Makongoro Nyerere apata ajali ya gari Babati

Huyu ndo yule aliekuwa anaongea vitu vya ajabu kwenye kampeni?

Mkuu wakati mwingine tujaribu kuwa waungwana kidogo, habari hii kama ingehusu masuala ya,
harusi au sherehe kweli - lakini linapo kuja suala la ajali au kifo - tusitumbikize utani. Natoa ushauri tu kwa nia njema.
 
Atajua mwenyewe. Unafiki siwezi.
 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.

Mwananchi
 
Huyo alikuwa amelewa,Pia alikuwa ana speed...adhabu yake alipe ng'ombe wa watu na kondoo..pia POLISI-MAGAMBA wa mpe speeding ticket ili iwe fundisho kwa vigogo wa magamba
 
Jamaa kaua ng'ombe saba na kondoo mmoja, alikuwa anaendesha gari gani na speed ngapi? Mimi ng'ombe mmoja tu alitaka kuleta balaa na wala hakufa.
 
makonogro..jpg

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara kwa binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.

Chanzo: MWANANCHI
 
Duh...pole mheshimiwa.

Huyo mchunga Ng,ombe anaitwa William German....ni Mzungu ama?
 
Back
Top Bottom