaji nami kufungua kituo cha afya itabidi nitumie jina na vyeti vya mwingine ambaye nitakuwa namlipa pesa kila mwezi badala ya kutumia jina na vyeti vyangu!

Naomba kuwasilisha!
 
Back
Top Bottom