Makonda: Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania wala Mwenyekiti wa CCM

Sanaa na usanii!!! Wako karibu na wananchi baada ya kuona cdm inanyemelea ikulu! Daa siasa kweli si hasa.
 
Yani kinachonikera UVCCM ni utitiri wa matamko, upuuzi unaofanywa chadema nao wameuchukua, sentensi za Dr Slaa tuna taarifa n ooh tuna nyaraka naona unahamia UVCCM. Pmakonda mimi na wenzangu tumeelewa unachojaribu ku_ insinuate but you are too low and worthless scrotum
Tumia busara kumjibu kaka, hutapoteza kitu.
 
Last edited by a moderator:
1017328_645316442198554_899216478_n.jpg
 
mleta uzi ujajuwa kuwa mti weny matunda ndio upigwao mawe??

Ni sawa najua kwamba mti wenye matunda siku zote ndio hurushiwa mawe!
Swali langu la msingi hapa ni kwanini makosa au madhaifu ya Kikwete na serikali yake anahusishwa Lowassa,je ni kweli nguvu ya pesa aliyonayo Lowassa yaweza kuwa ndio sababu ya serikali ya Ccm chini ya mh Kikwete kushindwa kuchukua maamuzi magumu na kuwawajibisha baadhi ya viongozi waandamizi kwa kushindwa kwao ktk kutumikia wananchi?

Mfano mawaziri mizigo waliotajwa kushindwa kuwajibika ipasavyo ktk nafasi zao kwa wananchi,je mh Lowassa anahusika vipi kwa uteuzi wao hata jana tukamsikia kiongozi mmoja wa Ccm Paul Makonda akimtuhumu Lowassa kwa kudai kuwa anatumia pesa za Rushwa kumuhujumu Nape na Kinana?
 
Makonda amechoka na amechoshwa na wakuu wake.wakubwa wa ccm ni waoga wanabweka awangati,nasema hata kama Makonda kahandikiwa ameonekana anauwezo wa kusoma na kusema.kukomaa au kuoneana aibu ndiyo umasikini tulionao ktk nchi hii leo.nampongeza makonda.
 
chama cha mizigo (ccm) kupitia kwa kijana wake paul makonda kimesema kuna watu (hakuwataja majina) ndani ya chama wanaobeza na kufifisha juhudu za nape nauye na kinana. makonda amesema watu hao ambao ni wazee wastaafu wanapanga kile alichokiita 'uhaini'. pia akasema kijana yoyote makini hawezi kubeza kazi ya nape wala ya kinana.

Jamani Kiukweli Hivi Kitendo cha Kinana hapo ktk Picha Nae Kujifanya Anaendesha Sijui hicho Kigari cha Hao Watoto Ndiyo Inamaanisha Nini? Hiyo Ndiyo Siasa? Logic behind hapo ni Nini? Nilikuwa Mgumu Kuamini Upuuzi wa Chama ila Sasa Naanza Kushawishika na Upuuzi Wake. Na Uwezo Wangu Mdogo wa Siasa Sidhani Kama Watanzania Wanataka Unafiki huo wa Kinana wa ktk Picha hiyo bali Wanataka Siasa Safi, Uwajibikaji, Kupambana na Rushwa na Ufisadi, Hali bora Ya Kimaisha, Elimu Bora, Usawa ktk Kugawana Keki Yetu Ya Taifa, Huduma Bora za Kijamii Kuanzia Upatikanaji wa Dawa Mahospitalini, Pembejeo za Kilimo na Maji Salama na Ya Uhakika na Matumizi Mazuri Ya Rasilimali Zetu. Na Siyo Kila Kinachosemwa na Upinzani basi Nyie Mkichukulie Kama ni Chuki au Tusi Kwenu bali Onyesheni Political Maturity Yenu Kwa Kuyakubali Mawazo Yao Kwa Maslahi Ya Nchi Yetu. Leo Nafunguka Kwani Hiki Chama Kimetoka Mbali na Huko Nyuma Hakikuwa Hivi ila Leo ni Fujo na Kero tupu na Kubwa Linalosumbua ni Unafiki na Njaa Kama Si Uroho wa Madaraka. Picha Hiyo hapo Ya Kinana Imenikera Sana haswa Nikiangalia Jamii Yetu Kubwa Inavyoteseka na Hali Ngumu Ya Maisha. Mnaudhi!!!!!!!!!
 
James.L.Laiser Kwa hili ni wazi Lowasa anafanywa kafara. Nilikuwa simuungi mkono Lowasa kwa sasa nimebadili msimamo wangu ninamuunga kwa asilimia mia moja.CCM mmeshindwa kutupeleka katika nchi ya maisha bora kwa kila mtanzania.Msimzingizie Lowasa.Watanzania siyo mbumbu tunaelewa nani ni tatizo.
 
Last edited by a moderator:
===============
Video (On Lowassa):



.
Mbona mna divert attention ya watz,sisi tunataka kuona mawaziri mizigo wamefukuzwa,nape kinana wamezunguka nchi nzima kuwatangazia watz kuwa watawang'oa mawaziri mizigo na sasa mnatapatapa,Kwani lowasa ndo alochagua baraza jipya?? unatumika wewe
 
mtu yeyote ambaye akili ni timamu na anaijua historia ya tanzania na siasa zake hawez kubeza mafanikio ya ccm.

