MachoMakavu
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 367
- 44
Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda leo alikutana na waandishi wa habari baada ya kuahirisha Bunge kutolea ufafanuzi suala la posho na tamko la serikali bungeni kuhusu mgomo wa madaktari.
Katika mkutano huo, Spika kadai kwamba watanzania wengi wanadhani wabunge hulipwa posho za kila siku kwa siku zote 365 za mwaka, jambo ambalo si kweli. Posho hizo hutolewa pale tu wanapokua na mikutano ya bungeni Dodoma.
Spika pia kafafanua kwa nini Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu mgomo wa Madaktari bungeni. Kwa maelezo yake, Spika anaeleza kwamba tamko hilo ni lazima liandaliwe kwa maandishi, wabunge wote wagawiwe na kulipitia kabla ya kusomwa rasmi. Mchakato wa kuliandaa bado unaendea wizara ya afya na baada ya wabunge kugawiwa tamko hilo litajadiliwa.
Source: Taarifa ya habari TBC saa 2 usiku.
Hivi tuna kiongozi hapo?