Makonda amepewa rushwa au ni kweli anahitajika?

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Wakati wa utawala wa JK kulikuwa na msemo mashuhuri sana ambao ilisemekana ulitolewa na Rostam Aziz kama ushauri wake kwa JK. Msemo huo ulikuwa unasema " Kwenye udhia penyeza Rupia"

Kusema kweli wakati ule ulikuwa ukitaka tu cheo au fedha kwenye utawala wa JK basi tafuta skendo lipuka nayo siku mbili tatu utasikia umeteuliwa ukuu wa wilaya au umepewa fedha ya kufanya mambo yako unyamaze.

Naona kama Mama kama mwanafunzi mzuri wa JK anaweza kufuata nyayo hizo kuelekea 2025. Watu wote ambao wanaweza kuwa tishio kwake au wapiga domo wanaweza kuwekewa tonge mdomoni ili wasipige kelele kelele.

Makonda kapewa rushwa ili atulie au ni kweli chama kinamuhitaji wakati huu kwa nafasi aliyopewa?
 
Hii ni mbinu ya kutughilb sisi wa Kanda ya Ziwa, lakini tunasema hivi: HATUDANGANYIKI !!!!
 
Makonda kapewa rushwa ili atulie au ni kweli chama kinamuhitaji wakati huu kwa nafasi aliyopewa?
Makonda huyo huyo aliyewahi kumtwanga kofi hadharani Waziri mkuu na Makamo wa rais mstaafu ana uhalali gani wa kuwa kiongozi?!

Wanaosema ccm imepoteza muelekeo wasikilizwe
 
Wakati wa utawala wa JK kulikuwa na msemo mashuhuri sana ambao ilisemekana ulitolewa na Rostam Aziz kama ushauri wake kwa JK. Msemo huo ulikuwa unasema " Kwenye udhia penyeza Rupia"

Kusema kweli wakati ule ulikuwa ukitaka tu cheo au fedha kwenye utawala wa JK basi tafuta skendo lipuka nayo siku mbili tatu utasikia umeteuliwa ukuu wa wilaya au umepewa fedha ya kufanya mambo yako unyamaze.

Naona kama Mama kama mwanafunzi mzuri wa JK anaweza kufuata nyayo hizo kuelekea 2025. Watu wote ambao wanaweza kuwa tishio kwake au wapiga domo wanaweza kuwekewa tonge mdomoni ili wasipige kelele kelele.

Makonda kapewa rushwa ili atulie au ni kweli chama kinamuhitaji wakati huu kwa nafasi aliyopewa?

Mkuu hulka na tabia ya Makonda ya kutumika bila ya yeye kuona aibu au kuhoji. Kumbuka Alivyo tumika kipindi cha JK na JPM.

Walioamua kumuweka hapo kwenye uenezi wanao ushahidi wa maovu yote aliyoyafanya kipindi cha Mwendazake.

Kwa ushahidi huo, unamlazimisha Makonda afuate maelekezo/maagizo yao bila kuhoji wala kukwepa.

Makonda ni mzuri kutumika kwa kufuata maagizo na maelekezo bila kuhoji.

Kutokana na hali hiyo naona amepewa maagizo na maelekezo ya kufanya siasa za kiungwana au kistaraabu maana uthubutu na uwezo huo anao.

Pamoja na hayo karata ya kanda ya ziwa imezingatiwa hasa uhusika na ushawishi wake katika kundi la wafuasi wa Mwendazake.
 
Hivi kweli una akili timamu upige kura kwa sababu Makonda ni mtu wa kwenu?
 
Kama una akili timamu fuatilia watu waliokuwa wanamsapoti makonda zama za uongozi wake.... T.i.d!!, Shishi baby, Haromnize.
 
Back
Top Bottom