Sawa Tunalikiri hilo ila Usizuie Watu Kufunguka Kwa Uozo Wa Sasa Wa Chama na Ukiona Unasemwa Sana Inaamana Una Tatizo hivyo Yakupasa Kujifanyia Tathmini ili Ubadilike. Kwani CCM ni Msahafu? Mimi Penye Mema Yake Nitapongeza na Pia Wakiharibu Sitosita Kukisema ILA KWA SASA CHAMA KINAKWENDA MRAMA na Wakurya Wana Msemo Wao " MASARE YESAMBUKILE ISAKA NA MOTO " na Wakongo wa DRC Nao Wana Msemo Wao " AZOMATA AZOMATE ". Chama Kina Watu Makini sana ila Hawathaminiwi, Hawasikilizwi na Hawapendwi Pia Kwakuwa Wao Hawapendi Yanayoendelea ndani Ya Chama na JK Asipoangalia Chama Kitamfia na Mzimu wa Mwalimu Nyerere na Karume Utamwangukia. Azimio La Arusha Lirudishwe Nadhani Kidooooooo................go Nidhamu Itarudi ndani Ya Chama otherwise Naona Kifo Rasmi cha Chama Chetu na Mparaganyiko Mkubwa na Haswa ktk Kuanzia na Chaguzi za Awali za Chama Zinazoanza Mwaka Huu na Shughuli Nzima ipo Mwakani 2015.
 
Sijui nikuiteje kwa waraka wako kwasababu yote uliyoyaandika hapa hayana ukweli...

Kwanza umeanza kwa kusema watawala wamekuwa karibu na wananchi..sijaelewa kauli hii kwani wananchi hao ndio waliopandishiwa bei ya umeme na gesi na kujibiwa kama wameshindwa kutumia umeme watumie kibatari? Hapo kero za wananchi zmetatuliwaje??

then tukiangalia upande wa maji kwa mkoa wa Dar es salaam ni kero kuna wilaya au kata maji yanatoka 24 + 7 lakini kuna watu maji wanakunywa ya chumvi mpaka wanapata magonjwa. Hapo kero gani imetatuliwa??

Usilete vineno neno ili ujaze tumbo lako kusema kinana ametatua kero za wakulima na wafugaji wakati baada ya mikutano yao kumetokea mauaji ya kutisha kiteto kati ya wakulima na wafugaji huku waziri mkuu akiwaachia wamalizane wenyewe yeye anadhani walimtaka aende akawaone tu...na hapo je kero zmetatuliwaje?

Tofautisha maneno na utendaji kiukweli Kinana alipata shavu la kutalii mikoani akale ubwabwa na wananchi wasio na akil na utashi wa kujitambua na kujielewa na CCM hupenda watu hao huwatumia na kuwaacha kama walivyo.

Sioni hoja ya msingi kwenye uzi uloleta hapa labda uende ukatoe huu ushauri kwa wapuuzi wenzio Lumumba then next time ukiamua kuandika jaribu kuushirikisha ubongo wako sawasawa.
 
Makonda pamoja na walio nyuma yako nawaambieni anayefaa kuwa rais wa Tanzania ni Lowasa.Tunakumbuka utendaji wake alipokuwa waziri mkuu.Alikuwa mfuatiliaji mkubwa,hakuvumilia uzembe,alikuwa jasiri.Alithubutu kutoa maamuzi magumu kinyume na rais wetu wa sasa ambaye anataka kuwapendezesha watu wote wakati taifa linaangamia.Makonda unaposema hafai inaonyesha jinsi gani umeshindwa kuwaelewa Watanzania wanamtaka nani. Kumbuka mwaka 2005 mlimchafua sana Ahmed Salim.Sasa mmeanza kwa Lowasa.Tumewashtukia
 
Kikwete akitaka kuwatendea haki Watanzania aiwezeshe chadema ishinde uchaguzi 2015 au amkabidhi Ngoyayi mikoba yake...
Haya ndio maonbi yangu kila siku nikumbukapo kumuombea rais wangu JK.
Mungu awe pamoja naye.
 
Lowassa ni kiongozi mvumilivu na mwenye busara sana angalieni wanavyomwandama. Lakini yeye amepiga kimya tu anawatazama! Nachoamini amewasamehe akina Nape kwani hawajui watendalo wasubirie tu 2015 kwani watanzania ndo waamuzi hata wapige domo vipi Watanzania wameshajua kinachoendelea dhidi ya Lowassa! Mungu mwenyewe anajua!
 
James.L.Laiser Ndugu yangu unauliza naniii ya mbuzi wakat mkia unauona?Kwa mila na woga wetu huwezi kumtuhumu kiongozi mkuu wa nchi
 
Last edited by a moderator:
Jamani si mwenyekiti wangu wa taifa pia ni mjumbe wa sekretarieti na isitoshe ndo mwenyekiti wake pia au mi ndo nimebugi.
Kama hali ndo hiyo, inamaanisha wajumbe walifikisha yalioyowajaa mioyoni mwao lakini yeye hakuridhika na akaamua kuendelea na shughuli kama jana kama juzi.
Kumshitaki au kuiunga mkono sekretarieti ni kutupotezea muda na kutokifahamu hiki chama kikukuuuuu. Tafakari
 
Back
Top Bottom