ntemintale
JF-Expert Member
- Sep 6, 2016
- 952
- 1,872
Paul Makonda ni Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi. Bila kuathiri Muundo wa Utumishi Serikalini, yeye Makonda ni Kiongozi wa Chama Cha Siasa Kama ilivyo kwa Chadema, TLP na CUF. Kwa hiyo chain of Command ya Utendaji wa Serikali haimtambui Mwenezi wa Chama Cha Siasa kuwa ni Reporting Unit kwenye Chain of Commnd ya Serikali.
Kitendo cha kuwasimamisha hadharani watumishi wa Serikali na kuwahoji Kisha kutoa maelekezo na hukumu ni Kinyume cha sheria kanuni taratibu za Utumishi na utawala bora.
Tutafakari kidogo, Je mwenezi wa Chadema, CUF, TLP na vyama vingine navyo vikiamua kuwahoji Watumishi hadharani, tutakuwa na utaratibu wa aina gani?
Serikalini kuna taratibu zilizo wazi za kupeleka malalamiko na mamlaka za kinidhamu zipo kutenda haki ikiwemo Kukata Rufaa.
Hizi Drama za Makonda kwa Watumishi zina lengo lipi. Kumbuka hata watumishi wa Serikali nao ni watu na wana haki sawa ya kuheshimiwa na wajibu wa kutenda haki