Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,770
2,092
makonda5.jpg

MAKONDA AAINISHA MPANGO KAZI WA VIPENGELE SITA: LETS MAKE ARUSHA GREAT AGAIN!

April 8, 2024
Arusha


⦁ Mapokezi yamenitia moyo wa kuwa mtumishi mwema na mtetezi wa wanyonge. Kamwe sitaungana na fisadi kukandamiza haki zenu, nitakuwa sauti yenu mpaka ukamilifu wa dahali

⦁ Nawashukuru kwa maombi. Kwa dua njema mlionifanyia. Nimekoswa koswa mara tatu kupoteza maisha, na nawaambia, sitakufa bali nitaishi. Niyasimulie matendo makuu ya Mungu.

Nina mambo au mawazo sita. Lakini lazima nifanye kwanza ziara mniambie, ili yale tunayowaza sisi yafanane na majibu ya changamoto zenu. Nakuja kwenye wilaya zote sita tukutane. Ili kusudi tupate sauti moja.

La Pili: Hakuna maendeleo bila umoja. Tukishikamana bila kujali dini, kabila, chama, tutapiga hatua. Mkoa usiwe wa malumbano ya kisiasa, bali mkoa wa kujenga uchumi imara, na wa biashara kwa watu wake.

⦁ Sijaja kukandamiza wanasiasa. Sijaja kutangua torati. Wapinzani mkitaka kunishirikisha mnishirikishe. Mkitaka hata mafuta kama tunaweza tutachangia.

Jambo la tatu, najua Arusha ni mji wa kitalii. Rais Samia ameipendelea Arusha, hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje aungane nanyi. Takwimu za serikali za sekta ya utalii zinatofautiana kati ya Maliasili, na RAS wa Mkoa, na Bodi ya Utalii. Unajiuliza, hawa watu si ni serikali moja ? Which means vyumba hakuna! Kumbi za mikutano hakuna. Tutajenga kumbi mbili kubwa za mikutano. Tutajenga apartment ya vyumba 400, na kiwanja cha mpira cha watu 30,000. Tuache siasa za kunyoosheana vidole, hazituingizii pesa.

Jambo la nne. Ninalo tangazo jema kwa yeyote anaedai haki yake: Kwa neema na mapenzi ya Mungu utaipata. Kama niko nimekanyaga mahali hapa, na nina kibali cha Rais, basi haki yako utaipata. Hujui kusoma, hujui kuongea ukaeleweka, huna hela, nitakulinda na kukupigania!

Jambo la tano. Watendaji na watumishi wote Arusha popote ulipo, funga mkanda! Mkurugenzi, RPC, Mkuu wa Idara, DC, Uhamiaji, kaa kwenye kiti chako ueneee. Habari ya kutumia madaraka kuwakandamiza wanyonge, kupendelea wenye pesa imefika mwisho. Kwenye idara yako kama huwakudumii wananchi, cha mtema kuni utakiona.

⦁ Arusha tembeeni kifua mbele. Ya Kwamba Mtaheshimika kwa utu wenu, sio pesa, elimu wala connection. Wanaosema niketolewa uenezi, nimeletwa u RC, sasa CCM nilikuwa nasema wafanye wengine, huku nafanya mwenyewe. Ofisi yeyote ukienda wakikuhudumia vibaya njoo kwangu. Hospitali ukijibiwa vibaya, Polisi wakikunyima dhamana, njoo kwanguuuu... Silogeki! Hofu iliondoka na kitovu waliponikata...

⦁ Jambo la sita: Kamishna wa ardhi NJOO HAPA! Una miezi mitatu kumaliza migogoro ya ardhi. Mnongoza kwa rushwa! Na msijioendekeze kwangu kwa kunipa kiwanja, Arusha viwanja ninavyo. Ardhi ni kilio namba moja...

⦁ Afisa Mipango Miji NJOO HAPA! Mnazalisha squatter! Hakuna mipango miji, mmeshuhudua inajengwa bypass lakini hamkwenda mkapanga na kupima viwanja kuwe na barabara zinazopitika. Mnashinda kule Bulka na Sanawali kwa sababu kuna rushwa. Sasa una miezi mitatu tutakuita utoe ripoti umekuta migogoro mingapi, umetatua mingapi, umekuta watu wangapi hawana hati, umetoa hati ngapi. Na, umejipangaje kuhakikisha migogoro mingine isitokee... Migogoro ya ardhi inasababishwa na nyinyi wataalam wa ardhi! Mtendaji, Mtumishi, usipojipanga tunakupanga!

⦁ Uhamiaji: Mtu ana nyaraka zote, kwa nini passport ichukue siku 14? Na foleni ya Namanga foleni masaa matatu. Natka iwe mwisho dakika 60!

⦁ Mabango kila mahali, mara masaji, mara dawa za kienjeji, hapana. Tunataka screens. Watu wanatushangaa.

⦁ Sisi ni matajiri kuliko wanaokuja kutuhurumia! Maji Arusha yanatoka matope, na kuna suala la bili kubambikizwa. Zinakuja kufungwa mita za pre-Paid.

