JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Posted by JokaKuu | May 15, 2012
..kwa jinsi nilivyomuelewa Makongoro Nyerere kutokana na maelezo yake anakwenda ktk bunge la EAC kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoa pingamizi lake ktk masuala ya ARDHI, na kupigania kuanzishwa kwa SHIRIKISHO LA KISIASA la Afrika Mashariki.
..Makongoro Nyerere anafikiri kinachohitajika ni wa-Tanzania "kuelimishwa" ili kuondoa "hofu" waliyonayo kuhusu masuala ya ardhi. anadai kwamba wa-Tanzania hatuna "elimu" juu ya "matumizi endelevu" ya ardhi na ndiyo maana tuna "hofu" kuhusu raia wa EAC kuwa na haki ya kumiliki ardhi ya Tanzania.
..Kuhusu kuanzishwa kwa Shirikisho, Makongoro Nyerere anadai tunapaswa kuanzisha shirikisho la kisiasa ili nchi za Afrika Mashariki ziwe na "sauti moja."
..mimi nadhani wabunge walikosea ktk kumchagua Makongoro Nyerere kuwa mwakilishi wetu kwenye bunge la EAC. nasema hivyo kwasababu msimamo alio nao na mambo aliyoazimia kuyatetea ktk bunge la EAC ni kinyume na matakwa ya wa-Tanzania kama walivyoelezea ktk Tume ya kukusanya maoni ya Prof.Samwel Mwita Wangwe.
..inatia wasiwasi sana lakini sidhani kama wenzetu[makongoro, etc] wanajifunza kutokana na matatizo waliyonayo majirani zetu kuhusu suala hili la ardhi. Kenya wamekuwa na migogoro isiyokwisha kutokana na sera zao mbaya za umiliki wa ardhi. Pia mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda chanzo chake ni ukabila na matatizo ya ardhi. Sijui kwanini wanasiasa kama Makongoro Nyerere wanakosa umakini na kauli zao kuhusu suala la ardhi hapa Tanzania, wakati there r lessons to learn all around us.
..kuhusu Shirikisho malengo ya Kenya na Uganda ilikuwa 2013 tuwe na shirikisho la kisiasa. Mimi nadhani mawazo hayo ni ya hatari kabisa ukizingatia what it takes kuunda shirikisho hilo. Sijaona duniani shirikisho la kisiasa linalotumia sarafu tofauti za fedha, but that was what was about to happen in East Africa.
..kwa mitizamo yake nadhani Makongoro Nyerere amepotoka kimtizamo na atakuwa mbunge wa Kenya na siyo wetu wa-Tanzania.
mnaweza kusoma zaidi kupitia linki hii hapa : Makongoro: Tusihofie Shirikisho | Gazeti la MwanaHalisi (Makongoro: Tusihofie Shirikisho | Gazeti la MwanaHalisi)
NB:
..Alhaji Adam Kimbisa amesikika akisema kwamba atatetea msimamo wa wa-Tanzania kuhusu ardhi kwa nguvu zake zote.

Last edited by a moderator: