Makosa yanayofanywa na wanaume wengi kwenye kumvutia mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kuamini kuwa na mwanamke anavutiwa sana na mwonekano tu
Kwa sisi wanaume tunavutiwa na mvuto zaidi, lakini mwanamke anavutiwa nawe kutokana na vile anavyojisikia akiwa nawe. Akijisikia amani, usalama kujiachia kwako basi unampata/ kumtunza kirahisi.

Lakini usipomfanya mwanamke ajisikie usalama na amani kwako, hata uwe na mwonekano gani/ au na vitu gani hawezi kukaa nawe, labda kama anakutumia kwa vitu ulivyo navyo.

Kwa mwanamke anayekupenda na ambaye yupo tayari mjenge maisha, mara nyingi hatojali mwonekano wako, zaidi ya vile unavyomfanya ajisikie kwako. Hivyo usijali sana kuhusu mwonekano wako, au kama huna gari au nyumba cha msingi ni kujiboresha kila siku.

Sababu kadri unavyokuwa na mwonekano mzuri ndivyo utazidi kuvutia wanawake wengi zaidi na kumpata umtakaye, lakini ili kumtunza ni muhimu kuangalia vile unavyomfanya ajisikie akiwa nawe.

Kuficha/ kumdanganya mwanamke malengo yako
Sababu ya kuogopa kumkosea au unaogopa utamkosa ukimwambia ukweli kuwa unamtaka. Yeye atakuona rafiki tu. Mwisho wa siku utaumia mana utakuwa unaona wivu akiwa na wanaume wengine. Usije ukaficha unavyojisikia kwa mwanamke, haijalishi unamtaka na unaogopa kumpoteza kiasi gani.

Mwanaume vaa ujasiri na mtokee unayemtaka, lakini kuwa makini, usije ukawa omba omba wa penzi au kumwambia mwanamke kila kitu na kiasi gani unampenda mapema. Nenda naye taratibu.

Pia usijifanye rafiki halafu baadae ndio mtakuwa wapenzi. Mara nyingi mahusiano ya hivi mwanamke ndio mwenye nguvu na maamuzi. Heri uwe kwenye mahusiano ambayo wewe ndio mwenye nguvu na maamuzi.

Kutojiamini
Mwanaume unapimwa kwa ujasiri wako. Mwanamke anapenda awe na mwanaume jasiri zaidi kati ya wote wanaomtongoza. Amini kwamba we unajiamini kuliko huyo mwanamke.

Wanaume wengi wanaona mwanamke kwa nje na kumuogopa sababu anaonekana kujiamini, lakini ukweli ni kwamba wanawake ni waigizaji wazuri. Usiwaogope. Pia wanatarajia wewe utakua unajiamini zaidi kuliko wao.

Kumuachia mwanamke uongozi
Hiki ni kitu namba moja wanawake hawapendi. Kuachiwa uongozi na mwanaume wake. Na kuonesha kuwa hapendi, ataanza kukununia/ kuleta drama zisizo na msingi. Au unamfanyia hiki anasema sio, unamfanyia kile bado hana shukrani na anakulaumu.

Na wewe ili kuepusha makelele unamuuliza “nikufanyie nini uridhike” naye kwa kuwa hajui kitakachomridhisha anakuambia “chochote utakachoona sawa”/ “sijui mimi”(huku kanuna/kakasirika).

Yote hayo maana yake umeacha kumuongoza. Umemuweka katika nafasi ambayo hata yeye mwenyewe haelewi jinsi ya kujielezea. Cha kufanya ni kuanza kuwa kiongozi wake kama ulivyokua kipindi unamtongoza.

Onesha uongozi wako kwenye, kumuongoza na kwenda utakapo, kuongoza mazungumzo, kuchagua mpike nini na kumuongoza atoke kwenye drama zake.

Kuamini wanawake wote ni waongo/ wabaya/ malaya/ wachunaji
Wanawake wa hivyo wapo lakini sio wote. Kama umekutana na wanawake wa hivyo, kabla ya kuwalaumu jichunguze kwanza wewe. Angalia kama imani yako inakuruhusu kuwa na wanawake unaowataka.

Ndege wanaofanana huruka pamoja. Ukibadili imani yako kwanza utaweza kukutana na wale uwatakao. Pengine uliumizwa sababu ulikua haujui tofauti za kupenda kati mwanamke na mwanaume. Ni muda wa kujifunza.

Kudhani mwanamke anafikiri kama wewe
Si tunafikiri moja kwa moja, hatupindishi mambo, lakini mwanamke anafikiria kitu kimoja kwa namna tofauti tofauti. Huwezi mwelewa ufikiri wake. Sisi tunafikiri, huyu nimemnunulia vocha, nimempa hela ya kula na niliwahi kumtoa out hivyo inabidi anipe tunda, lakini yeye anafikiria kivingine kabisa.

Ndio maana ukifikiria hivyo na kumuomba penzi atakwambia ngoja afikirie kwanza, au atakuzungusha wakati we unaona ni jambo rahisi na dogo. Tambua kuwa wanafikiria tofauti, ila wanawapenda kuongozwa, ili uwaepushe na kufikiria sana.

Kutomjali
Muda mwingine tunajifunza usimjali sana mwanamke, ni jambo zuri kwa kipimo chake. Usipomjali kabisa ukiamini atakupenda zaidi, ataona huna malengo naye. Akitokea mtu mwingine wa kumjali zaidi na anajua kumfanya ajisikie mwanamke, atakuacha.

Sawa usijali sana kupitiliza lakini nimejifunza kuwa ili kuwe na mahusiano imara, lazima ujali vitu vidogo vidogo ambavyo hubomoa au hujenga mahusiano.

Kubweteka
Unategemea kuna mtu atakuja kukuokoa lakini miaka inazidi kwenda. Haujiboreshi ili kupata unachotaka miaka inazidi kwenda. Haujifunzi jinsi ya kuboresha mahusiano yako miaka inazidi kwenda. Huongei na wanawake na huna wa kuishi nae/kuoa miaka inazidi kwenda.

Unakaa kusema wengine lakini hujiangalii miaka inazidi kwenda. Una mwanamke lakini mpo mpo tu miaka inazidi kwenda. Haumridhishi mwanamke wako miaka inazidi kwenda. Mwisho wa siku unaachwa, unaona wanawake wote walewale tu, au unakosa mwanamke halafu unaona wanawake wote walewale tu.

Epuka kubweteka.
 
Ngoja nitarudia kusoma nielewe vizuri, halafu nijaribu kuapply nione kama itafanya kazi...
 
Haya makitu mna copy na ku paste...ground mambo ni tifauti
 
Back
Top Bottom