⦁ Ndugu zanguni, mambo ni mengi. Tutakaa mtanambia mnataka RC wa aina gani lakini kamwe sitawasaliti. Maombi yenu ndio yananiweka hapa. Wajane, vijana, wazee wananambia endelea. Sitawaangusha. Sitalumbana na mtu. Mwenye wazo la kutengeneza ajira, mwenye wazo la kujenga uchumi, kuboresha Arusha, mlango uko wazi.

⦁ KIla anaekuja Arusha apokelewe na kikombe cha kahawa. Ni mji unaotupatia pesa nyingi sana, hatuwezi kuuacha bure. Lets make Arusha Great Again.

⦁ Najua Yapo mambo ya Stendi. Ya soko. Ya boda. Ya dala dala. Ya Tatu Mzuka. Ya bajaji. Ya Wadudu. Nipeni muda.

⦁ Tarehe 12 tutampokea Rais katika tukio kubwa la kumuenzi Hayati Sokoine aliyefanya kazi ya heshima katika taifa hili. Ndio maana mimi ni mchanganyiko wa mtoto wa masai, wa jeshi, wa kisukuma... Sieleweki kwa sababu Mungu amejaa ndani yangu. Nimechukua combination zote nzuri ndo maana pa kunyooka tunanyooka kweli kweli.


⦁ Nimeongea na RPC tunaenda kuongeza nguvu ya ulinzi Arusha, maduka hayafungwi saa 11, saa 12 mbili. Zinakuja camera, taa za kutosha, patrol za baskeli za polisi, pikipiki, rescue team, mpaka helicopter za patrol. Kuhakikisha mnalindwa barabara.

⦁ Mungu wangu na awabariki sana
 
Huyo ndiye Makonda Mwamba kama Mwamba.kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara. Mtu aliyetangaziwa mwisho na Maadui zake lakini Mungu akautangaza mwanzo wake wa ushindi wa kishindo.kiongozi aliyeinuliwa na Mungu na kupewa kibali mkononi mwake.kiongozi mwenye ushawishi na anayependwa kama pesa. Kiongozi anayechanua muda wote utafikiri bustani ya kitalii.
 
Makonda kwa kuongea na kupanga tu, anaweza kweli kweli...

Lakini, baada ya muda jaribu ku-quantify matokeo ya vitu vyote anavyovitaja, hakuna matokeo...
 
Huyo ndiye Makonda Mwamba kama Mwamba.kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara. Mtu aliyetangaziwa mwisho na Maadui zake lakini Mungu akautangaza mwanzo wake wa ushindi wa kishindo.kiongozi aliyeinuliwa na Mungu na kupewa kibali mkononi mwake.kiongozi mwenye ushawishi na anayependwa kama pesa. Kiongozi anayechanua muda wote utafikiri bustani ya kitalii.
Acha ushoga kijana wa kinyiha toka Mbozi. Kumshabikia Zerobrain ni kujishusha thamani. Hakuna kitu atakusaidia
 
Huyu jamaa anajua Kula pesa ya umma

Pesa anaanza kupiga hapo katika ziara, atapiga pesa binafsi mno mbali na gharama za msafara
 
Hivi napenda kujua, wakuu wa mikoa Huwa wanapokelewa na wananchi wanaporipoti kazn???
 
Watu wa TISS ni kwanini mnashindwa kumwamba Boss wenu Rais Samia kuwa huyu mtu Paul Makonda hafai na kama anampenda sana basi amtupe tu huko Ubalozini akapumzike? Nimeangalia Video Clip yake akiwa anajitambulisha huko Mkoani Arusha alikotupwa baada ya Kufeli katika Uenezi nikagundua kuwa Kisaikolojia ana tatizo Kubwa mno la Kiakili na huenda Yeye hajijui na hata Wanamzunguka nao hawajui.

Makonda hakuna Mkoa ambao unatakiwa uwe nao makini na uende nao kwa Step kama huo wa Arusha ulipo. GENTAMYCINE pamoja na Usela Nnya wangu wote, Ujanja na Ubabe wa Kimusoma (Mkoani Mara Kwetu) nikienda huko huwa nakuwa Mpole hutoamini kwani nimeishi huo Mkoa, naujua na Watu wa huko Kiasili huwa HAWABIPIWI na UKIWABIPU tu haraka sana wanakupigia.

Ukiwa Mwenezi nilikuambia na Uzi upo kuwa hutodumu hapo hata ndani ya Miezi Sita na kama Kawaida yao au Kawaida yenu baadhi ya watu hapa JamiiForums yakanipuuza GENTAMYCINE lakini kile kile nilichokitabiri juu ya Paul Makonda kimetokea.

Haya Makonda na leo tena nakwambia kuwa hata huko Arusha ulikopelekwa ni Kimkakat zaidi ili Watu wamalize Shughuli mapema kwani tayari umeshaonekana ni tatizo halafu umeshajulikana kuwa kuna Mtu huwa unajifanya Kumpenda mbele za Mic za Media ila ukikaa Vijiweni Kwako na Washkaji pale Mbezi Beach na Masaki huwa Unamkashifu na Unamdharau hakuna mfano na ukimsifia Baba yako wa Hiari aliyemaliza safari yake 2021.
 
Back
Top Bottom